Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey
Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa
sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini
Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki
Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey
Mlimuka akiwapongeza Vijana wanaounda kundi la The Voice ambao ni
wasanii wa fani ya Akapela mara baada ya Kutoa burudani katika sherehe
ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki
katika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
Kundi
la The Voice likitoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa
Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue
Pearl
Baadhi
ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia matukio
yaliyokuwa yakiendelea katika Sherehe ya Mwaka ya Wafanyakazi wa Mfuko
wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Blue
Pearl.
Afisa
Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti
na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa
mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya
Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika
mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam
Pichani
Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa
Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka
2013.
Wafanyakazi
wa PPF wakifuatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la The Voice
katika Sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika
Hotel ya Blue Pearl.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akimtunza Mmoja ya waimbaji
wa kundi la the voice lililokuwa likitoa burudani wakati wa sherehe ya
Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Mwisho mwa Wiki katika
hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar
Wadau
wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na
zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki
katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.Pichote na
Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
EmoticonEmoticon