Na Masanja Mabula - Pemba .
Wakongwe wa soka Kisiwani Pemba Timu ya Jamhuri ya Pemba imebainika kuwa ni moja ya vilabu vinavyongoza kuwafuta kazi makocha wake ambapo kwa kipindi cha miaka mitano klabu hiyo imewahi kufundishwa na makocha watano .
Utaratibu huo wa kuwafukuza makocha wanaoifundisha klabu hiyo , huenda ikawa ndiyo sababu ya kuifanya ishindwe kufanya vyema kwenye ligi kuu ya soka Visiwani Zanzibar kwani wachezaji wameshindwa kushika mbinu na kocha ambao wamekuwa hawadumu na kikosi .
Timu hiyo ambayo ni ya kwanza kuwahi kuchukua ubingwa wa ligi Kuu wa Zanzibar kwa timu za kutoka Kisiwani Pemba , msimu uliopita ilifundishwa na Kocha Salum Bausi ambaye muda mfupi alibwaga manyanga kwa kile alichodai kupingana na uopngozi wa klabu hiyo .
Bausi ambaye kwa sasa ni kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar , aliicha timu ya Jamhuri baada ya kubaini uswahiba uliopo kati yake na timu ya Mafunzo ya Mjini Unguja .
Kocha mwengine aliyewahi kuifundisha na kuipa mafanikio ni Renatus Shija ambaye aliwezesha kushika nafasi ya pili ya ligi kuu ya Zanzibar na kuishiriki ligi ya Shirikisho Barani Afrika ambapo walitolewa katika hatua ya kwanza na timu ya Hwange kutoka Zimabwe .
Shija ambaye alikuwa nakubaklika na wachezaji pamoja na mashabiki wa timu kutokana na mbinu zake , alitimuliwa na nafasi yake ikashinkwa na Sebastian Mkoma ambaye naye hakuchukua duru na kubwaga manyanga .
Baada ya kocha Sebastian kuiacha timu hiyo ilikuwa chini ya Kocha msaidizi Mohammed Mzee , na msimu huu timu hiyo iliongezea nguvu kwa kumwajiri kocha Said Mohammed ambaye naye amaipa kisog hivi karibuni kutoka na sintofahamu kati yake na Viongozi .
Kwa sasa timu hiyo yenye mashabiki wengi Kisiwani Zanzibar inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya kushuka uwanjani mara 11 huku ikiambulia alama tatu baada ya kutoka sare michezo mitatu pekee .

EmoticonEmoticon