AINGIA KANISANI NA BASTOLA YANYE RISASI 8-KISARAWE...POLISI WA MKAMATA

April 05, 2015

Hofu‬ imewakumba waumini wa ‪Kanisa‬ ‪Katoliki‬ la Mtakatifu Stephano, ‪‎Kisarawe‬ mkoani ‪‎Pwani‬ katika ibada ya Ijumaa Kuu baada mtu mmoja kukamatwa katikati ya ibada ya Ijumaa Kuu akiwa na bastola yenye risasi nane.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka kwa waumini na kuthibitishwa na polisi, mwanaume huyo ambaye si muumini wa kanisa hilo anadaiwa kutaka kufanya uhalifu kanisani hapo na alikamatwa baada ya waumini kushtukia mienendo yake isiyo kuwa ya kawaida.
Tukio hili limetokea katika kipindi ambacho kuna tishio la uhalifu unaohusishwa na ‪‎ugaidi‬ katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo kuna uporaji wa silaha unaofanywa na watu wasiojulikana baada ya kuwaua polisi.
Vilevile tukio hili limetokea wakati waumini hao hawajasahau mauaji ya kutisha nchini ‪Kenya‬ ambako magaidi wamevamia Chuo Kikuu cha ‪‎Garissa‬ na kuua wanafunzi 147.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »