Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

RC MALIMA AWAKARIBISHA MAAFISA MAWASILIANO MKOANI MOROGORO

April 03, 2025 Add Comment


Na Mwandishi wetu, Morogoro.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewakaribisha maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa serikali wanaotarajia kukutana kwenye mkutano wao  wa mwaka utakofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 8-12 aprili, 2025.


Mhe. Malima ameyasema hayo leo tarehe 3 aprili, 2025 wakati wa kikao cha pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali katika ofisi yake.

Amesema kama mkoa ameupokea mkutano huo na itakuwa faraja kwa wananchi wa Morogoro kwani ni jambo kubwa kufanyikia mkoani kwake, “Mimi ni mdau mkubwa wa mawasiliano tangu zamani, hivyo mkutano huo ni muhimu kwani afisa mawasiliano ni nafasi kubwa kwenye ngazi serikalini ambapo mtajengewa uwezo na hivyo kunyoosha na kutoa habari kwa wananchi kwa usahihi”.


Hata hivyo Mhe. Malima amewataka maafisa mawasiliano wanaoshiriki mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kwenye Mkoa huo ukiwemo hifadhi ya Taifa Mikumi pamoja na hifadhi ya milima ya Udzungwa.

Mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha maofisa mawasiliano wa serikali unatarajiwa kufanyika Morogoro katika ukumbi wa hoteli ya Morena kuanzia tarehe 8 hadi 12 aprili, 2025.

RC DKT BALITDA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUTENDA MATENDO MEMA

March 31, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian leo ameungana na Waislamu mkoani Tanga kushiriki katika ibadaa ya Eid-alfitr iliyofanyika kwenye Msikiti wa Ijumaa Jijini Tanga huku akiwataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kutenda matendo mema.

Dkt Batilda aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo ambapo aliwataka waumini kuendelea kutenda matendo mema ambayo walikuwa wakiyafanya katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na kuendelea kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Baraka tele na maisha marefu

Alisema wanamshukuru mwenyezi mungu kwa Baraka na wanamuombea Rais Dkt Samia Suluhu kilalaheri na mwenyezi Mungu aendelee kumpa maisha marefu na Baraka tele

“Nimefikisha salamu za Rais Samia Suluhu ambaye anawatakia wote salamu za Eid Mbarak na anawaomba muendele kufurahia na kuendeleza matendo mema ambayo tuliyafanya kwenye mwezi wa ramadhani”Alisema

“ Jana Rais Dkt Samia Suluhu aliweza kutushika mkono wakuu wa mikoa wote na kutoa sadaka ya mbuzi kila kituo na kupelekea kwenye vituo vya watoto yatima ili watoto waliopo kwenye mazingira magumu wawaze kufurahia sikukuu hivyo tunaendelea kumuombea rais kilalaheri na mwenyezi mungu ampe umri na maisha marefu na Baraka tele”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu hana shaka na wanaamni wana Tanga na watanzania wanamuelewa na kumkubalia hivyo ushindi wa kishindo huku akiwataka waendelee kuwa na ukarimu,utulivu



 kuwa na ukarimu.

TANESCO YAIBUKA KINARA TUZO ZA UBORA ZA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA ZA PRST 2024

March 30, 2025 Add Comment


📌Shirika labeba tuzo 4 kati ya 12 zilizoandaliwa.


📌Mawasiliano ya Kimkakati na Ubunifu vyatajwa kati ya sababu za Ushindi huo.


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kung'ara baada ya kushinda jumla ya tuzo 4 kati ya 12  zilizotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania(PRST)kwa mwaka 2024.


Tuzo hizo zilizotolewa 29, Machi 2025 jijini Dar es Salaam zililenga kutambua mchango wa Idara za Uhusiano na Mawasiliano za  Sekta ya Umma na binafsi ambazo zimekua  mstari wa mbele na mahiri katika mawasiliano ya kimkakati.

TANESCO imeibuka mshindi wa kwanza kwenye vipengele vya "Best Digital PR Campaign" kupitia kampeni yake maboresho ya mita za LUKU (TID) ya ''Mita yako tuna kazi nayo'' (TID)iliyofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii.


Kipengele cha ''Best PR Department of the year 2024" iliyotokana na Muundo na utendaji bora wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Shirika.

Imeshinda pia kipengele cha ''Best Crisis and Communication Plan and Strategy" kutokana na Kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara zinapotokea changamoto kuwa wepesi kutoa taarifa,ufafanuzi wa haraka na mawasiliano ya kimkakati.


Mbali Mafanikio hayo ya Kitaasisi Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Irene Gowelle ameibuka Mshindi wa Tuzo ya "Tanzania PR Golden Star of the Year" kwa mchango wake katika kusimamia mawasiliano ya kimkakati na ubunifu katika kuwasiliana na Umma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi  Irene Gowelle  alieleza kuwa tuzo hizo ni heshima kubwa kwa Shirika ikiwa ni ishara ya kutambulika kwa kazi kubwa zinazofanyika katika  mawasiliano kwa umma na juhudi kubwa ya Kurugenzi katika kutekeleza majukumu yake kikamilifu. 


‘’Tuzo hizi ni kubwa sana kwa TANESCO, tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuwasiliana na Watanzania ili kujenga taswira nzuri ya Shirika letu na  kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi,alifafanua Bi Irene.


Vilevile ameushukuru uongozi wa Wizara ya Nishati,Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika kufanikisha shughuli mbalimbali ndani ya  Kurugenzi ya Mawasiliano hatua ambayo imechangia kazi za mawasiliano zinazofanyika kuonekana na kutambulika kwa jamii.


"Napenda nichukue nafasi hii kuushukuru Uongozi wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO kwa ushirikiano mkubwa ambao unatuwezesha na kutupa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu kwa weledi na ufanisi mkubwa"


Kwa upande wake Rais wa PRST Bw. Assah Mwambene, alisema utoaji wa tuzo hizo ni kutambua na kuthamini kazi za idara za mawasiliano za Sekta ya Umma na Binafsi ili kuboresha utoaji wa huduma katika maeneo yao.


Tuzo za PRST zinalenga kutambua mchango wa  mafanikio ya mawasiliano ya kimkakati katika sekta ya umma na binafsi nchini ambapo TANESCO imeonesha umahiri wake katika sekta ya mawasiliano ya kimkakati kwa mwaka 2024.

TANESCO YASHINDA TENA TUZO ZA UBORA HUDUMA KWA WATEJA ZA CICM

March 30, 2025 Add Comment






📌Urahisi wa upatikanaji huduma kwa njia za kidigitali watajwa moja ya kigezo cha kushinda tuzo hiyo

📌MD Gissima aibuka kidedea kwa Kusimamia Maboresho yenye tija huduma kwa wateja Sekta ya Umma.

Shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya the ''Most improved Organization'' eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).

Tuzo hizo zimetolewa 28, Machi 2025 jijini Dar es Salaam ambapo Shirika limepata tuzo hiyo baada ya kufanya maboresho ya kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi Irene Gowelle amesema Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika ikiwa ni ishara nzuri ya maboresho yanayofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.

‘’ Tuzo hizi ni heshima kubwa kwa TANESCO, zinatuongezea ari ya kufanya vizuri zaidi,tutaongeza ubunifu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu’’






Aidha , Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga na yeye alishinda Tuzo ya heshima ya Kiongozi anayefanya mabadiliko chanya yenye tija upande wa huduma kwa wateja katika Sekta ya Umma.

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.