Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii
Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo wakati
akiongea na watoto pamoja na walezi wa kituo cha Malezi na Makuzi ya
Watoto cha Mtambani, Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.
(Picha zote na Hassan Mabuye)
Baadhi ya watoto wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani wakiwa katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo
wakati akiongea na wanachuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
Wanachuo cha Maendeleo ya
Wananchi Kibaha pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya
pamoja na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa
Dkt. Pindi Chana.
………………………………………………..
Na Hassan Mabuye
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana amefanya ziara ya
kutembelea kituo cha kulelea Watoto Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kwa
lengo la kuangalia maeneo ambayo yanahitaji maboresho pamoja na kujionea
hali halisi ya uendeshaji wa vituo vya kulelea Watoto.
Katika ziara hii Mheshimiwa
Naibu Waziri alitembelea kituo cha Malezi na Makuzi ya watoto Kilichopo
katika kata ya Mtambani Mlandizi jumatatu tarehe 27 Aprili 2015, ambapo
aliongea na Walezi na wasimamizi kukienzi na kukitunza kituo hicho.
Aidha Mheshimiwa Pindi Chana amewahusia wasimamizi na wazazi kuyapa
kipaumbele mambo yanayohusu Watoto kuanzia kwenye familia na kuyaweka
katika bajeti za kila siku za familia kwani taifa la kistaarabu
linajengwa kuanzia kwa watoto wadogo.
Mheshimiwa Naibu Waziri
alifanikiwa pia kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Kibaha ambapo aliwahusia vijana kuzingati masomo yao wakati wazazi bado
wana nguvu za kuwasomesha. “Unadhani siku hizi ukikimbia shule au
kutoroka masomo unamkomoa nani, mzazi au mwalimu? Unajikomoa mwenyewe
sababu baadae wewe ndo utabeba majukumu na pengine ndio utakuwa mzazi na
maisha ya sasa ni elimu na ujuzi” alisisitiza Mhe. Pindi Chana.
Aidha Mheshimiwa Pindi Chana
katika ziara hii alikutana na vikundi vya Wanawake walionufaika na
mikopo inayotolewa na Benki ya Wanawake Tanzania eneo la Picha ya Ndege
Kibaha.
EmoticonEmoticon