Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts
CHATANDA AWATAKA WABUNGE WANAWAKE WA CCM KUTIMIZA WAJIBU WAO KUWATUMIKIA WANAWAKE NA WANANCHI

CHATANDA AWATAKA WABUNGE WANAWAKE WA CCM KUTIMIZA WAJIBU WAO KUWATUMIKIA WANAWAKE NA WANANCHI

January 30, 2024 Add Comment

  Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,akizungumza katika Mkutano na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,akisisitiza jambo kwa Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima wakati wa kikao kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

  Baadhi ya wabunge wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,(hayupo pichani) wakati wa kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu ,Dodoma .

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amefanya Kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima lengo Likiwa ni Kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kuwatumikia wanawake na wananchi Nchini kwa kufanya Mikutano ya Hadhara ya kuisemea Miradi ya Serikali iliyofanywa na Serikali ya awamu sita chini ya uongozi wake Dkt Samia SuluhuHassan.

Akizungumza leo na Wabunge wanawake wa CCM Nchini Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi katika Mikoa yenu basi sasa niwaombe wabunge muendelea kutembelea miradi na kuisemea kwa wananchi ili wajue Serikali yao imefanya nini kwenye maeneo yenu.

Mwenyekiti Chatanda amewaomba Wabunge wanawake wa CCM Nchini kuendelea kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye Uchaguzi na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa ambayo utaaza hivi karibuni.

"Sisi ndio Jeshi la Mama basi niwaombe wanawake wenzangu mwende kwenye Mikoa yenu fanyeni Mikutano ya Hadhara na kuhamasisha wanawake kugombea kwani wanaweza endapo mkiwahamasisha watahamasika kwa kasi"

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema nimefurahishwa sana na baadhi ya wabunge wanawake ambao wanaendelea kupambana katika kuhakikisha wanafanya Mikutano ya Hadhara na kusemea miradi iliyofanywa katika maeneo yenu hivyo niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kusemea Serikali ya Rais samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti Chatanda amesema Wabunge wangu Nawapenda sana sana muendelea kupambana katika kuhakikisha wananchi na wanawake walipo katika maeneo yenu wajue nini Serikali yao inafanya katika kuwaletea Maendeleo.

Nae Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari amewapongeza wabunge wanawake kwa kufanya kazi katika Mikoa yao na kuwaomba kuendelea na juhudi hizo katika kusemea miradi na kusikiliza kero za wanawake na kuweza kutatua kwa wakati.

"Sisi kama viongozi wenu tupo pamoja na nyie katika kutatua changamoto yoyote ambayo inakwamisha kazi zenu na niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kutatua Migogoro na changamoto zilizopo katika maeneo yenu."

Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jokate Mwegelo amewashukuru wabunge wanawake kwa kujitoa kwa wingi kuja kusikiliza Mwenyekiti na kuwaomba yale yote ambayo Mwenyekiti kazungumza basi yafanyiwe kazi ipasavyo kwa Maslai ya Jumuiya yetu ya Wanawake.

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUTUMIKA KISIASA KUCHOCHEA VURUGU

January 29, 2024 Add Comment

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka vijana kutokukubali kutumika kisiasa katika kuchochea vurugu, uhasama na maandamano yasiyo na tija kwa taifa.


Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Kongamano la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma.

Amesema uchumi wa dunia nzima umeathiriwa na UVIKO - 19, vita baina ya mataifa pamoja athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo uimarishaji wake sio suala la muda mfupi.

Amewasihi vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kutetea maslahi ya Taifa pamoja na kutumia ushawishi wao kuwahimiza vijana wengine na watu wazima kuendelea kuiunga mkono CCM kwa kuwaonesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais amewataka UVCCM kuendelea kuungana na kushikamana ili kujenga Jumuiya iliyo bora na yenye nguvu.

Amesema UVCCM kama zilivyo Jumuiya nyingine za Chama ni muhimu katika kukiimarisha Chama hivyo ni lazima ibaki katika umoja wake kwa kuepuka kutengeneza makundi, majungu, matamko ya vitisho na kauli zisizofaa.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewasihi Vijana kutambua adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujenga demokrasia na kuimarisha utawala unaojali maslahi ya watu ili kujenga ustahimilivu kwa kuepuka migongano, kutafuta suluhu na mapatano pale kunapotokea kutoelewana, kuleta mageuzi yatakayochochea kukua na kushamiri kwa nchi pamoja na kujenga na kuimarisha mifumo mbalimbali katika nchi.

Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa vijana kuuthamini na kuulinda kwa nguvu zote Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kukemea baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza mafanikio ya Muungano huo.

Pia amewataka Vijana wa CCM kuwa kielelezo cha uadilifu, kufanyakazi kwa bidii na kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi, mila na desturi.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa UVCCM na vijana wote nchini kutumia mitandao ya kijamii vizuri ili kujipatia maarifa.

Amesema vijana wanapaswa kutumia fursa ya maendeleo ya TEHAMA kushiriki mijadala yenye tija inayolenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewataka vijana kushiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema suala hilo ni pamoja na kushiriki kikamilifu katika kupanda na kutunza miti na kusaidia kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji moto hovyo.

Aidha amewataka Vijana kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ya kupikia ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yameendelea kuwa makubwa na kusababisha upotevu mkubwa wa misitu nchini.

Katika Kongamano hilo mafanikio mbalimbali ya Serikali ya Awamu ya Sita yameanishwa yakiwemo katika sekta za Afya, Kilimo, Maji, Elimu, Nishati na Miundombinu.

Pia UVCCM wamkabidhi tuzo ya mafanikio kwa Rais pamoja na fedha kwaajili ya kumwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohammed Ali Kawaida wakati alipowasili katika Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohammed Ali Kawaida iliyotolewa na UVCCM kwaajili ya kumwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025. Fedha hizo zimetolewa wakati wa Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohammed Ali Kawaida iliyotolewa na UVCCM kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.
KATIBU MWENEZI CCM PAUL MAKONDA AHIMIZA WATANZANIA KUIPENDA NCHI YAO KWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

KATIBU MWENEZI CCM PAUL MAKONDA AHIMIZA WATANZANIA KUIPENDA NCHI YAO KWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

January 25, 2024 Add Comment






*Atoa rai kwa Watanzania kutotoa maneno ya kulaani Nchi kwani kufanya hivyo ni kujinyima mafanikio katika Nchi uishiyo._

“Tuna kila sababu ya kuipenda Tanzania, ndio nchi yetu, hazina yetu, urithi wetu na ndio mpango wa Mungu wetu kuwepo hapa lazima tuendelee kuimarisha Amani na Utulivu wetu”

“Watu wengi wanapenda kulaani nchi yao lakini mimi niwasihi isije ikatokea jambo ukaanza kutamka maneno ya laana kwasababu hautafanikiwa kwenye nchi uliyoilaani”

“Ukikasilishwa na mtu usitoe neno la kulaani Taifa lako kwakuwa Taifa hili ndio litabeba watoto wa watoto wako kama sio wewe basi watakula neema watoto zako na kama sio watoto zako basi wajukuu zako”

“Kwahiyo tuendelee kuliombea Taifa letu na Rais Samia na tunaposema tumuombee Rais wetu na Viongozi wetu watu wengi wanahitaji tunataka kuwaombea nini, we fikiria kama sio Utulivu, Msaada, Upendo wa Rais Dkt. Samia leo hii kungekuwa na maridhiano? na haya yote anaendelea kuyafanya kwa kuzingatia kanuni yake ya 4R ? Ndio maana tunasema tumuombee”

Makonda ameyasema hayo wakati akiwahutubia wana CCM na wanamchi wa Babati mkoani Manyara akiwa katika Diary yake ya kuhamasisha uhai wa Chama cha Mapinduzi na utlfuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayoendelea katika mikoa 20 ya Tanzania.

    

DK. NCHIMBI AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA ANC KOMREDI MBALULA

January 25, 2024 Add Comment

 

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akipokea zawadi ya kitabu kiitwacho "Dare Not Linger: The Presidential Years" kilichoandikwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela na Mandla Langa, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS),  leo Jumatano, Januari 24, 2024. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, ambaye yuko nchini kwa ajili ya kushiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, kitakachofanyika Januari 25, 2024, nchini Tanzania. Mazungumzo ya makatibu wakuu hao wawili yamefanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS),  leo Jumatano, Januari 24, 2024.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, leo Jumatano, Januari 24, 2024, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha, mkoani Pwani.  




MWENEZI MAKONDA AAMKIA OFISI ZA HALMASHAURI JIJI LA ARUSHA

MWENEZI MAKONDA AAMKIA OFISI ZA HALMASHAURI JIJI LA ARUSHA

January 24, 2024 Add Comment

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amefika katika Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha kuona utekelezaji wa Agizo la Chama Cha Mapinduzi aliilotoa la kumtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha Ofisi inafunguliwa na kusikiliza, kutatua na kusuluhisha migogoro, kero na changamoto mbalimbali za Wananchi.

Makonda amesema jambo hilo lisiwe la siku moja na isiwe kusubiria hadi viongozi wa kitaifa waje na watoa maagizo na badala yake wao wenyewe kujiwekea taratibu hizo ili kusudi kuhakikisha changamoto za Watanzania zinatatuliwa kwa wakati na kufikia dhamira ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.