DKT.BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA PUMA DUNIANI

May 27, 2025 Add Comment


📌 Tanzania na PUMA kuimarisha ushirikiano


📌 PUMA kuendelea kuwekeza zaidi Tanzania


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nishati ya PUMA Energies, Duniani Bw. Mark Russell.


Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Mei 27, 2025 jijini Dodoma, Dkt. Biteko ameipongeza Kampuni ya PUMA Energies kwa kuwekeza nchini na kutoa huduma ya viwango vya juu katika bidhaa zake pamoja na kuzingatia wazawa katika nafasi za juu za utendaji za Kampuni hiyo nchini. 


Vilevile, ametoa rai kwa PUMA Energies kuendelea kuwekeza zaidi nchini na kusema kuwa Kampuni hiyo inaweza kujenga vituo zaidi vya kuweka gesi kwenye magari ili kusaidia upatikanaji wa huduma kwa wananchi. 

Kuhusu nishati safi ya kupikia, Dkt. Biteko ametoa wito kwa Kampuni ya PUMA kuwekeza katika eneo hilo na kusema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano wake kwa Kampuni hiyo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nishati ya PUMA Energies, Bw. Mark Russell amesema kuwa Kampuni yake imewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 24 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya kujaza gesi kwenye magari katika mikoa ya Dar es salaam na kimoja Dodoma.


MWISHO.

VERTEX YAJA NA UWEKEZAJI KIGANJANI

May 27, 2025 Add Comment



NA MWANDISHI WETU

MTENDAJI Mkuu wa Vertex International Securities limited Mateja Mgeta amewataka watu kuwekeza kupitia huduma ya Vertex Mobile Trading App ambayo itawasaidia wananchi kufanya uwekezaji kwa wepesi kwa kuwa ni moja ya njia nyepesi kwa watumiaji.

Mateja amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Vertex Mobile Trading App yenye lengo la kuwapa wepesi wawekezaji kupitia simu janja zao.

Amesema lengo la ujio wa app hiyo una sura mbili ambazo ni kuwapa watu maarifa ya uwekezaji kwa urahisi iwe mtu anahitaji kuwekeza hisa katika makampuni yaliyoorodheshwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) hivyo imani ni kubwa kuwa elimu ndio funguo ya ushiriki wa uwajibikaji.

Sababu ya pili iliyowasukuma kuanzisha Vertex Mobile Trading App kulenga kurahisisha mfumo wa uwekezaji kuufanya uwe wazi, rahisi na salama kwa watumiaji ambao mwekezaji au mwekezaji mtarajiwa anayetumia simu janja (smart phone) anaweza kufungua akaunti ya hisa, kununua au kuuza hisa kupitia kiganjani pasipokuwa na ulazima wa kufika ofisni kwao.

"Masoko ya mitaji yana jukumu muhimu sana katika kukusanya fedha kwa ajili ya matumizi yenye tija yanayotumika kama njia ambazo akiba inaweza kuelekezwa kwenywe miradi inayochochea ukuaji wa uchumi, ubunifu na kutengeneza ajira,"amesema Mateja.

Aidha Mateja amesema uwekezaji uchangia kikamilifu katika ajenda ya uchumi wa Taifa, hivyo kutokana na uwekezaji unaweza kuimalisha masoko ya mitaji ya ndani, kupunguza utegemezi wa ufadhili kutoka nje na kukuza uwekezaji utakaochochea ustawi wa pamoja.

Mateja ametoa pongezi kwa mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania (CMSA) chini ya Mtendaji wake Mkuu CPA Nicodemus Mkama kwa kuweka mazingira wezeshi katika soko kwani bila miongozo yao wasingeweza kufika walipo sasa.

Pia alitoa pongezi kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Peter Nalitolela kwa mchango wao mkubwa kuhakikisha Vertex Mobile Trading App mafanikio ya hisa kiganjani ambayo yamefanywa na wao Vertex International Securities limited.

Kwa upande wa mwakilishi kutoka CMSA Alfred Mkombo amesema wao mamlaka ya msoko ya mitaji wanafurahi kuona maendeleo kama haya ambayo yanawapa watu urahisi wa kuwekeza kupitia simu zao viganjani.

"Simu imekuwa kitu kikubwa zipo hadi vijijini mtu anaweza kushiriki minada inayotokea Dar es Salaam bila kusafiri na kutumia gharama kubwa, Vertex Mobile App imetengenezwa ili kuleta mageuzi na ni tekinolojia ambayo inatumika kwa wepesi bila hata kutumia nguvu,"

"Tunapenda kuona teknolojia hizi zinaleta tija zaidi tunawapongeza sana Vertex kwa namna ya kipekee kufikia hatua hii kubwa sana ya mafanikio ambayo inaakisi sera na sheria usimamizi unaoleta mazingira bora,"amesema Mkombo.

Huku Ali Othman kutoka DSE amesema jambo lililofanywa na Vertex ni kubwa na litaleta mafanikio makubwa kwa kuwa ni njia nzuri na rahisi kwa watu kutumia.

"App ina kila kitu kwa mtumiaji wa mtandao wowote Vertex Mobile Trading App imewarahisishia hii ni hatua nzuri inaongeza ushindani na ubunifu mpya kwa watu wote kuwekeza iwe mjini na hata vijini,"amesema Othman.









SERIKALI YAITAKA COMMUNITY NETWORK KUSAMBAZA TEHAMA VIJIJINI

May 27, 2025 Add Comment
Serikali kupitia Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeitaka Taasisi ya School of Community Network kuongeza juhudi za kuanzisha vituo vya mafunzo ya TEHAMA katika mikoa mbalimbali nchini, hususan vijijini, ili kuwajengea vijana ujuzi wa kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidigitali.

LESOTHO WAVUTIWA NA REA

May 27, 2025 Add Comment
-Wampongeza Rais Samia katika suala la uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia

MBOGGO ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TANGA KUPITIA ACT- WAZALENDO HUKU AKIHAIDI KUIREJESHA TANGA YA VIWANDA

May 27, 2025 Add Comment
Katibu wa Chama cha ACT -Wazalendo  Wa Jimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda (kushoto)  akimkabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Tanga mwanachama wao John Charles Mboggo  (katikati)  kulia ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Tanga (ACT Wazalendo) Zaharan Mohamed


Na Oscar Assenga, Tanga.

KADA wa Chama Cha ACT –Wazalendo Mkoani Tanga John Charles Mboggo amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga kupitia chama hicho huku akihaidi kuirejesha Tanga ya Viwanda ambayo ni ndoto kubwa ya wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema lenbgo la kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ni kutaka kuhakikisha anatoa mchango wake katika kurejesha viwanda vya Tanga ambavyo wananchi wamekuwa na kiu navyo.

Alisema kwamba kwa sababu viwanda ni ajira  na nguvu kazi ya Tanga wanaongelea kuna vijana asilimia 68 ya vijana wakitumika kwenye viwanda watakuwa na uchumi kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa Ujumla.

“Tanga tunaamini sisi ni watu tunaamini watu wa kuleta maendeleo na ndio maana tunawahamasisha wananchi wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kura  kwa lengo la kuwachaguoa viongozi watakaowaongoza”Alisema



Aidha alisema kwamba wasione aibu kutokana na uwepo wa hila mbalimbali wanajua namna ya kubaliana nayo ili kuhakikisha hazijitokezi kwenye mchakato huo.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Tanga  Anasi Mohamed Rweymamu alisema kwamba wanaendelea kuwakaribisha wagombe na kura zao wa maoni ndani ya chama ndizo zitakazoamua nani anaweza kupeperusha tiketi ya chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge.

Alisema kwamba ACT Wazalendo ndio chama pekee ambacho kinaweza kupeperusha vyema Bendera yake katika kuibuka na ushindi kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Tanga na Tanzania kwa upekee.

Naye kwa upande Katibu wa ACT  WaaJimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda alisema kwamba wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi kama chama hicho Taifa kilipotangaza kwamba zoezi la kuchukua fomu kutoka Aprili 18 mwaka huu mpaka 31 mwezi Mei katika nafasi za Ubunge na Udiwani.

Alisema kwamba katika uchaguzi huo wamejipanga kwamba wagombea watakao wapitisha katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo watakuwa imara kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera hiyo.

Mwisho.