Na Oscar Assenga, Korogwe.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu
CCM Taifa kupitia wilaya ya Korogwe Vijijini,Dr.Edmund Mndolwa amesema
atahakikisha anawahamasha wakina mama wilayani hapa kutumia kilimo cha alizeti
kwa sababu ni mkombozi wa maendele na wakulima wa zao hilo mara nyingi wanakuwa
na fedha zao mikononi .
Dr.Mndolwa alitoa kauli hiyo wakati akitoa mada katika semina
ya wakina mama wajasiriamali iliyokua ikielezea kuhusu umuhimu kilimo cha zao
la alizeti na kushirikisha wajumbe wa baraza la Umoja wa wanawake wa chama cha
mapinduzi (UWT) wilaya ya Korogwe vijijini iliyofanyika katika ukumbi wa CCM
wilaya ya Korogwe .
Alisema kuwa ubora na umuhimu wa zao hilo ni mkubwa kutokana na
kuwa ni miongoni mwa mazao ambayo hayahitaja mvua nyingi ili kuweza kustawi na huwa hayaingiliani na kilimo
cha mahindi ambapo aliwataka wakinamama hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi
wazuri katika jamii zao kupanda zao hilo ambalo soko lake kupatikana ni rahisi
pamoja na mkulima kuweza kujikomboa kimaisha.
Mndolwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wazazi (CCM)mkoa wa Tanga
alisema katika kitu cha kwanza wakulima wa zao hilo wakae kwenye vikundi ili
kuweza kuangalina mamna ambavyo wanaweza kulima zao hilo kwa kushirikiana kwa
pamoja ili kuweza kuendesha maisha yao kupitia kilimo.
“Ajira kubwa inapatikana kupitia kilimo na kuwashauri wakinamama
wahakikishe wanalima alizeti kwa sababu hakiingiliani na mazao mengine ikiwemo
mahindi na wala hakiitaji mvua nyingi hivyo wakipanda zao hilo wataona faida
zake kwa kipindi kifupi “Alisema Dr.Mndolwa.
Aidha alisema atahakikisha anapita kila tarafa kuhamasisha wananchi kulima zao hilo ambapo uhamasishaji
huo utakwenda sambamba na kuwashawishi watu wenye uwezo mkubwa kuweka mashine
za kukamulia alizeti katika maeneo mbalimbali wilayani humo nia ikiwa ni kuwapa
dona wakavue samaki.
Mndolwa aliwataka wakina
mama waunde vikundi kila kata ili kuweza kufanya mpango wa kutoa shamba kwa
vijana hekta tano ili kuweza kuwainua vijana kiuchumi na kuwaepusha na
kuendelea kukaa vijiweni ikiwemo kujihusisha na vitendo viovu visivyotakiwa
katika jamii zao.
Alieleza kuwa endapo malengo hayo yatafanikiwa itasaidia kuwaondoa
vijana kwenye vijiwe ambavyo wanakuwa wakitumia muda mwingi kutumia madawa ya
kulevya pamoja na kujadili jinsi gani ya kupata pesa kwa njia zisizo za halali
hali ambayo sio nzuri kwa maisha yao ya baadae.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe
Vijijini,Nassoro Hemed Nassoro “Mali Ngumu”alisifu jitihada zinazofanywa na
Dr.Mndolwa kwa kuona umuhimu kuwaandalia semina wakinamama hao na kuleza kuwa
itawasaidia kuweza kujiajiri wenyewe kuliko kuendelea kuwa tegemezi katika
jamii zao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon