Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), Eliud Mvella
amejiunga na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Amejiunga
na Sekretarieti ya TFF katika Idara ya Sheria na Vyama Wanachama kuanzia leo (Mei
21 mwaka huu) ambapo atashughulikia masuala ya wanachama.
Mvella
alijiuzulu rasmi wadhifa wake IRFA jana (Mei 20 mwaka huu). Mwenyekiti wa IRFA,
Cyprian Kwihyava amepokea barua ya kujiuzulu huko ambapo ameelezea masikitiko
yake kwa uamuzi huo wa Mvella.
Ni
imani ya TFF kuwa Mvella atatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi wa
mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha uhusiano wake na wanachama wake.
TFF
ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
EmoticonEmoticon