BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA

July 24, 2025 Add Comment


*📌Yakutana na Mhandisi Mramba kueleza uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hauna athari kimazingira*


*📌Yaialika Wizara ya Nishati kushiriki Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York*


*📌Mramba aahidi kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia utekelezaji miradi ya Nishati*


Benki ya Dunia (WB) imeeleza kuwa itatoa fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha  umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.


Hayo, yameelezwa na Mtaalam wa Nishati kutoka Ofisi ya Benki ya Dunia nchini Tanzania, Dkt. Rhonda Jordan wakati alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba katika Ofisi za Wizara ya Nishati Mji wa Serikali Mtumba Julai, 23 Jijini Dodoma.


Dkt. Rhonda amesema kuwa kwa sasa benki hiyo imeridhia kutekeleza mradi huo baada ya kujiridhisha kuwa hauna athari za kimazingira kama ilivyokuwa ikielezwa hapo awali.


“Bodi ya Wakurugenzi sasa itapitisha fedha kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo, ambao ulikuwa ukisuasua kutekelezwa kwa madai ya kuathiri mazingira, lakini sasa bodi imeridhika na itatoa fedha za kuanza kuutekeleza”, amesema Dkt. Rhonda



Katika hatua nyingine, Dkt. Rhonda ameialika Wizara ya Nishati kushiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika Jijini New York nchini Marekani mwezi Semptemba, 2025.



Katika mazungumzo yao, Katibu Mkuu Mramba amemueleza Dkt.Rhonda kuwa wataendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo ule wa usafirishaji umeme wa Tanzania-Zambia (TAZA) na mingine inayofafana kama hiyo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga na Mhandisi Nishati Mkuu John Mageni.

WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA MIUNDOMBINU YA ELIMU IRINGA-RC KHERI

July 23, 2025 Add Comment
Kwa kutambua kazi iliyofanywa na serikali Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Kheri James amewahimiza wananchi Mkoani humo kuhakikisha wanalinda na kuitunza miundombinu iliyojengwa katika sekta ya elimu mkoani humo ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kuufikisha mkoa katika lengo la kuinufaisha jamii kielimu na taifa kwa ujumla.

BIL 67.507 KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU SEKONDARI MKOA WA LINDI NA PWANI

July 23, 2025 Add Comment
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mradi wa kuboresha elimu ya sekondari-SEQUIP katika Mkoa wa Lindi imetoa Shilingi Bilioni 31,716 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule ikiwemo ujenzi wa shule mpya za Sekondari za kata 28.

DC KOROGWE AIPA KONGOLE MUHIMBILI NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION KWA HUDUMA ZA MATIBABU MKOANI TANGA

July 22, 2025 Add Comment


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema amekoshwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bure zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila kwa kushirikiana na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika kambi inayofanyika viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe mkoani Tanga.

 

Akizunguza katika kambi hiyo Mhe. Mwakilema amesema serikali inaendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya afya kwa kutambua umuhimu wa sekta hiyo kwa wananchi na namna inavyoweza kuchochea Uchumi wa nchi kwa kuwa jamii yenye afya madhubuti itakuwa imara katika shughuli mbalimbali za uwekezaji


“Nawapongeza sana Muhimbili na Vodacom Foundation Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboreshaji wa huduma za afya, wanaamini sana huduma za ubingwa bobezi zinazotolewa nanyi kutokana na historia na uwezo wenu wa muda mrefu hapa nchini ndio maana mnaona wamejitokeza kwa wingi” amebainisha mhe. Mwakilema. 


Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto MNH. Dkt Aika Shoo amesema timu hiyo imejipanga kwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaofika katika kambi hiyo wanapata huduma bora kwa wakati bila gharama yeyote na hivyo amewaomba waendelee kujitokeza kwa wingi.


Naye Meneja wa Eneo -Vodacom Korogwe Bw. Kaanankira Nanyaro amesma Vodacom Tanzania Foundation wataendelea kushirikiana bega kwa bega na Muhimbili katika kuhakiisha kuwa wananchi wanapatiwa huduma za afya kadri itakavyowezekena.


MNH na Vodacom Tanzania wameanza kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bila malipo kuanzia Julai 21 hadi 23, kwa wakazi wa Tanga ambapo baadaye huduma hizo zitahamia katika Mkoa wa Kiliamjaro kuanzia Julai 25 hadi 27, 2025

DKT.BITEKO AHANI MSIBA WA MZEE MGANGA NGELEJA

July 22, 2025 Add Comment

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ahani msiba wa Baba Mzazi wa William Ngeleja, Mzee Mganga Ngeleja aliyefariki Julai 16, 2025 na kuzikwa jana (Julai 21, 2025) Kijijini kwake Bitoto, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza.