DKT.BITEKO ATETA NA SPIKA WA BUNGE LA MOROCCO

May 15, 2025 Add Comment


📌 *Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara.






CCM TANGA KUSHIRIKIANA NA TFF KUBADILISHA MUONEKANO WA UWANJA WA CCM MKWAKWANI

May 15, 2025 Add Comment

 






Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wamefanya ziara maalumu ya ukaguzi wa uwanja wa CCM Mkwakwani ambao umefanyiwa maboresho makubwa na hivyo unaweza kutumika kwenye mchezo wa nusu fainali wa CRDB Federation Cup kati ya timu ya Yanga na JKT.

Akizungumza mara baada ya kuutembelea uwanja huo,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman alisema kwamba uwanja huo kutokana na maboresho makubwa upo tayari kwa ajili ya mchezo huo utacheza Mei 18 mwaka huu.

Alisema kwamba walifanya maboresho makubwa ya uwanja huo sehemu ya kuchezea ambayo ilikuwa na changamoto awali kwa jitihada walizifanya viongozi kwa kushirikiana na TFF kupitia Rais Karia waliwaunga mkono CCM kwa jitihada za kufanya ukarabati wa uwanja wao na TFF kugharamia majani sasa mambo yapo vizuri.

Aidha alisema lakini matarajio yao kwa kushirikiana na TFF wameshaandaa michoro namna ya kuubadilisha muonekano wa uwanja huo uwanja wa Mkwakwani kwa kuweka viti na kutengeneza jukwaa la kisasa.

“Lakini pamoja na hilo pia tutabadilisha muonekano wa vyumba vya kubadilisha nguo,vyoo nk na sasa hivi tumeshakamilisha michoro na tupo kwenye mchakato wa kutafuta wadau ili waweze kutuunga mkono

Hata hivyo alisema kwamba mchezo wa Nusu Fainali hiyo kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga ni heshima kubwa kwao na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuweza kuipa sapoti nusu fainali hiyo .

Mwisho.

Benki ya CRDB yawakaribisha Wanahisa kwenye Mkutano Mkuu wa 30

May 14, 2025 Add Comment

 

Arusha 14 Mei 2025 - Benki ya CRDB imewataka wanahisa wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha, ambapo Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya Mwaka 2024, inayoonyesha maendeleo makubwa ya kifedha, kiutendaji na kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kwani utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa na umma, itakayofanyika Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025, katika ukumbi wa Simba, AICC. “Semina hii ya kihistoria itakuwa chini ya kaulimbiu yetu ya mwaka huu: ‘Miaka 30 ya Ukuaji wa Pamoja,’ na itafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio yetu ya pamoja, changamoto tulizozishinda, na mwelekeo wetu wa miaka ijayo,” amesema Dkt. Laay.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, kujadili mapendekezo ya maboresho ya Katiba ya Benki, kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2024 ambapo pendekezo la gawio la Sh 65 kwa hisa litawasilishwa sawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa yamekamilika kwa asilimia 100. Nsekela amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki moja kwa moja na kwa njia ya kidijitali. “Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” amesema Nsekela huku akiwahakikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.
Nsekela amewahamasisha wanahisa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu huo wa kihistoria, akisisitiza kuwa uwepo wao ni muhimu kwa ajili ya kushuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 30. “Tumejenga taasisi imara inayotoa huduma bora, tumeongeza thamani kwa wanahisa, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu. Hii ni fursa adhimu kwa kila mwanahisa kujivunia sehemu yake katika mafanikio haya na kushiriki kuamua mustakabali wa benki yetu katika miaka ijayo,” amesisistiza.

WMA YAHAKIKI VIPIMO ASILIMIA 99 YA LENGO

May 14, 2025 Add Comment
Veronica Simba - WMA

Serikali kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) nchini imekagua na kuhakiki vipimo 1,013,859 ambavyo ni sawa na asilimia 99.2 ya lengo la kukagua vipimo 1,022,342 katika mwaka wa fedha 2024/2025.

TANZANIA,MOROCCO KUCHOCHEA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI

May 14, 2025 Add Comment

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu, Mhe. Leila Benali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco, Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 14, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati nchini Morroco

Naibu Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco, Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 14, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati nchini
Naibu Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu, Mhe. Leila Benali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco, Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 14, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati nchini


Sehemu ya wajumbe mbalimbali alioambatana nao Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko wakati wa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco, Mei 14, 2025.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu, Mhe. Leila Benali mara baada ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco.

katika mazungumzo hayo, Dkt. Biteko aliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini pamoja na Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa  nishati vijijini (REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mei 14, 2025.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu, Mhe. Leila Benali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco, Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 14, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati nchini Morocco.



📌 Matumizi ya teknolojia kupewa kipaumbele Sekta ya Nishati


📌 Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Tanzania na Ufalme wa Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa matumizi ya teknolojia katika Sekta ya Nishati ili kuiwezesha sekta hiyo kuwa na mchango endelevu nchini.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa  Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipokutana na Mwenyeji wake Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco.


"Mwaka 2016 Tanzania na Morocco zilisaini hati ya makubaliano (MoU) ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya umeme, mafuta na matumizi ya nishati mbadala ili yapewe kipaumbele katika nchi hizo, ". Amesema Dkt. Biteko


Mhe. Dkt. Biteko amesema pamoja na maendeleo ya nishati yaliyofikiwa, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati mbadala ikiwa na matarajio ya kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda na madini jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.


Ametaja mambo mengine ni pamoja na kubadilishana uzoefu miongoni mwa wataalam katika sekta ya nishati ikilenga kuifanya kuwa na tija kwa taifa na uchumi kwa ujumla.


Kwa upande wake, Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali amesema kuwa Tanzania inaweza kubadilisha sura yake kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi. 


Amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana gizani hivyo, njia ya kuleta maendeleo na ustawi wa watu ni kuwaangaza maisha yao kwa kupitia sekta ya Nishati.


Aidha, Mhe. Benali amepongeza kwa dhati juhudi za Rais Samia kuwa kinara wa maendeleo ya nishati safi ya kupikia, Tanzania na Afrika kwa ujumla. 


Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi katika eneno la Morocco, Mhe. Ally Mwadini, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa  Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).


Mwisho.