Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA (EACOP) HAUATHIRI SHUGHULI ZA KIUTENDAJI ZA WANANCHI

July 18, 2025 Add Comment


📌 Watenga maeneo maalumu ya vivuko vya Wananchi na wanyama kuondoa usumbufu wakati ujenzi ukiendelea


*📌Wapongeza Serikali kwa kasi ya ujenzi inayoendelea eneo la kutandaza mabomba ardhini na utoaji ajira kwa wazawa


*📌 Vipande takribani 86,000 kutumika kwenye ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima,Uganda hadi Chongoleani,Tanga.


Na Neema Mbuja, Tanga


Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga haujaathiri shughuli mbalimbali za wananchi kwenye Mkoa na vijiji ambapo bomba hilo linapita.


Hayo yameelezwa leo 18 Julai,2025 wilayani Muheza Mkoa wa Tanga na Msimamizi wa mradi kwenye kipande namba 16 kinachojumuisha uunganishaji wa mabomba na uchomeleaji wake kabla ya utandikaji wa mabomba chini ya ardhi eneo la wilaya ya muheza mkoa wa Tanga Mhandisi Thomas Mhando, wakati alipokuwa akitoa tathmini ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la EACOP kwa hapa nchini.

‘’ Niwatoe hofu wananchi na watanzania kwa ujumla wananchi wanaendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa bila kuathiriwa na kazi inayoendelea na wametengewa maeneo maalumu ya kupita na mifugo yao pamoja na madaraja’’ Alisisitiza Mhandisi Mhando.


Amesema kuna jumla ya vijiji 225 kutoka Chongoleani hadi Mtukula Uganda  ambavyo mradi unaendelea na utekelezaji wa kazi mbalimbali na bado wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida za kiuchumi na ujenzi wa barabara pia unazingatiwa.

Ameongeza kuwa jumla la vipande takribani 86,000 vya mabomba vitatumika kwa ajili ya usimikaji wa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Uganda mpaka Chongoleani ambapo kila bomba lina ukubwa wa mita 18 kwa ajili ya kusukumia mafuta kuelekea kwenye matenki maalumu ya kuhifadhia mafuta.

Akizungumzia kuhusu ajira za wazawa wakati wa utekelezaji wa mradi wa EACOP Afisa Rasilimali watu kutoka Kampuni ya CPP inayotekeleza mradi kipande namba 16 Bi Draco Kyando amesema kuwa, tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa EACOP wazawa waishio kwenye vijiji ambavyo mradi unapita wamenufaika na ajira na hivyo kuinua uchumi wao.

‘’ Tunaishukuru sana Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya muongozo wa wazawa kwanza (local content) ambapo hadi sasa jumla ya wazawa 369 wamepatiwa ajira katika kipindi cha kota iliyopita ya mwezi wa tatu mpaka wa sita.

Kwa upande wao wananchi walionufaika na ajira kwenye mradi huo wameishukuru Serikali kwa kutambua umuhimu wa wananchi wake na kuwapatia ajira na kuongeza kuwa nradi umkuwa mkombozi wa maisha yao na familia zao

‘’ Niseme tu ukweli mradi huu imekuwa wa mafanikio makubwa sana kwetu si tu kwenye ajira kwa wazawa, bali hata kubadili kabisa maisha ambapo mfano mzuri ni mimi nisingeweza kujenga nyumba kama hii mpaka nakufa kana sio mradi huu wq EACOP’’ Alisema Bwana Abdallah Jumaa mkazi wa kitongoji  cha Chanzi.



Kambi namba 16 ni moja ya kambi za ujenzi za mradi wa EACOP ambapo inayohifadhi mabomba yanatumika kwa ajili ya kusukuma mafuta ambayo yanatoka Sojo kuja Muheza kwa ajili ya ujenzi wa mradi.

TANZANIA NA KENYA WAZINDUA RASMI MAUNGANISHO YA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

July 18, 2025 Add Comment

 


Na Oscar Assenga, MKINGA

SERIKALI ya Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCCL) na kuunganisha Mkongo wa Mawasiliano Baharini inayopitia Mombasa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (ICTA).

Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Uchumi wa Kenya Mhandisi William Gitau pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Jerry Silaa ambapo walisema kwamba hatua ya uzinduzi huo ni nzuri kutokana na kwamba italeta faida kwa Mataifa yote mawili.

Alisema kwamba wanapongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi nzuri na kubwa ambayo imewezesha mpango huo na kueleza hatua ya kuunganisha mkongo wa mawasiliano kati ya Tanzania na Kenya ulikamilika tokea mwezi Januari mwaka huu na kuanzia Aprili Mosi mwaka huu mawasiliano yalianza kupita baina yay Tanzania na Kenya .

Aidha alisema kwamba Serikali imeweza kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kukuza matumizi ya tehama na kidigitali sambamba na kufungua fursa kwa nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki na Jumuya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kutumia miundombinu iliyopo ya mkongo wa Taifa ya Mawasiliano na wao wanaendelea kutekeleza maelekezo yake aliyoyatoa Desemba 10 2024.

“Kazi ya kujenga Miundombinu ya nchi moja ni kazi moja lakini ukibaki nayo haina faida yoyote ni kama nyumba umejenga na kuweka wayaringi lakini haujaweka umeme kutoka Tanesco kazi tunayoifanya ni kuhakikishaa miundombinu ya Kenya na Tanzania na iliyopo chini ya bahari kama ulivyosema Kenya imeunganika na Sauth Sudani inaunganika pamoja”Alisema

Waziri Silaa alisema kwamba Mkurugenzi wa TTCL alisema vizuri tayari leo wameunganisha na Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Malawi ,Mozambiq na Zambia na sasa wanaanza mradi mkubwa wa kupitisha kebo chini ya ziwa Tanganyika kuunganisha Tanzania na Kongo DRC maunganiko yaliyofanywa leo kwa upande wa Tanzania yameunganishwa na nchi sita hivyo ni kazi kubwa ya kupongezwa sana

Aliongeza kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Julai 29 mwaka 2024 alizindua mkakati wa uchumi wa kidigitali Tanzania na moja kati ya nguzo sita ni nguzo ya miundombinu na kinachofanyika ni moja ya maelekezo yake yaliyopo kwenye mkakati huo ya kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano inaimarika.

“Kuunganisha miundombinu hii zipo faida nyingi faida ya kwanza pale Dar Tanzania tunaunganika na mikongo iliyopo chini ya habari ambayo ni matatu wenzetu wa Kenya Mombasa wameunganika na mikongo ya bahari nane na kwa miunganiko ya leo Tanzania wanapata fursa ya kuweza kuunganika na mikongo nane iliyopo Mombasa ambalo ni jambo kubwa sana”Alisema .

Akiziungumzia Faida ya kuunganika kwa mikondo ni uhakika wa mtandao na kama watakumbuka mwaka jana walipata tatizo la kukatika mkongo wa chini ya bahari uliounganika Dar na hivyo kupelekea kukosekana kwa mtandao (Internet) kwa nchi hivyo kuchati kunakuwa hakuna na ukikosa mtandao benki miamala inakuwa hakuna ,uongozaji wa ndege,kukata tiketi na biashara na utalii ni jambo kubwa kwenye dunia ya leo.

Hata hivyo alisema kuunganika na njia hiyo kwenda Kenya maana yake tatizo lolote linaloweza kujitokeza kwenye mkongo unaoingia Dar maana yake watanzania wataendelea watapata mawasiliano kupitia mikongo inayoingia inayoputia Mombasa vilevile kupata hitilafu kwa mkongo unaoingia Mombasa basa wakenya watapata mawasiliano kwa mikongo inayopita Dar.

Alisema faida nyengine ni ni gharama nafuu na hivyo kuchochea biashara na vijana kupitia bunifu,utalii kuongezekana na milango ya biashara inafunguka na nimataumia yake watanzania na wakenya watatumia muunganiko huo kwa faida ya biashara kwa nchi mbili.

Awali akizungumza Waziri wa Mawasiliano wa Kenya William Kabogo alisema uzinduzi wa mkongo huo ni hatua muhimu kwa mataifa yote mawili hasa katika kuimarisha huduma za mawasiliano ya uhakika na kupunguza changamoto za kukatikatika kwa mtandao

Alisema jambo la msingi ni ushirikiano kwa nchi zote mbili kwa kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo ya kimkakati ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababisha kukatika kwa umeme na mtandao.

“Lakini jambo hilo lisiishie kwenye maunganisho ya leo leo bali wafike maeneo mengi ya Namanga,Holili na mengine tuongeze wigo kwa nchi mbili na yatusaidie kufanya diplomasia ya kiuchumi,kidigitali na ninaimani jambo hili linawezekana “Alisema

Mwisho.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWA BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI -JAB KUHUSU UKIUKWAJI WA SHERIA NA MAADILI YA HABARI

July 18, 2025 Add Comment

 


DKT.YONAZI AIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU MAONESHO SABASABA

July 18, 2025 Add Comment


Na Mwandishi wetu- Dodoma


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya Taifa.


Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo tarehe 18 Julai, 2025 Ofisini kwake jijini Dodoma akikabidhiwa tuzo na  Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga iliyotolewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025.



Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kupokea tuzo kumeongeza motisha katika ushiriki wa maonesho yajayo makubwa ya Kimataifa ya Sabasaba  na kutambua mchango wa Ofisi hiyo iliyoutoa kwa wananchi katika kipindi chote cha maonesho hayo na kutambua huduma ianayotolewa kwa wananchi.

“Ofisi ya Waziri Mkuu imefurahi sana kupokea tuzo hii kama ishara ya kutambua ushiriki wetu na mchango ambao Ofisi yetu inatoa kwa wananchi hivyo tunaamini ushiriki wetu unaofuata utakuwa wa viwango vya juu sana,” Alisema Dkt. Yonazi.



Pia  aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazofanya chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ndio mratibu wa Maonesho kwa  kuhakikisha maonesho hayo yanaleta tija na mageuzi makubwa katika sekta ya kiuchumi kwa wananchi na Kimataifa.


“Tunazishukuru sana Taasisi mbalimbali ambazo tumeshirikiana nazo na viongozi ambao wameendelea kutupa maelekezo yaliyowezesha kufanya vizuri katika maonesho hayo na tunaamini kwamba tutaendelea kuwa washindi au hata washindi wa jumla,”Alishukuru.

Ikumbukwe Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 07 Julai, 2025 na kufungwa na Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa  katika viwanja vya maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 13, 2025.

RAIS SAMIA ATOA BIL 19.6 UJENZI WA MIRADI YA ELIMU (SEQUIP) MKOANI NJOMBE

July 18, 2025 Add Comment
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP mkoani Njombe.