Katibu wa vijana umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha
mjini Jamali Khimji akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema
Kiusa(27)katika ofisi za umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana
kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama
cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido
akionyesha fomu aliyochukua leo.
Neema Kiusa(27)ambaye ni mgombea ubunge viti maalumu
kupitia chama cha Mapinduzi akiwa na mumewe Andrea Shija, pia ni mama
wa mtoto mmoja
Neema Kiusa(27)Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama
cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido
akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha baada ya
kuchukua fomu .
…………………………………….
Mgombea ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa
leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa
Arusha,ambapo amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa
kutatua changamoto ya ajira
Neema ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya
Longido alisema kuwa ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya
muda mrefu sana hivyo endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana
bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arushaa
Pia mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake anayempa
ushirikiano mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo
aliwataka wanaume wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo
wataonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi
Kwa upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha
mjini Jamali Khimji amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza
kwa wingi kuchukua fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana
katika mkoa wa Arusha
Khimji alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua
fomu ya kuwania nafasi hiyo ni kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na
awe ametimiza vigezo vya chama hicho
EmoticonEmoticon