NHIF WAKABIDHI MASHUKA 400 HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA TEULE.

July 08, 2015
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugen Mikongoti akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Muheza,Esteria Kilasi wakati walipokwenda kukabidhi mashuka 400 kwa hospitali ya wilaya ya Muheza Teule.

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.



Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugen Mikongoti akimkabidhi mashuka 400 mkuu wa wilaya ya Muheza,Esteria Kilasi kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Muheza Teule ambayo inakabiliwa na uhaba wa mashuka

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akipanga mashuka walioyakabidhi kwa hospitali ya wilaya ya Muheza Teule ambapo walikabidhi mashuka 400 kwa ajili ya wagonjwa wanaokwenda kulazwa

HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza mkoani Tanga inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa mashuka kwa wagonjwa hali ambayo inawalazimu kubeba kwa ajili ya kujifunika wakati wakiwa wodini.
Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeweza kusaidia kutoa mashuka 400 zenye thamani ya shilingi milioni saba(7000,000) kwa lengo la kulipatia ufumbuzi  tatizo hilo.

Akizungumza jana mara baada ya kupokea msaada huo wa mashuka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugen Mikongoti, Mkuu wa wilaya ya Muheza,Esteria Kilasi aliwashukuru kwa kuipatia hospitali hiyo msaada huo ambao utasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa mashuka waliokuwa nayo.

Alisema kuwa msaada huo ambao umetolewa na mfuko huo umefika kwa wakati muafaka na hivyo kuhaidi kuutumia katika matumizi yaliyokusudiwa kwenye maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa mashuka ili waweze kupata.
   
“Mimi binafsi niwashukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa msaada huu kwa hospitali kwa sababu hali ya mashuka ilikuwa sio nzuri kwa wodi kwani baadhi ya wagonjwa wanalazimika kutumia ya kwao“Alisema DC Kilasi.
Aidha alishukuru kwa kupewa mkopo wenye masharti nafuu ambao utalipwa kwa miaka miwili kwa ajili ya ukarabati wa wodi zilizokuwa na uchakavu lengo likiwa kuziboresha ili huduma zinazotolewa ziweze kuwa bora.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti alisema kuwa lengo lao mfuko huo ni kuhakikisha vituo vilivosajiliwa kutoka huduma kwa wananchi vinapata mikopo hiyo rahisi ambayo wanaitoa.

Alisema kuwa waliona watoe mikopo ya vifaa tiba, ukarabati wa majengo na dawa kwenye  hospitali na vituo vya Afya kwa lengo la kusaidia kuweza kukabiliana na changamoto walizonazo ili waweze kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.

Eugeni ambaye ni Mkurugenzi anayesimamia Mfuko wa Afya ya Jamii alisema kuwa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kila mwaka wanatenga shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kutoa vifaa tiba wakikusudia kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Naye,Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga,Ally Mwakababu alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Muheza zinafanya vizuri sana katika eneo la afya kitendo ambacho kinapeleka kutoku kosekana dawa kwenye vituo mbalimbali.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »