Na Oscar Assenga,Tanga.
CHAMA cha siasa cha ADC kilichokuwa kikijiimarisha Mkoani hapa, kimepata pigo baada ya kuondokewa na viongozi wake watatu wa ngazi ya Mkoa na Wilaya waliyohamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA).
Viongozi
hao wa ADC waliyokihama chama hicho na kujiunga na Chadema na nyazifa zao ni Kamishina wa Mkoa wa Tanga, Jadi Bamba, Mwenyekiti wa wanawake Wilaya ya Handeni, Mwanamvua Mganga na Katibu wa Chama wa Wilaya ya hiyo, Hamida Msumeno.
Wakizungumza mara baada ya
kupokea kadi mpya za uanachama wa Chadema, viongozi hao walieleza sababu za kukihama chama chao cha ADC kuwa zinatokana na kuridhishwa na siasa za Chadema ambazo hazipo Chama kingine.
Walisema kuwa hawakuhama kwa kurubuniwa bali ni baada ya kubaini kuwa ADC hakuna kazi za
siasa ambazo walizitegemea kuwepo kwa ajili ya kukomboa wananchi wa Tanzania na kwamba Chama makini ni Chadema.
Akiwatangaza katika sherehe za kuwapokea wanachama hao wapya, Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje alisema kuwa viongozi hao ni mashujaa na kwamba anatarajia watakuwa chachu ya vuguvugu la kisiasa ndani ya Mkoa wa Tanga.
Bahweje alisema kuwa si viongozi hao pekee lakini anampango wa kupokea wengine kutoka vyamba mbalimbali vya siasa ikiwemo CCM ambacho alidai kuwa kimekuwa mufirisi kwa kuwa na viongozi wasiyo na maono juu ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha aliwaomba wananchi na wanaCCM kwa ujumla kukiunga mkono Chadema kwa madai kuwa ndicho chenye malengo na mikakati ya kulikomboa taifa hili kutokana na kuendesha siasa za kistaarabu na zenye kuleta matumaini.

EmoticonEmoticon