MAGWIJI WA KLABU YA BARCELONA WAANZA KUWASILI NCHINI

April 05, 2015

Nguli wa soka wa timu ya taifa ,Uholanzi na vilabu vya Ajax na Barcelona,Johan Cruyff (Kulia) akiongozana na mwenyeji wake,Rayco Garcia mara baada ya kuwasili katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)


Dixon Busagaga (Kushoto) wa Globu ya Jamii na Busagaga's Orijino Blog akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa ziara hiyo ya magwiji wa Barcelona.


Mratibu wa ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona nchini ,Royco Garcia ,(kulia) akiwa na mdau wa soka wa mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Hai,Harold Kifunda wakati wa mapokezi ya gwiji wa soka wa timu ya taifa ya Uholanzi na vilabu vya Ajax na Barcelona.


Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii akizungumza jambo na mratibu wa ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona nchini ,Royco Garcia ,uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro  wakati wa ujio wa gwiji wa soka wa timu ya taifa ya Oholanzi na vilabu vya Ajax na Barcelona, Johan Cruyff.


Na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog..

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na vilabu vya ,Ajax na Balcelona,gwiji Johan Cruyff amewasili jana majira ya saa 4:45 za asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo ,Cruyff akiwa ameambatana na familia yake alipokelewa na Rayco Garcia ,mratibu wa ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania watakao cheza mechi ya kirafiki dhidi ya wakongwe wa soka hapa nchini jumamosi ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo,Cruyff alisema anafurahi kufika Tanzania kwa mara ya kwanza na kwamba amefurahia hali ya hewa ya Joto ukilinganisha na nchi anayotoka ambayo kwa sasa ni msimu wa baridi.

Alisema ana matarajio makubwa baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania ikiwemo kuona wanyama wa aina mbalimbali katika hifadhi ya taifa ya Serengeti pamoja na kutembelea fukwe za bahari katika kisiwa cha Zanzibar kabla ya mchezo huo wa kirafiki.

“Nasikia furaha kufika Tanzania,na hali ya hewa ni nzuri,hali  ya joto,tunategemea kutembelea maeneo mengi ya vivutio ,tunaenda kutizama wanyama katika hifadhi ya Serengeti na baadae kutembea fukwe huko Zanzibar,tunategemea kuona vitu vingi vizuri.”alisema Cruyff.

Kuhusu mchezo wa Jumamoshi ,Cruyff alisema mashabiki wategemeee burudani toka kwa wakongwe hao wa Barcelona na kwamba mchezo huo hautakuwa wa ushindani isipokuwa wataonesha burudani ambayo ni matarajio ya wengi.

“Kitu cha kwanza ni kwamba mashabiki watapata Burudani,hatutacheza ili kushinda ingawaje tutapenda kushinda ,lakini kikubwa ni kutoa burudani kwa mashabiki,wafike tu uwanjani kufurahia mchezo”alisema Cruyff.

Cruyff ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’O ,1971,1973  na 1974 aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma katika mazoeizi ni kuzingatia maelekezo ya walimu ili kujenga morali ya timu na wachezaji kwa ujumla.

“Naweza sema kwa wachezaji pekee ,wanapaswa kufanya mazoezi kwa bidii,wajaribu kujiweka vizuri kila mara,na kitu kizuri katika michezo ni umoja wa timu ,mkishinda mnashinda pamoja na mkipoteza mnapoteza pamoja”alisema Cruyff.

Kuelekea katika Pambano la Jumamosi tayari waratibu wa mashindano hayo walisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba baadhi ya wachezaji wa Barcelona watakao shuka uwanjani siku hiyo ni pamoja na wakongwe Edaga Davis ,Deco,Patrick Kluivert na Simao Sabrosa.

Historia ya Cruyff.
Mdachi Hendrik Johannes Cruijff alizaliwa Aprily 25 mwaka 1947 katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi, akajulikana kama Johan Cruyff ambaye hadi sasa ni meneja wa klabu ya Catalonia ya nchini Hispania.

Cruyff ni miongoni mwa wachezaji maarufu walio anzisha falsafa ya Total Football ambayo ilienea kote duniani hatua iliyopelekea kuwa mmoja wa wachezaji wenye sifa kubwa katika historia ya soka duniani.

Cruyff alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za kombe la dunia la Fifa ,mwaka 1974 ambapo alifanikiwa kupata zawadi ya mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa mashindano.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »