Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser .
Shear
Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa
kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP
Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia
vipodozi.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.
Shear
Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa
kitanzania kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa,
nywele, vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya
urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali
mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.
LuvTouch
Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania.
Kuna aina kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na
ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi
vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.
Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI, Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha
Nasser Katikati akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea
Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga
kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa
Kitanzania.Mpango Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia
vipodozi..Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu
Pinda
Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu
Ndolvu Akieleza jambo leo wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi
huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Pamoja na Aunty Sadaka Gandi
Aunty
Sadaka Gandi akiwa ni dada mkuu wa Atakayewashauri wasichana
watakaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia Manjano Foundation.
EmoticonEmoticon