NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amewahakikishia Watanzania kuwa uchaguzi wa kupata Kamati mpya ya
Utendaji ya shirikisho utafanyika Oktoba 27 mwaka huu kama ilivyopangwa.
“Wazungu
wanasema ije mvua au jua, uchaguzi utafanyika. Isipokuwa tunachotaka
kuhakikisha ni kuwa unakuwa uchaguzi huru na wa haki,” amesema Rais
Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF leo
mchana (Oktoba 7 mwaka huu).
Amesema
mchakato unakwenda vizuri kilichobaki ni revision (mapitio) na rufani,
masuala ambayo yako mbele ya Kamati ya Rufani ya Maadili na Kamati ya
Rufani ya Uchaguzi.
Rais
Tenga amesema lengo la hatua hizo si kuzuia watu wasigombee kwani ni
lazima mambo ya msingi ikiwemo sifa za wagombea yaangaliwe, lakini
kwenye haki ni lazima kuhakikisha inatendeka hata kama ni kwa mtu mmoja.
Mchakato
wa uchaguzi ulivutia waombaji 58 ambapo watatu wamekata rufani Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi kupinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi wakati
wengine wanane masuala yao yamepelekwa Kamati ya Rufani ya Maadili kwa
njia ya mapitio (revision) ili kupata mwongozo wa utekelezaji.
Mwongozo
huo umeombwa na Sekretarieti ya TFF kwa Kamati ya Rufani ya Maadili kwa
vile Kamati ya Maadili iliwaona waombaji wanane wa uongozi
waliofikishwa mbele yake kwa makosa ya kimaadili kutokuwa na hatia,
lakini wakati huo huo ikitambua kuondolewa kwao kwenye kinyang’anyiro
cha uchaguzi kulikofanywa na Kamati ya Uchaguzi.
EmoticonEmoticon