Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu
Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian
Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo
jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian
anatarajiwa kuzikwa kesho mchana(Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu
ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati
alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es
Salaam leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi
ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu
ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao
Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuifariji familia ya Marehemu
Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es
Salaam leo(picha na Freddy Maro)
EmoticonEmoticon