TPDC Yadhamini na Kushiriki Mbio za Marathoni kwa Lengo la Kuelimisha Umma Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia

May 17, 2025 Add Comment
 Baadhi ya wanachama wa TPDC Runners Club wakiwa katika picha ya pamoja

MAJALIWA: SANAA INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI

May 17, 2025 Add Comment


_▪️Awataka wasanii wawekeze zaidi katika sanaa ili kuongeza wigo wa ajira_

 


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema sekta ya utamaduni na Sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wasanii na Taifa, kuongeza fursa za ajira, kurasimisha kazi za sekta sambamba na kuimarisha maadili ya jamii.


Waziri Mkuu ametoa wito kwa wasanii nchini waweke kipaumbele cha kuwekeza mapato yatokanayo na kazi zao katika shughuli za mnyororo wa thamani wa sanaa ili kuongeza wigo wa kuajiri vijana katika sekta hiyo na kuongeza pato la Taifa.


Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Mei 17, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Wadau wa Utamaduni na Sanaa uliofanyika kwenye Ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam. Amesema sekta hizo zimeajiri makundi yote jumuishi yakiwemo ya watu wenye ulemavu, vijana, wazee na watoto kwa jinsia na hali tofauti na watu wote.

Waziri Mkuu amesema zaidi ya hayo, sekta hiyo inakuza ujasiriamali na biashara ndogondogo na za kati. ”Sote tumewashuhudia wasanii wakianzisha biashara, kuzirasimisha na kuziweka katika mfumo unaotambuliwa na mabenki ili  kuzitumia kama dhamana kwenye taasisi za kifedha ili kupata mitaji kwa shughuli mbalimbali.”


Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wasanii wote nchini wajitahidi kutengeneza kazi bora zaidi na kurasimisha shughuli zao za sanaa katika mamlaka husika za binafsi na Serikali ili kila msanii awe rasmi na aweze kunufaika na fursa zilizopo.

Amesema Sekta za Utamaduni na Sanaa inatoa mchango mkubwa katika uchumi kote ulimwenguni, ambapo Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ya mwaka 2022, imebainisha kuwa sekta hizo zilichangia asilimia 3.1 ya Pato la Dunia (GDP), huku ikitoa asilimia 6.2 ya ajira sawa na ajira milioni 50 duniani kote.


Waziri Mkuu amesema kwa kutambua umuhimu wa sekta za utamaduni na sanaa, Serikali imefanya jitihada mahsusi za kuendeleza sekta hizo.  Jitihada hizo ni pamoja na kuimarisha mifumo kisera na rasilimalifedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kisekta.


Pia, Waziri Mkuu amesema sambamba na kutunga sera, Serikali imetunga sheria na kanuni zilizoleta mageuzi ya shughuli za utamaduni na sanaa. ”Mifumo hiyo ya kisheria, imewezesha shughuli za utamaduni na sanaa kuondoka kwenye dhana ya kuwa burudani pekee na kuwa ajira rasmi zinazochangia kukuza pato kwa mtu binafsi na Taifa.


Amesema hatua hiyo kwa upande mwingine ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 Ibara ya 241 inayoielekeza serikali kuboresha tasnia ya sanaa nchini ili kuiendesha kibiashara  na  kuongeza upatikanaji wa fursa zaidi za ajira kwa makundi yote ya jamii.


Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema Mkutano huo ni wa pili katika mfululizo wa mikutano ya wadau wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania inayolenga kuwakutanisha ili kubadilishana uzoefu, kujadili mafanikio na changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana nazo.


Akizungumzia kuhusu mahitaji ya mikopo kwa wasanii amesema ni makubwa kuliko mtaji walionao na kwa upande mwingine wadau wanaomba kiasi cha juu cha mkopo kinachotolewa cha shilingi milioni 100 kiongezwe mara dufu ili kiendane na uhalisia wa uwekezaji kisekta.


“Tumetoa mikopo yenye masharti nafuu kwa zaidi ya miradi 580 ya wasanii, hii inaonesha kwamba Serikali imedhamiria katika kuiinua sekta ya Utamaduni na Sanaa kama kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Hadi sasa tumefanikisha marejesho kwa asilimia 96 hadi sasa, jambo ambalo linaonesha uwajibikaji wa wanufaika.”


Amesema wakati wizara inaendelea na jitihada za kutafuta vyanzo vingine endelevu vya fedha, wanamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za makusudi za kuhakikisha bajeti ya Mfuko wa Utamaduni inaongezeka kila mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026 imefikia sh bilioni nne kutoka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2023/2024.

RAIS SAMIA AELEKEA DODOMA KWA TRENI YA SGR KUSHIRIKI ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

May 17, 2025 Add Comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambapo pamoja na majukumu mengine pia atashiriki  zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.



MWALIMU ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO WENYE UHITAJI ,RAIS SAMIA ATAJWA

May 17, 2025 Add Comment


CDE Mwalimu Nebu Malekela (katikati), wa Shule ya Msingi Magereza iliyopo Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya akikata keki wakati wa sherehe ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa aliyo sherehekea na watoto wenye uhitaji wanaolelewa Kituo cha malezi ya watoto hao Hospitali ya Igogwe Mei 12, 2025. Kushoto ni Mlezi wa kituo hicho, Sister Gloria Mwanjelila.

...................................

Na Dotto Mwaibale

JAMII imetakiwa kujenga tabia ya kusaidia watu wenye uhitaji hasa watoto kwani inasaidia kuwapa faraja na kujiona kama watoto wengine wanaoishi na familia zao.

Ombi hilo limetolewa na Mlezi wa Kituo cha kulea watoto wenye uhitaji katika Hospitali ya Igogwe iliyopo Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Sister Gloria Mwanjelila wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Cde. Mwalimu Nebu Malekela wa Shule ya Msingi Magereza Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya iliyofanyika Mei 12, 2025.

“Hawa watoto wanahitaji faraja kama wanayopata watoto wengine katika familia zao jamii inapokuja kuwatembelea na kushiriki nao kwa mambo mbalimbali kwao inakuwa faraja kubwa na si lazima mpaka kutoa msaada wa vitu ingawa ni wa muhimu kulingana na mahitaji yao mbalimbali,” alisema Mwanjelila.

Akimzungumzia Mwalimu huyo alisema amekuwa ni mtu wa kujitoa mara kwa mara kutembelea kituo hicho na kutoa msaada kwa watoto hao na kueleza kuwa hata wakati wa kusherehekea sikukuu ya pasaka alifika katika kituo hicho na kuwaletea vitu mbalimbali akiwa ameongoza na wanajumbe Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kutoka Kata ya Kiwira baada ya kuratibu tukio hilo.

“Hawa watoto ni wa jamii nzima na ndio tunaowategemea kuwa viongozi wa kesho sisi kama walezi wao hatuwezi kuwatoshelezea mahitaji yao yote hivyo kwa pamoja tukishirikiana tutaweza kuwapatia mahitaji yao mengine ambayo wanayakosa kutoka kwetu,” alisema mlezi huyo.

Alisema Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia Dkt. Samia Suluhu Hassan haiwezi kuvihudumia vituo vyote vyenye wahitaji hapa nchini hivyo ni vema jamii ikajenga utamaduni wa kusaidia eneo hilo ikiwa ni kuungamkono jitihada hizo za Serikali

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo Mwalimu Nebu Malekela alisema aliona sherehe ya kumbukizi yake ya kuzaliwa afike katika kituo hicho na kusherehekea na watoto hao kwa kukata keki pamoja ambapo pia aliwapelekea zawadi.

“Lilikuwa tukio dogo lakini lenye furaha tulikata keki , tukala, kunywa, kuimba na kucheza pamoja na watoto hakika tuli ‘enjoy’sana,” alisema Mwalimu Malekela.

Ndugu zangu wanajamii Neno la Mungu linasema dunia na vyote vilivyopo ni mali ya Mungu pamoja na wewe mwenyewe na hata akiamua kuichukua mali zake atazichukua zote lakini kwa upendo mkubwa ametupa akili ya kuimiliki mali hiyo na zaidi ya yote akatupa nafasi ya kumrudishia sehemu ndogo tu ya mali zetu akituhitaji kuwasaidia wahitaji badala yake na ndio maana anatoa nafasi kwa wenye kitu kidogo kulisaidia kundi hilo kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri.

Mwalimu Nebu Malekela  akionesha upendo kwa kumlisha keki mmoja wa watoto wa kituo hichoMwalimu Nebu Malekela akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao wenye uhitaji

MKURUGENZI MKUU REA AISISITIZA BODI MPYA YA ZABUNI KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

May 17, 2025 Add Comment
-Aipongeza Bodi ya Zabuni iliyomaliza muda wake kwa kazi nzuri iliyofanya