MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Mrisho Gambo, amesema
wilaya yake imetekeleza agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa asilimia
65.
Gambo aliyasema hayo hivi karibuni katika ya kutembelea ujenzi wa
vyumba vya maabara unaoendelea katika kata mbalimbali wilayani hapa na
kueleza kuwa wilaya hiyo ipo kwenye hatua nzuri ya makusanyo ya
michango ya wananchi ambapo Novemba mwaka huu tatizo la maabara
litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Lucas Mweri, alisema
mtendaji atakayeshindwa kusimamia kazi hiyo atakatwa mshahara wake, ili
aone umuhimu wa na unyeti wa jambo hilo kwa maslahi ya kizazi cha sasa
na kijacho.
Diwani wa kata ya Mazinde, Abdalah Mangare, alisema wananchi wameona
umuhimu wa ujenzi wa vyumba vya maabara na kukubali kuchangia.
Chanzo Tanzania Daima
EmoticonEmoticon