MBOGGO ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TANGA KUPITIA ACT- WAZALENDO HUKU AKIHAIDI KUIREJESHA TANGA YA VIWANDA
siasaNa Oscar Assenga, Tanga.
KADA wa Chama Cha ACT –Wazalendo Mkoani Tanga John
Charles Mboggo amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge katika Jimbo
la Tanga kupitia chama hicho huku akihaidi kuirejesha Tanga ya Viwanda ambayo ni
ndoto kubwa ya wananchi wa mkoa huo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya
kuchukua fomu hiyo alisema lenbgo la kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ni kutaka
kuhakikisha anatoa mchango wake katika kurejesha viwanda vya Tanga ambavyo
wananchi wamekuwa na kiu navyo.
Alisema kwamba kwa sababu viwanda ni ajira na nguvu kazi ya Tanga wanaongelea kuna
vijana asilimia 68 ya vijana wakitumika kwenye viwanda watakuwa na uchumi
kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa Ujumla.
“Tanga tunaamini sisi ni watu tunaamini watu wa kuleta
maendeleo na ndio maana tunawahamasisha wananchi wenye sifa za kupiga kura
kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kura kwa lengo la kuwachaguoa viongozi
watakaowaongoza”Alisema
Awali akizungumza Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la
Tanga Anasi Mohamed Rweymamu alisema
kwamba wanaendelea kuwakaribisha wagombe na kura zao wa maoni ndani ya chama
ndizo zitakazoamua nani anaweza kupeperusha tiketi ya chama hicho kwenye nafasi
ya Ubunge.
Alisema kwamba ACT Wazalendo ndio chama pekee ambacho
kinaweza kupeperusha vyema B
Naye kwa upande Katibu wa ACT WaaJimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda alisema
kwamba wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi kama chama hicho Taifa kilipotangaza
kwamba zoezi la kuchukua fomu kutoka Aprili 18 mwaka huu mpaka 31 mwezi Mei
katika nafasi za Ubunge na Udiwani.
Alisema kwamba katika uchaguzi huo wamejipanga kwamba
wagombea watakao wapitisha katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo
watakuwa imara kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera hiyo.
Mwisho.
TPAWU YATAKA MCHAKATO KIMA CHA CHINI SEKTA BINAFSI UHARAKISHWE
habari
Mwenyekiti TPAWU Taifa Daniel Bariyanka Joachim akizungumza kwenye kikao hicho
Na Godwin Myovela, Morogoro
CHAMA cha
Wafanyakazi Mashambani na Kilimo nchini (TPAWU) kupitia kikao cha Baraza Kuu la
chama hichoTaifa, kimeomba kuharakishwa kwa mchakato unaoendelea wa kupanga kima
cha chini cha mshahara sekta binafsi, kuzingatia maoni ya wadau-sambamba na kuhakikisha
kima hicho kutopungua Tsh. 350,000 kwa mwezi, ili kusaidia kumudu gharama za maisha.
Mwenyekiti
TPAWU Taifa, Daniel Joachim, alitoa tamko hilo wakati wa kikao hicho kilichofanyika
mkoani hapa mwishoni mwa wiki, ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza baraza hilo
limezingatia hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi mwaka
huu, kuhusu utaratibu wa kisheria unaoendelea kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
“Kufuatia tamko
la Rais mkoani Singida, tunamuomba waziri mwenye dhamana kuharakisha mchakato wa
utafiti wa kima cha chini cha mshahara sekta binafsi na kitangazwe kwenye gazeti
la serikali ili kianze kutumika sambamba na kile cha watumishi wa umma kitakachoanza
Julai Mosi mwaka huu,” alisema Joachim na
kuongeza;
“Wakati wa mchakato huo baraza linamuomba waziri mwenye dhamana pamoja na bodi ya kima cha chini cha mshahara sekta binafsi ifanye maandalizi hayo kwa kuzingatia maoni ya wadau ambao ni waajiri na wafanyakazi.”
Aidha,
baraza hilo limewaomba waajiri wote kuzingatia takwa la sheria la majadiliano mahali
pa kazi ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi kupitia mikataba ya hali bora za kazi
kwa mujibu wa kifungu cha 68 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini sura ya
366.
Katika hatua
nyingine, Tpawu imekemea na kulaani vitendo vya baadhi ya waajiri ambao hutumia
kima cha chini cha sekta husika kama sababu ya wao kutoongeza mishahara, jambo ambalo
halikubaliki.
“Huu ni mtazamo
potofu sababu unakwamisha lengo la kutungwa kwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,
pamoja na Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani Na. 98 vinavyotoa haki ya majadiliano
mahali pa kazi,” alisisitiza Joachim
Hata hivyo,
alimsihi Rais Samia kusaidia wafanyakazi wa sekta binafsi hasa sekta ya kilimo kupata
mshahara unaoweza kuwasaidia kumudu gharama za maisha ya kila siku-mathalani-ikiwa
sekta ya umma watalipwa kima cha chini Tsh.500,000 basi sekta binafsi kima cha
chini kabisa kisipungue Tsh.350,000 kwa mwezi.Katibu
Mkuu TPAWU Taifa John Vahaye akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe
Baraza Kuu TPAWU Taifa wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye kikao hicho
MITAA 58 HALMASHAURI YA MJI WA TARIME IMEFIKIWA NA UMEME-MHE KAPINGA
📌 *Ni kati ya mitaa 81 ya Halmashauri ya Mji wa Tarime*
*📌 Asema kazi ya kupeleka umeme vitongojini ni endelevu*
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imefikisha umeme kwenye mitaa 58 ya Mji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kati ya mitaa 81 ya Halmashauri hiyo.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Kembaki aliyeuliza Serikali itapeleka lini umeme katika mitaa 18 ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.
"Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina mitaa 81, kati ya hiyo mitaa 58 tayari imefikiwa na umeme, na mitaa 23 bado haijafikiwa na umeme." Amesema Kapinga
Ameongeza kuwa, mitaa 13 inapelekewa umeme kupitia mradi wa Hamlets Electrification Project - IIA (HEP IIA) unaotekelezwa na Mkandarasi Dyname Construction Engineering, na mitaa 10 iliyobaki itafikishiwa umeme katika miradi inayofuata.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake (UWT), Mhe. Zaytuni Swai aliyeuliza kuhusu jinsi Serikali ilivyojipanga kupeleka umeme maeneo ya pembezoni mwa mji wa Arusha hususan kwenye Kata ya Telat, Mhe. Kapinga ameeleza kuwa, Serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika maeneo ya pembezoni (Peri Urban) kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo lengo lake ni kusambaza umeme maeneo ya pembezoni mwa mji.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Pareso alyeuliza kuhusu Vitongoji vya Wilaya ya Karatu kutokuwa na umeme na vichache vilivyo kwenye mradi kupelekewa nguzo 40 ambazo hazitoshelezi mahutaji na kuiomba Serikali kuongeza idadi hiyo, Mhe. Kapinga amesema kuwa kwa kawaida miradi ya Vitongoji inawigo kulingana na kazi aliyopewa Mkandarasi, hata hivyo amesema kuwa Wilaya ya Karatu ipo katika mradi wa Vitongoji 9,000 ambao utaanza kutekelezwa hivi karibuni na kusisitiza kuwa, miradi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ni endelevu.