Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa
heshima za mwishomapema jana katika viwanja vya Leaders kwa mwili wa
msanii wa Filamu nchini Marehemu Adam Philip Kuambiana aliyefariki
ghafla mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mjane
wa marehemu Adam Kuambiana, Bi. Janeth Rite akiwa katika wakati mgumu
kutokana na kushuhudia mwili wa mme wake ukiwa katika jeneza.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa
salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali, kwa familia, ndugu, jamaa na
marafiki wa marehemu Adam Philip Kuambiana wakati wa shughuli za kutoa
heshima za mwisho kwa marehemu iliyofanyika leo katika viwanja vya
Leaders jijini Dar es Salaam, kushoto ni mjane wa marehemu Bi. Janeth
Rite.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso akitoa
salamu za rambirambi kwa niaba ya Bodi ya Filamu kwa familia ya marehemu
Adamu PhilipKuambiana aliyekuwa msanii wa Filamu na mkurugenzi wa
Kampuni ya kutengeneza filamu ya APK akiyefariki ghafla siku ya jumamosi
kutokana na ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akitoa salaam za rambirambi
kwa niaba ya Manispaa ya Kinondoni ambapo mjane wa marehemu Adam
Kuambiana anafanyakazi kama Diwani wa Kata ya Kunduchi. ,kushoto
katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara na mjane wa marehemu Mhe. Janeth Rite
Msanii
wa Muziki wa injili na Bongo Flava Stara Thomas akiimba kwa hisia
wakati wa shughuli ya kutoa heshi za mwisho kwa mwili wa marehemu Adam
Kuambiana leo katika viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere akitoa salaam
za rambirambi kwa niaba ya Bongo Movie wakati wa shughuli za kutoa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Adam Philip Kuambiana.
Msanii
wa Filamu Jacob Steven – JB akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa marehemu
Adam Kuambiana katika tasnia ya Filamu nchini,katika maelezo yake JB
amesema kuwa Adam alikuwa injini katika sanaa ya filamu hivyo ni pengo
kubwa ambalo hajui litazibika namna gani.
Msanii
wa Filamu nchini Wema Isack Sepetu akiwa katika majonzi makubwa wakati
wa shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa msanii mwenzake
marehemu Adam Philip Kuambiana iliyofanyika katika viwanja vya Leaders
jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili
wa marehemu Adam Kuambiana wakiwa katika taswira mbalimbali.
Picha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini-WHVUM
EmoticonEmoticon