Madereva
nchini wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani,kutotumia vinywaji
vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea
ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,
katika kampeni ya uhamasishaji wa usalama barabarani iliyozinduliwa leo
na serikali kupitia Jeshi la polisi,Baraza la Taifa la Usalama
barabarani na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania eneo la Mwenge
jijini Dar es Salaam ambapo pia alishiriki katika zoezi la kuwagawia
madereva pete maalum za kuwakumbusha kutotumia simu za mkononi
wanapokuwa wanaendesha magari na pikipiki.
Alisema
madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali
zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua hususani katika kipindi hiki
kuelekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na aliipongeza Vodacom
Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na
tatizo hili ambalo limekuwa sugu .
Naye
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la Polisi,Kamanda
Mohamed Mpinga amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya
ajali “Watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto
hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni
hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama
ilivyokusudiwa”Alisema
Kwa upande wake,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Umma wa
Vodacom,Rosalynn Mworia, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na
serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama
lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha
murua na marefu.
”Tunaomba
madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu,usalama wa
abiria mnaowabeba na watumiaji wengine wa barabara".
Aliongeza
kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za
kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni
ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia
sheria za usalama barabarani.Mbali na kampeni hii alisema kwa mwaka huu
kampuni ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Alisema
kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa
madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es
Salaam,Mwanza na kampeni itaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika
uzinduzi huu wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa
usalama barabarani walitoa uhamasishaji wa madereva kuacha kuongea na
simu wanapoendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini
kama wanatumia vilevi lilifanyika.
Waziri
wa Mambo ya Ndani Mh.Mathias Chikawe (watatu kutoka kulia) akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika
eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi
jijini Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango
cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za
kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto,wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia,
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed
Mpinga,mwenyekiti wa usalama barabarani wilaya ya Kinondoni Hua
Tluway,wapili (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani Hamza Kassongo na Henry Bantu

wa Mambo ya Ndani Mh.Mathias Chikawe (wapili kutoka kulia) Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn
Mworia, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda
Mohammed Mpinga,mwenyekiti wa usalama barabarani wilaya ya Kinondoni Hua
Tluway,wapili (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani Hamza Kassongo na Henry Bantu (kulia) wakishangilia baada ya
uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge
makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es
Salaam, uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe
mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva
kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Waziri
wa Mambo ya Ndani Mh.Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn
Mworia, wakati alipokuwa akimuelezea matumizi ya pete maalumu za
kidoleni ambazo huwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi
wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya
Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam, uzinduzi huo
uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva Kushoto
ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed
Mpinga Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza
Kassongo na Henry M. Bantu (kulia) na Mjumbe wa baraza hilo Hamza
Kasongo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Mathias Chikawe (kushoto) akimuonyesha dereva
wa pikipiki pete zenye ujumbe wa “Wait to Send” wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya
barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam,
uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa
madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha
kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.wengine
wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga
Waziri
wa Mambo ya Ndani Mh.Mathias Chikawe (kushoto) akishuhudia dereva wa
pikipiki akivalishwa pete zenye ujumbe wa “Wait to Send”
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo
la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi
jijini Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na upimaji wa kiwango
cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za
kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto.wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga

Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga
akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya usalama barabarani iliyozindiliwa na Waziri wa Mambo ya
Ndani Mh.Mathias Chikawe katika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya
Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam leo, uzinduzi huo
uliambatana na upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na
ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za
mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
EmoticonEmoticon