Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

WATANZANIA KUNUFAIKA NA MASHINDANO YA CHAN 2025,AFCON 2027

January 15, 2025 Add Comment


*📌 Mashindano yameipa heshima Tanzania kimataifa*


*📌 Rais Samia kinara wa Michezo nchini*


*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*


Watanzania watanufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zitakazopatikana kuelekea katika mashindano wa CHAN 2025 na AFCON 2027.


Hayo yamebainishwa leo Januari 15, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Michezo kuelekea CHAN 2025 na AFCON 2027 jijini Dar es Salaam. 


"Nchi yetu imepata heshima kubwa kimataifa na hii haiji kwa bahati mbaya imesababishwa na ukuaji wa demokrasia iliyojengwa na Rais Samia kwenye mataifa mbalimbali duniani," amesema Dkt. Biteko.


Aidha, Dkt. Biteko amewapongeza wadau wa michezo waliotoa mawazo ya kuanzishwa kwa kongamano hilo ili kutangaziana fursa zitakazotokea wakati wa mashindano hayo. 

Ameeleza kuwa, mashindano yatawakutanisha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali na kuna wajibu wa kufanya maandalizi kwa ufanisi mkubwa ili kunufaika na mashindano kupitia fursa mbalimbali za usafirishaji, malazi na burudani. 


"Fursa za mashindano haya zitakuza uchumi wa nchi yetu na kufanya vikundi vya watu au kampuni mbalimbali kufanya biashara na kukuza uchumi wao na hatimaye kuondoa umaskini miongoni mwetu," ameongeza Dkt. Biteko. 



Vile vile, Dkt. Biteko amempongeza Rais Samia kwa kuwa kinara wa kuhamasisha ushiriki wa watanzania katika sekta ya michezo ili vijana kukuza uchumi wao. 


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwijuma amesema lengo la kongamano ni kupokea maoni ya wadau mbalimbali na kuchanganua fursa zitakazokuja pamoja kuelekea mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027 ambazo watanzania watanufaika nazo.

Mashindano ya CHAN 2025 yanatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu na AFCON yamepangwa kufanyika mwaka 2027.







UDSM MARATHON KUBORESHA MAISHA YA WANAFUNZI

December 07, 2024 Add Comment



📌 Dkt. Biteko Ahimiza Wadau Kuchangia Ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi


📌Awashukuru Wadhamini wa UDSM Marathon


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameeleza amefurahishwa kwake na uendeshaji wa UDSM Marathon na kusema kuwa inasaidia kufanikisha malengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendelea kutoa elimu bora na kuboresha mazingira ya wanafunzi.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 7, 2024 mara baada ya kushiriki mbio hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM MARATHON) zilizofanyika chuoni hapo.



“ Ni dhahiri kwamba mbio hizi zimekuwa muhimu kwa Chuo hiki na jamii kwa ujumla. Tukio hili limeleta pamoja wadau mbalimbali na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” amesema Dkt. Biteko.


Ameongeza “Natambua kwa misimu mitano mbio hizi zimekua zikichangia katika ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi kinachojengwa hapa katika Kampasi Kuu ya Mwalimu Nyerere Mlimani. Ujenzi wa kituo hiki ulianza kwa michango kutoka kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na washirika mbalimbali wa maendeleo ya elimu ambapo jumla ya shilingi bilioni 4.4 zimechangwa kutoka kwa wadau.”



Aidha, awamu ya kwanza ya ujenzi imekamilishwa kwa kutumia fedha za ndani  na hivyo kazi kubwa iliyobaki ni kukamilisha awamu ya pili ili kutimiza ndoto ya kuwa  na Kituo cha Wanafunzi  kitakachowezesha wanachuo kuwa na maeneo ya kujifunzia na  kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.


Ujenzi wa awamu ya pili unahitaji shilingi bilioni 3.3 na hivyo kufanya gharama za ujenzi kwa awamu hiyo kufikia shilingi bilioni 9.4 badala ya shilingi bilioni 6 zilizokadiriwa awali ambazo zimebadilika kwa sababu mbalimbali.



Akiwahakikishia ushiriki wake katika kufanikisha ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo Dkt. Biteko amesema  “Nataka niwatoe wasiwasi kuwa jambo hili ni letu sote kwa kuwa majengo haya yatatumika kwetu sote. Nalibeba suala hili kwa uzito wake ili kilichoahidiwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi kipatikane kwa wakati,” 



Pia, ametoa wito kwa wadau mbalimbali 

kuunga mkono jitihada za kuwezesha mbio hizo kufanyika kwa ustadi mkubwa na kwa kuwa zimeonesha kupitia mshikamano, wanaweza kufanikisha malengo makubwa ya kijamii na kielimu. Sambamba na kuhimiza  uongozi wa Chuo kuandaa namna ya kukutanisha wadau zaidi ili kuchangia fedha za kukamilisha ujenzi wa kituo.


Vilevile, Dkt. Biteko amempongeza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa usimamizi wake katika shughuli za maendeleo ya Chuo hicho.



Kwa upenda wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Chuo hicho kinathamini mchango wa Serikali katika ujenzi wa Kituo hicho cha wanafunzi.



Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (Utawala na Fedha), Prof. Bernadeta Kilian amesema Chuo hicho kilianzisha ujenzi wa kituo cha wanafunzi kwa ajili ya kupumzika na kukuza uwezo wa kubuni au kupata mawazo Mapya.


DKT.BITEKO ASHIRIKI UDSM MARATHON

December 07, 2024 Add Comment

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishiriki UDS Marathon iliyoandaliwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya Wanafunzi chuoni hapo kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete, Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa William Anangisye Jijini Dar es Salaam





WAZIRI DKT ASHATU KIJAJI MGENI RASMI MASHINDANO YA RIADHAA YA CLIMATE CHANGE 2024 PANGANI

November 29, 2024 Add Comment




WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Riadhaa ya Climate Change 2024 yatakayofanyika wilayani Pangani kesho Novemba 30 mwaka huu.

Mashindano hayo yameandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope kwa kushiriana na Asasi nyengine za Mtandao wameandaa mbio hiyo fupi katika Mji Mkongwe wa Pangani na wageni kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani watashiriki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya alisema maandalizi  ya mbio hizo yamekamilika na yamefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo wanatarajia Waziri Dkt Ashatu Kijaji kuwasili wilayani humo akiwemo Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka,

Msuya alisema kwamba kwa upande wa njia ambazo zitatumika kwa wakimbiaji hao zipo katika hali nzuri na maeneo ya malazi yapo vizuri huku akisisitiza suala la ulinzi na usalama limeimarishwa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa.

Alitaja mbio ambazo zitakimbiwa na wakimbiaji kuwa ni zile zenye umbali wa Kilomita 21,Kilomita 10 na Kilomita 5 ambapo wakimbia wasiopungua 300 kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanatarajiwa kushiriki mbio hizo.

Aidha aliwakaribisha wadau wote wa mbio na mazingira huku akieleza lengo lake ni kushirikisha wadau wa mazingira kuchangia upatikanjaji nishati safi ya kupikia ikiwa kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu ambaye ndie kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupika katika Taifa ,Africa na Duniani .

Hata hivyo alisema kwamba wanatarijia kupata majiko ya gesi na nishati mbadala kwa kaya mbalimbali hasa zile ambazo hazijiwezi kutumia nishati safi kwa sababu ya kipato.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope Fortunata Manyeresa kwamba kupitia mbizo hizo wanakwenda kuleta hamasa mpya na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake

Manyeresa alisema pia itawajengea wananchi uhimilivu na ustahilimivu kwa masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi na wanaamini kwamba yana athari kubwa kwa jamii na yanawalenga sana wanawake.

Alisema kwa sababu mwanamke ndio wanakwenda kutafuta kuni na maji na usalama wa chakula nyumbani ukiwa dhaifuna kukiwa hakuna chakula watoto wanakwenda kumuambiwa mama.


MBUNGE UMMY AZINDUA LIGI YA WILAYA YA MPIRA WA MIGUU (TDFA ODO UMMY CUP),AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO

November 18, 2024 Add Comment

 


* Akabidhi seti za jezi 27 na mipira 31.

* Mbunge Ummy kudhamini michezo yote 98. TDFA yasema ndio mara ya kwanza kupata Udhamini wa  Ligi ya Wilaya ianzishwe.

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu tarehe 17/11/2024 amezindua ligi ya mpira wa miguu inayosimamiwa na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Tanga (TDFA) iliopewa jina la TDFA ODO UMMY CUP 2024/25.

Ligi hiyo inayoshirikisha Vilabu 27 vya Tanga Mjini itajumuisha jumla ya michezo 98 itakayochezwa katka viwanja vya Lamore Jijini Tanga

Sambamba na kutoa seti za jezi 27 na mipira 31, Mhe Ummy ataendelea kutoa pesa za uendeshaji wa ligi hiyo kwa michezo yote 98 na kuahidi zawadi nono kwa washindi wa 4 wa TDFA Odo Ummy Cup ambao pia watakwenda kucheza Ligi ya Mkoa.

Akiongea kwa niaba ya katibu mkuu TDFA ,katibu msaidizi  Salimu Kalosi amempongeza Mhe Ummy na kusaema toka ligi hiyo ianzishwe hawajawahi kupata udhamini wa aina yoyote. Amemshukuru Mhe kwa kuweka historia Tanga Mjini na pia kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono michezo hususani Mpira wa Miguu Tanga Mjini.

Ufunguzi huo ulihudhuriwa na vilabu vyote 27 kutoka kila Kata, Viongozi wa CCM na serikali pamoja na wananchi na mashabiki wa mpira wa miguu.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini
18/11/2024.