CHAMA cha ngumi za Ridhaa Mkoa wa Tanga,(TBA)kimeanza mkakati kabambe wa kuhakikisha mchezo huo unaenea katika wilaya mbalimbali mkoani hapa kwa kuunda timu ya mkoa ambayo itashirikisha wilaya zote.
Akizungumza jana,Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Tanga,Mansour Soud alisema timu hiyo itakuwa ikiuwakilisha mkoa huu kwenye mashindano mbalimbali ya mchezo huo ikiwa na matumaini ya kulitangaza vema jina la mkoa.
Soud alisema licha ya hivyo wameanza mchakato wa kutembea kila wilaya kwa ajili ya kuzindua vilabu vya mchezo wa ngumi kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na mbili lengo likiwa kuinua vipaji vyao na hatimaye kuukuza mchezo huo.
Alisema timu ya mchezo huo ya mkoa ipo kwenye maandalizi mazuri ya kujiandaa na mashindano ya majimaji yatakayofanyika Songea mkoani Ruvuma mwishoni mwa mwezi Julai ikiwemo mashindano ya klabu bingwa ya mchezo huo.
Aidha alisema mashindano ya klabu bingwa huenda yakafanyika mkoani Kigoma ambapo mabondia wanaocheza ngumi za ridhaa mkoani hapa watakuwa wakishiriki endapo hatutakuwepo kwa mabadiliko ya aina yoyote ile.
Hata hiyo aliwapongeza mabondia wane wa mkoa wa Tanga ambao
walifanikiwa kupata medala za dhahabu na fedha kwenye mashindano ya kumuenzi Rais wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela yaliyofanyika jijini Dar s Salaam mwezi uliopita.
Aliwataja mabondia hao kuwa ni Mohamed Kidari ,Ally Bosnia,Patric Mweri ambao waliwakilisha vema mkoa huu kwenye mashindano hayo.
Katika hatua nyengine mwenyekiti huyo alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo na sehemu ya kufanyia mazoezi kwa mabondia kitendo.
Aliyaomba makampuni na wahisani kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje kujitokeza kuwasaidia ili waweze kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo kurudisha historia ya mchezo huo mkoani hapa.
EmoticonEmoticon