Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts
DKT BITEKO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO TICD.

DKT BITEKO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO TICD.

April 27, 2025 Add Comment




Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, akizungumza mkoani Arusha

Happy Lazaro, Arusha .



Arusha .Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Arumeru, hususan mradi wa kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Arumeru na ujenzi wa jengo la utawala la Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, (TICD).


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tengeru, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 katika miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.




Arusha DC imepokea zaidi ya shilingi bilioni 49.6, na Arumeru imepokea zaidi ya shilingi bilioni 51 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hili ni jambo kubwa, wananchi wana kila sababu ya kumshukuru Rais kwa jitihada hizi,” amesema Dkt. Biteko.

Ametaja mafanikio yaliyopatikana kupitia uwekezaji huo kuwa ni pamoja na upatikanaji wa umeme kwa vijiji vingi, ujenzi wa shule, maabara, vituo vya afya, hospitali, miradi ya barabara, pamoja na miradi ya kilimo.

Aidha, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika ambazo zimefanikiwa kuzalisha umeme kwa asilimia 100.

Pamoja na mafanikio hayo, Dkt. Biteko alieleza kuwa Serikali bado inafanya kazi ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya maji, barabara na miundombinu mingine.

“Serikali ni sikivu. Tutahakikisha barabara zinazohitajika zinajengwa, daraja na huduma za maji zinapatikana. Tutaendelea kutekeleza miradi yenye tija kwa wananchi,” ameongeza.

Tusijaribu kuichezea amani. Ni msingi wa maendeleo yote. Rais Samia ameapa kuilinda kwa gharama yoyote, na sisi wote tuna jukumu hilo,” amesema Dkt. Biteko.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru.

Mradi huo, wenye thamani ya shilingi bilioni 5.664, unatekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 17, 2025.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Taasisi hiyo ya TICD , Dkt. Bakari George, hadi sasa ujenzi huo umeshagharimu shilingi bilioni 2.7.

Jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu na sakafu nne, likiwa na jumla ya ofisi 44 pamoja na kumbi tano zitakazoweza kuchukua watu 545 kwa wakati mmoja.

Dkt. Biteko yupo katika ziara ya siku tano mkoani Arusha, ambapo tayari ametembelea wilaya za Monduli, Longido na Arumeru, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

RC DENDEGO AIPONGEZA TASAC

April 27, 2025 Add Comment



Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa utekelezaji wa majukumu yake ya kuhakikisha Sekta ya usafiri majini inachangia kukuza Uchumi wa Taifa.

Ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea Banda la TASAC, leo tarehe 26 Aprili,2025 katika Maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mandewa mkoani Singida.

“Sekta ya usafiri majini inakua kwa kasi sana, hivyo natoa rai kwa TASAC kuendelea kusimamia sekta hii ili iweze kuleta mabadiliko katika nchi,” amesema Mhe. Dendego.

Akiwa katika banda hilo Mhe. Dendego alipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi, Bi. Mariam Mwayela kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC ikiwemo kudhibiti na kusimamia usalama, ulinzi wa vyombo vya usafiri na utunzaji wa mazingira majini; udhibiti wa huduma za usafiri majini pamoja na kutoa huduma ya uwakala wa forodha kwa bidhaa mahsusi kwa mujibu wa Sheria.  



“Sisi kama TASAC tumekasimiwa majukumu ya kudhibiti na kusimamia usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira ya vyombo vya usafiri majini na kuhakikisha vyombo, abiria na mizigo vinakua salama lakini pia kwa kuzingatia miongozo ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi kuhakikisha watumishi wote wanakuwa katika hali ya usalama katika mazingira wanayofanyia kazi,” amesema Bi. Mwayela.

Katika maonesho hayo, wadau mbalimbali wametembelea Banda la TASAC akiwemo Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paul Sangeze.

TASAC ni moja ya taasisi zinazoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya OSHA yenye kauli mbiu “ Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali katika kuimarisha Usalama na Afya Mahali Pa Kazi". 

Maonesho haya yanatarajiwa kufikia kilele mnamo tarehe 30 Aprili, 2025.

MHE. MCHENGERWA ASISITIZA KUENZI MUUNGANO, AKAGUA MIRADI, WANANCHI WAMPONGEZA RAIS SAMIA

April 26, 2025 Add Comment

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania wote kuuenzi muungano ili kudumisha amani, umoja na udugu waliotuachia waasisi wa taifa laTanzania; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye huku akiwaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuimarisha usalama wa wananchi.

WATANZANIA WATAKIWA KUULINDA MUUNGANO "

April 26, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga,TANGA


WATANZANIA wametakiwa kuendelea kuenzi na kuulinda Muungano uliopo hapa nchini ambayo ni tunu kubwa ilioachiwa na Waasisi wa Taifa kwa miaka 61 sasa iliyopita ikiwemo kudumisha mshikamano na umoja

Hayo yalisemwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Maulidi wakati katika maadhimisho ya Muungano ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Aprili 26 ambayo mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo‘Muungano wetu ni dhamana heshima na tunu ya Taifa shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"


Zuberi alisema kwamba ni vema watanzania kuhakikisha wana dumisha umoja na mshikamano hususani wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi ikiwemo kuwasisitizia wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwa upande wa Urais,Ubunge na Udiwani.

Alisema pia ni vema watanzania waliopewa dhamana ya kusimamia sekta mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwawanatekeleza vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamaia maono ya serikali kawenye miradi ya maendeleo.

“Kauli mbiu ya maadhimisho Muungano wetu ni dhamana heshima na tunu ya taifa shiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kauli mbiu hiyo watanzania tumebarikiwa dhamana ya ya muungano wetu waibebe vizuri dhamana hiyo kwa sababu watanzania wanaheshima kubwa kutokana na muungano huo  hivyo heshima hiyo ni vema tuendelee kuidumisha tuilinde na hatimaye kujitokeza kwa wingi kujitokeza kuchagua viongozi wetu kwa amani na utulivu kwa maana ndio njia kushiriki kwenye uchaguzi mkuu’ameongeza


Awali akizungumza Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema kwamba tangu kuasisisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia awamu zote ni mambo mengi ya kimaendeleo yamefanyika hususani kwenye awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Sisi ambao tumeukuta muungano wajibu wetu ni kuutuza , mambo mengi yamefanyika lakini katika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suuhu Hassan yamefanyika mengi zaidi ikiwemo ucumi kuimarika kinachotakiwa ni kuhakikisha kwamba tunakwenda pamoja tukitanguliza mbele maslahi ya muungano wa nchi hizi mbili tunaomba sana amani iendelee kutwala” alisema Dkt. Buriani.

Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dastan Kitandula amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia sekta mbalimbali ikiwamo Afya ,Elimu, Miundombinu ambapo mkoa huo umenufaika kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati.


“Kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Tanga tunampongeza sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika muda ambao tumekuwa wawakilishi wa wananchi hatukuwahi kuona maendeleo makubwa kama haya ya kipindi cha awamu ya sita anayoiongoza” amesema Kitandula.
Mwisho.,


MCHENGERWA AADHIMISHA SIKUKUU YA MUUNGANO KWA KUKAGUA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO

April 26, 2025 Add Comment
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Aprili 26, 2025 amewasili Mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.