*WAREMBO WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2014 WATEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI

September 18, 2014

 Warembo wanaotarajia kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2014 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya taifa Mikumi jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 
 Kaimu Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Apaikunda Mungure, akiwagawia vipeperushi warembo wa shindano la Miss Tanzania 2014 walio tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani. Vipeperushi hivyo vina taarifa mbalimbali za hifadhi hiyo ya taifa. 
 Kaimu Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Apaikunda Mungure akiendelea kugawa vipeperushi kwa warembo hao. 
 Mwongoza watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Benina Mwananzila  akiwapa maelezo  warembo wa Miss Tanzania 2014 juu ya bwawa la viboko na mamba lililopo katika hifadhi hiyo wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 

Warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2014 wakiwa katika Camp ya Mbuyu iliyopo katika hifadhi ya taifa Mikumi jana walipotembelea hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 
Picha na Mpigapicha wetu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »