Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

SOLO MNAMUNGA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI KOROGWE VIJIJINI CHADEMA

November 14, 2024 Add Comment


NA MWANDISHI WETU,Korogwe

KADA wa siku nyingi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Oliva Kisaka maarufu Solo Mnamunga sasa ni Mwenyekiti mpya wa chama hicho Korogwe Vijijini mkoani Tanga baada ya kupata ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salim Sempoli.

Uchaguzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, na Solo alipata kura 53 huku mpinzani wake, Sempoli akiambulia kura 33 kati ya kura 86 zilizopigwa na wajumbe kutoka kata zote 29 za Jimbo la Korogwe Vijijini.

Mbali na mwenyekiti, nafasi zingine mbalimbali zilishindaniwa na kupata washindi ambao wanatarajiwa kukisaidia chama hicho kuendelea kujitanua na kuleta ushindani mkubwa wa kisiasa dhidi ya Chama Cha Mapindizi (CCM).

Washindi waliotangazwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti, Oliva Kisaka (Solo), Katibu, Thomas Lwoga aliyepata kura 48 dhidi ya Lucyana Andrea aliyeambulia kura 39.

Aidha nafasi zingine ni kama ifuatavyo kwenye mabano, Katibu Mwenezi (Ibrahim Wiss), mweka hazina (Twaha Juma), Mjumbe wa mkutano mkuu (Jumanne Billa), Mjumbe (Ramadhani Kihiyo), Baraza la Wazee, mtunza hazina ni (Said Ally Daffa), naibu katibu (Athuman Ndiga), katibu ni (Ally Juma Mtangi).

wengine ni makamu mwenyekiti (Jalali Salehe Mjenga), Mwenyekiti (Josiah Tumaini) huku nafasi katika Baraza la wanawake za wanawake (BAWACHA) washindi wakiwa ni Aminata Saguti (mwenyekiti),  katibu (Mwajuma Abdalla), mratibu wa uenezi akitajwa kuwa ni Anjelina Mhina na mweka hazina ni Esta Dastan. Kwa upande wa Bavicha, Mwenyekiti ni George Shafi, katibu ni Kaimu Yahaya, katibu mwenenzi ni Msumari Kembo na mweka hazina akiwa ni Adinan Hamisi huku mjmbe wa kaati ya utendaji akiwa ni Rehema Idd.


CCM:TAMISEMI IPUUZE MAKOSA MADOGO,KUKUZA DEMOKRASIA

November 12, 2024 Add Comment


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuwaelekeza wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kupuuza makosa madogo madogo yaliyotokea, ili kuruhusu wagombea wengi kushiriki uchaguzi huo. 


Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya hahari nchini, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa mfano wa makosa hayo yanayostahili kupuuzwa ni pamoja na wagombea kukosea herufi. 



Kupitia mkutano huo uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 12, 2024, Balozi Nchimbi amesema ni vyema TAMISEMI ikaangalia uwezekano wa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kutokana na makosa hayo madogo madogo ili kuhamasisha ukuaji wa demokrasia kwenye uchaguzi huo.


Aidha, kuhusu sehemu kubwa ya malalamiko mengi ya kuenguliwa kuonekana ni ya wagombea wa vyama vya upinzani, Balozi Nchimbi amewatoa shaka Watanzania kuwa, si kweli kwamba wagombea walioenguliwa ni wale wa vyama vya upinzani pekee, bali pia hata wagombea wa CCM wapo waliowekewa mapingamizi ya kugombea. 


“Waziri wa TAMISEMI tunajua anafuata sheria, lakini ni muhimu kutambua demokrasia yetu hii bado ni changa hivyo tunahitaji muda wa kuendelea kujiífunza…tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI katika nyakati za mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogo madogo ili watu wengi wapate nafasi ya kugombea", alisema Dkt. Nchimbi. 


#Ends

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AFANIKISHA MAFUNZO YA UCHAGUZI KWA MABALOZI 227 WA CCM BUKOBA MJINI

November 09, 2024 Add Comment


Mabalozi 227 wa Chama Cha Mapinduzi; CCM, Bukoba Mjini wamenufaika na mafunzo yaliyotolewa katika semina iliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira kuhusu Sheria za Uchaguzi na Vyama Vya Siasa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Wanawake katika Siasa

Aidha, wakati wa semina hiyo, Cde Issa Haji Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni aliongea moja kwa moja na mabalozi hao kupitia simu ya Mbunge Lugangira na kujibu hoja zao na kupokea Salaam za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mabalozi wa CCM wa Bukoba Mjini.
Lugangira akitumia simu yake kuwasiliana na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

Semina hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Omuka Hub na FES Tanzania, ilihudhuriwa pia na Shaban Mdoe, Katibu wa CCM Bukoba Mjini na Hadija Mkelenga, Katibu wa UWT Bukoba Mjini ambao pia walitoa mada.


Sehemu ya mabalozi hao.

Mbunge Neema Lugangira akishiriki kutoa mafunzo hayo.

KATIBU MKUU WA NLD DOYO AITAKA TAKUKURU KUWA MAKINI NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

November 05, 2024 Add Comment

 



Na Paskal Mbunga,Tanga

KATIBU wa Chama cha NLD Taifa Doyo Hassani Doyo ameiomba Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kuwa makini na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye suala la fomu za wagombea kujitoa kutokana na kwamba kanuni hiyo inakwenda kurasimisha rushwa.

 

Doyo aliyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Tanga kuelekea kwenye uchaguzi huo ambapo alisema kwa kutengeneza fomu hizo za wagombea kujitoa kwanini kanuni iwe na mawazo ya watu kujitoa.

 

Alisema kwa sababu watu wamechukua fomu na akili zao wenyewe timamu na hawajashawishiwa na mtu halafu kuwe na fomu ya kujitoa kugombea nafasi hiyo kwanini hivyo wanaiomba walisimamie zoezi la fomu za kujitoa ili kusiwe na watu waliojitoa.

 

“Tunaomba uchaguzi huu Takukuru waingie kwa kiwango kikubwa kuzuia rushwa hii maana mtu anachukua fomu mwenyewe kwa akili yake timamu bila kushawishi na mtu kujaza fomu ya kugombea nafasi hiyo,kwanini  wajitoa “Alisema

 

Hata hivyo Katibu Doyo aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhakikisha wasimamizi wasaidizi wanakuwa waadilifu kwa fomu ambazo wamechukua wagombea na kuzirejesha.

 

Alisema wawe kwa wagombea waliopitisha basi wawateue bila vikwazo ili waingie ulingoni na kuondoa manung’uniko yaliyojitokeza mwaka 2019 katika utawala uliopita.

 

Alisema kwa sababu tarehe 1 wagombea wamejesha fomu na wamekaa nazo wiki nzima hivyo ni muhumu watumie uadilifu kuona njia nzuri ya kuwateua wagombea ambao wametia nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo bila kuwekewa

 

Hata hivyo alisema kwamba chama hicho hivi sasa wamejipanga imara kuhakikisha kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wanasimamisha wagombea makini.

 

Alisema watafanya hivyo wakiwa na nia ya kuhakikisha wanawapa maendeleo watanzania na kuinua uchumi wao katika nyanja mbalimbali.


BALOZI NCHIMBI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CRC WA COMORO

November 03, 2024 Add Comment

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekutana na Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, Katibu Mkuu wa Convention for the Renewal of the Comoros (CRC), chama tawala nchini Comoro. 

Mazungumzo hayo ya pande mbili, yaliyohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya vyama hivyo, serikali na nchi hizo mbili kwa ujumla, yalifanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Novemba 2024.

Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Katibu wa Rais wa Comoro, yupo nchini kwa ziara ya kikazi inayoendelea kuanzia tarehe 2 hadi 5 Novemba 2024.

#Ends