Mapema
wiki iliyopita Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilitembelea miradi ya
maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini ili kukagua utekelezaji wake.
Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha kuzalisha samaki Morogoro, Skimu ya
Umwagiliaji Iringa vijijini, Maghala ya COWABAMA Iringa Vijijini, Ujenzi
wa Barabara ya Iringa – Dodoma, Bwawa la Mtera, Ujenzi wa Barabara ya
Manyoni – Itigi, utandikaji wa Reli eneo kati ya Kitaraka na Malongwe,
Shamba la Kitengule, One Stop Border Post Mutukula, Mkongo wa Taifa
Mutukula na Upanuzi wa mradi wa maji safi, Bomba Kuu la Ziwa Victoria.
Katika
kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo
kwa kuzielekeza Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za
utekelezaji kila robo mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya
maendeleo kuona hali halisi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini
mafanikio na changamoto na hatimaye kutoa ushauri katika ngazi husika
kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Moja
ya Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa
Sasa (MMS) na miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Miradi imeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano
(2011/12 – 2015/16) na ile ya Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika
mfumo wa kimaabara.
Naibu
Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa
nne kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kushoto) na
maafisa kutoka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pamoja na wataalam
wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Samaki kilichopo Kingolwira Mkoani
Morogoro wakiangalia sehemu maalum ya kukuzia vifaranga vya samaki baada
ya kutotoleshwa.
Naibu
Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri
(wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kulia)
pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo
kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma, hatua ulipofikia
na changamoto zilizopo kutoka kwa Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de
Kock (mwenye kofia).
Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri
(wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma
inavyoendelea wakati alipotembelea mradi huo pamoja na maafisa kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Pamoja nao ni Mtaalamu Elekezi wa mradi
Bw.Robin de Kock (mwenye kofia katikati).
Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa pili kushoto) pamoja na
maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipewa maelezo kuhusu
bwawa la kuzalisha umeme la Mtera kutoka kwa Meneja wa Kituo Bw.
Abdallah Ikwasa (wa nne kushoto). Hii ni sehemu ambapo uzalishaji wa
umeme unafanyika. Bwawa la Mtera linapatikana katika mikoa ya Iringa na
Dodoma. Lina uwezo wa kuzalisha MW 80 ambao unaoingizwa katika Gridi ya
Taifa.
Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(wa kwanza kushoto) na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa reli kutoka Kitaraka hadi
Malongwe mkoani Tabora kutoka kwa Bw. Raphael Mwandumbya (mwenye kofia)
ambaye ni Mkaguzi wa ujenzi wa reli hiyo. Mradi huu ni sehemu ya ujenzi
na ukarabati unaoendelea katika Reli ya kati ambao una urefu wa kilometa
89.
Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kushoto) na
maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiangalia uharibifu wa
barabara ambao unafanywa na wananchi wasio waaminifu kwa kuchota kokoto
pembezoni mwa barabara hiyo ambayo bado inaendelea kujengwa. Barabara
hii inajengwa na Nicholas O’Dwyer & company Ltd Consulting Engineers
ambapo kipande cha Manyoni hadi Itigi kipo katika hatua za mwisho
kukamilika. Lengo la mradi ni kuendelea kujenga barabara ya Manyoni –
Itigi kwa kiwango cha lami katika sehemu tatu za utekelezaji ambazo ni:
Manyoni – Itigi – Chaya (KM 89.35), Chaya - Nyahua (KM 90), na Nyahua –
Tabora (KM 85).
Jengo
kwa ajili ya kutolea huduma za mpakani (One Stop Border Post) Mtukula,
mradi ambao unahusisha ujenzi wa miundombinu inayosaidia utolewaji wa
huduma bora na za kisasa mpakani mwa Tanzania na Uganda. Lengo la mradi
wa One Stop Border Post ni kukamisha vituo vya utoaji huduma za pamoja
mipakani kati ya Tanzania na nchi za jirani.
Timu
ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(wa tatu kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wanaohusika na
Mkongo wa Taifa. Lengo la mradi kwa mwaka 2014/2015 ni mapitio ya
miundombinu ya Mkongo na mifumo kwa ajili ya maboresho, ujenzi Awamu ya
III sehemu ya kwanza ya upanuzi wa mkongo kwa maeneo yaliyobaki katika
awamu I na II na uhakiki wa ubora wa Mkongo.
Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara Mipango na Ufuatiliaji,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omary Abdallah (wa kwanza kulia) na
wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kuhusu
mafanikio na changamoto za Mradi wa Ranchi ya Taifa Misenyi kutoka kwa
Meneja wa Mradi Bw. Martin Ladislaus (katikati). Shamba hili la mifugo
lipo Karagwe, mkoa wa Kagera. Ni moja kati ya mashamba makubwa 9 nchini
ya uwekezaji, limepimwa na kupata hati miliki.
Ujumbe
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ukiongozwa na Naibu Katibu
Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (mwenye
t’shirt nyeusi) wakiangalia sehemu ya kuogeshea ng’ombe. Wengine ni
Meneja wa Mradi Ranchi ya Taifa Misenyi, Kagera Bw. Martin Ladislaus (wa
tatu kulia) na Meneja wa Mradi Ranchi ya Kitengule, Kagera Bw. Hemedi
M. Seif (wa pili kulia).
EmoticonEmoticon