Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Waamuzi
wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa
utimamu wa mwili (physical fitness test) utakaofanyika katika vituo
viwili.
Mtihani
huo utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es
Salaam na Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya
Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga,
Simiyu, Singida na Tabora.
Kituo
cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es
Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara,
Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki
wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si
vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki
katika mtihani huo.

EmoticonEmoticon