KIKOSI CHA FRIENDS RANGERS LEO. |
NA MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU za Soka Friends Rangers ya Dar es Salaam na African
Sports “wanakimanumanu” leo zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimishana sare
ya kufungana bao 1-1,ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi daraja la Kwanza inayoendelea kutimua vumbi kwenye maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Mechi hiyo ilichezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na
kushuhudiwa na wadau wa soka mkoani hapa kutoka maeneo mbalimbali.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani huku
timu zote zikionekana kushambuliana kwa zamu ambapo mpaka timu zote zinakwenda
mapumziko Friends Rangers walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na
Iddi Ismaili baada ya kupokea krosi iliyopigwa na Credo Dancan upande wa
magharibi.
Bao hilo liliweza kudumu mpaka timu zote zinakwenda
mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutokana na timu kufanya
mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji wake hali ambayo ilipelekea kucheza kwa
kujiamini na kucheza kwa umakini ikiwemo mashambulizi ya hapa na pale.
Wakionekana kujipanga vizuri,Friends Rangers waliweza
kutulia na kuanza kufanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa African Sports kwa
dakika kadhaa lakini bahati haikuweza kuwa yao baada ya wachezaji wake kupiga mashuti
makali yaliyokuwa yakipaa juu ya lango la wapinzani wao hao.
Hata hiyo timu hiyo iliweza kuendeleza wimbi la mashambulizi
langoni mwa African Sports mithili ya mbogo aliyejeruhiwa na hatimaye kuweza
kupata bao la kusawadhisha katika dakika ya 84 kupitia Maulid Abasi ambaye
alitumia uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuni bao hilo.
Akzungumza mara baada ya kumalizika,Kocha wa Friends
Rangers,Ally Yusuph Tigana alisema kuwa wanamshukuru mungu kwa kuweza kupata
pointi moja wakiwa ugenini ambayo itawasogeza kwenye nafasi ya juu kwenye
msimamo wa Ligi hiyo.
“Tunamshukuru
mungu kuweza kupata pointi moja ugenini hii ni muhimu sana kwetu tutakwenda kujipanga ili
kuhakikisha tunapata matokeo mazuri mechi yetu inayofuata “Alisema Tigana.
EmoticonEmoticon