Mshinda
wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)akikabidhiwa
hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘JayMillions’
baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo
katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka.Makabidhiano hayo
yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa
Tamasha la Mwana Dar Live lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili
mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda
namba 15544.
Balozi
wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary
Daud ‘Jaymillions’akiwasomea tarakimu kwenye hundi iliyokuwa na thamani
ya shilingi milioni 10/-wakazi wa mbagala waliofika katika tamasha la
Mwana Dar live lililofanyaika katika ukumbi wa Dar live mbagala jijini
Dar es Salaam katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka,Hundi hiyo
ilikabidhiwa kwa mshindi wa promosheni hiyo Shamila
Ramadhani(kusho)akiambatana na mumewe Abdallah Mahoka(katikati) Ili
mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda
namba 15544.
Mshinda
wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)pamoja na
mumewe Abdallah Mahoka wakiinua hundi yao juu ili wakazi wa mbagala
waliohudhuria tamasha la Mwana Dar Live waione baada ya kukabidhiwa
rasmi na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud(hayupo pichani) baada ya
kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo.Makabidhiano
hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa
Tamasha hilo lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua
kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwapagawisha washabiki wa muziki
wake waliofurika katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na
Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika
katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mamaa
Aisha Mashauzi akitumbuza muziki wa Taarabu katika Tamasha la Mwana Dar
Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya
pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es
Salaam.
Msanii
wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”akisaga sumu ipasavyo
kwa washabiki wa muziki wake wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live
lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka
na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wapenzi
wa burudani ya muziki wa kizazi kipya na muziki wa taarabu wamepata
burudani ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kutoka kwa magwiji wa muziki
wa kizazi kipya na taarabu katika matamasha ya burudani yaliyoandaliwa
na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania yaliyofanyika Coco Beach na Dar
Live ,Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tamasha
la wazi lililofanyika Coco beach liliwavutia wakazi wengi wa jiji
hususani vijana pia kuhakikisha watoto hawaachwi nyuma nao waliandaliwa
burudani zao ambapo waliweza kucheza na kufurahia sikukuu ya Pasaka.
Wasanii
wa kizazi kipya Bob Junior na Shilole waliacha historia ya aina yake
kwa mamia ya washabiki wa muziki wa kizazi kipya waliofika katika fukwe
ya Coco kwa jinsi walivyoweza kukonga nyoyo zao na kudhihirisha kuwa
muziki wao ni wa kiwango cha juu pia walikuwepo wasanii mbalimbali
chipukizi ambao pia walimwaga burudani kwa mashabiki.
Funga
kazi ilikuwa Dar live Mbagala ambapo msanii mahiri wa Bongofleva Ali
Kiba kwa kushirikiana na mwanamama anayetamba katika muziki wa taarabu
nchini Aisha Mashauzi walimwaga burudani za aina yake na kupagawisha
washabiki waliofika katika tamasha la Mwana Dar Live ukumbini hapo
kusherehekea sikuu ya Pasaka.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa kampuni yao
imeamua kuandaa na kudhamini matamasha haya kwa ajili ya kuwapatia
furaha na burudani wateja wake na wananchi kwa ujumla katika msimu huu
wa sikukuu ya Pasaka na kuweza kuwakutanisha washabiki na wanamuziki
wawapendao na itaendelea kufanya hivyo kupitia promosheni ya Ishi Kistaa
na aliwakumbusha wateja kutuma neno STAR kwenda namba 15670 ili wapate
fursa ya kuwakutanisha na wasanii wawapendao.
“Kama
ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “ukiwa na Vodacom maisha ni
murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia
tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana
tunaandaa na kudhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya
hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu
kwa kutuunga mkono”Alisema.
EmoticonEmoticon