Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

SimBanking kugawa milioni 240, magari matano kwa wateja wake

March 27, 2025 Add Comment

Ikizindua msimu wa tano wa kampeni ya yake ya Benki ni SimBaking, Benki ya CRDB imetangaza kutenga zawadi kiasi cha shilingi milioni 240 pamoja na magari matano.
Akizindua kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul amesema kwa mwaka huu benki imejipanga kutoa magari manne aina ya Toyota IST na Toyota Harrier ‘New Model’ moja kwa wateja watakaoibuka kuwa vinara katika matumizi ya SimBanking katika kukamilisha miamala yao na huduma nyingine.

Bonaventura amesema azma ya Benki ya CRDB siku zote ni kuhakikisha inatoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja wake na jamii ya Watanzania kwa ujumla hivyo itaendelea kuwekeza kwenye ubunifu wa kidijitali ili kukidhi mahitaji yaliyopo na yatakayojitokeza.

Katika kampeni ya mwaka huu ya SimBanking amesema kutakuwa na washindi wa kila siku na kila wiki watakaopata zawadi za fedha taslimu na gari aina ya Toyota IST na mshindi wa jumla ataondoka na Toyota Harrier.

“Tumetenga zaidi ya shilingi milion 240 zitakazotolewa kwa washindi wetu na kila baada ya miezi miwili tutatoa zawadi ya gari aina ya IST wakati mshindi wa jumla tutakayemtangaza mwishoni mwa mwaka atapata gari aina ya Toyota Harrier. Magari haya yote tutakayoyatoa kwa washindi wetu ni ‘New Model’ na yamekatiwa bima kubwa. Kwa wanafunzi wa vyuo, kuna simu za kisasa aina ya Iphone 16 zitakazokuwa zinatolewa kila baada ya miezi mitatu,” amesema Bonaventura.

Kwa miaka mitano ya kuendesha kampeni ya Benki ni SimBanking, amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa ambao kwa sasa kwani kila mwezi takriban wateja milioni moja wanafanya miamala mingi kupitia programu hiyo inayowaruhusu kukamilisha malengo yao wakiwa mahali popote ndani ya saa 24.

Bonaventura amesema Benki ya CRDB inaamini katika kutoa huduma bora na za kisasa ili kuchangia maendeleo ya wateja wake na taifa hivyo kuhitaji kuwekeza katika ubunifu unaoendana na mabadiliko ya teknolojia duniani. Amesisitiza kuwa SimBanking ni kati ya huduma bora inayotambulika duniani kutokana na urahisi, usalama na uhakika wa kukamilisha miamala kidijitali.

“SimBanking ni kati ya huduma za Benki yetu ya CRDB ambazo zimeleta mapinduzi makubwa katika kuchochea ujumuishi wa huduma za fedha nchini. Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011, SimBanking imetoa fursa kwa Watanzania wengi kujiunga na mfumo rasmi wa huduma za benki.





TBS YASISITIZA UMUHIMU WA KUHAKIKI USAHIHI WA VIPIMO ( UGEZI ) WA VIFAA VYA HOSPITALI , KULINDA AFYA ZA WATANZANIA.

March 27, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu.

Machi 26 , 2025 Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limewasihi Watumiaji mbalimbali wa Vifaa Tiba kuhakikisha wanapeleka Vifaa vyao TBS katika Maabara ya Taifa ya Ugezi ili kuhakiki Usahihi wa Vipimo wa Vifaa hivyo utakaowasaidia kuwa na uhakika wa majibu yanayotolewa na Vifaa hivyo suala litakalopelekea kujenga uaminifu na kulinda Afya za Wateja wanaowahudumia.



Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Leo hii katika Makao Makuu ya Shirika hilo Ubungo Jijini Dar Es salaam Afisa Vipimo Mkuu kutoka Maabara ya Taifa ya Ugezi iliyopo TBS Bwn. Joseph Mahilla amesema ni muhimu sana kufanya Uhakiki wa Usahihi wa Vipimo ( Ugezi ) kwenye sekta ya Afya kwa maana ya Viwanda vinavyotengeneza madawa ( pharmaceutical Industries ) *wanatakiwa kufanya ugezi ili dawa zinazozalishwa ziwe na ubora unaotakiwa* , pamoja na maeneo yote yanayotoa Huduma za Afya kama Hospitali , Vituo vya Afya na Zahanati ili kulinda Afya za Watanzania kwa maana kifaa kinapofanyiwa Ugezi kitatoa majibu sahihi yatakayomwezesha Daktari au mtu yeyote katika Sekta ya Afya kutoa maelekezo sahihi kwa mteja.


" Mfano katika Hospitali , Vifaa vinapokua vimefanyiwa Ugezi vitatoa majibu sahihi ya Vipimo ambayo yatamwezesha Daktari kujua mgonjwa ana tatizo gani na kuchukua hatua stahiki za kupambana na ugonjwa husika kwa haraka sana, *daktari hutoa matibabu kutegemea Majibu yaliyotoka maabara, hivyo kama maabara imefanyiwa ugezi daktari atatoa matibabu sahihi kwa mgonjwa na kumhakikishia usalama wake, hii pia itapunguza upotevu wa muda na fedha kwa kufanya ufuatiliaji wa matibabu sehemu nyingine ama kupewa dawa wakati hakuna ugonjwa. Kufanya ugezi kunachangia maendeleo katika Jamii " amesema Mahilla .

Kwa upande wake Bi. Clara Mwinami Afisa Vipimo TBS ametoa wito kwa Hospitali ambazo hazijafanya Ugezi wa Vifaa katika Maabara zao kufika TBS kwa maana Uhakiki wa Usahihi wa Vipimo wa Vifaa vyao utawasaidia kuaminika kwa Huduma wanazozitoa .

Bi. Clara alimalizia kwa kusema kuwa Shirika la Viwango Tanzania TBS kupitia Maabara yake ya Metrolojia wanatoa Huduma ya Ugezi katika maeneo mbalimbali ambayo wana Umahiri na wamepata Ithibati katika Maabara zaidi ya Saba kutoka SADCAS kwa maana majibu wanayoyatoa ni sahihi na yanakubalika kote ulimwenguni.

COSTECH WAKABIDHI RASMI ENEO LA MRADI KWA MKANDARASI KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA STI JIJINI DODOMA

March 26, 2025 Add Comment

 

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekabidhi rasmi eneo la mradi kwa mkandarasi TIL Construction Limited kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo jipya la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI)  jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukabidhi eneo hilo la mradi Machi 25,2025 jijini Dodoma  Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kutoka COSTECH, Dkt. Aloyce Andrew, amesema hatua hiyo inalenga kurahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wa taasisi hiyo.

"COSTECH ina jengo Dar es Salaam lakini tumeamua kujenga Dodoma kwa ajili ya kuwahudumia wadau wetu kwa ukaribu zaidi...,Jengo hili litakuwa na sehemu ya kuhudumia wabunifu, kuatamia kampuni changa, na kuratibu masuala ya utafiti," amesema Dkt. Andrew.

Amesema ujenzi wa jengo hilo, ambalo litajengwa eneo la Azina jijini humo  lenye mita za mraba 4,800, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 kufuatia kusainiwa kwa mkataba Machi 24, 2025.

Kwa upande wake, Mshauri Elekezi wa mradi huo kutoka Kampuni ya MEKON, Benedict Martin, amesema wamekuwa wakihusika katika usanifu wa jengo hilo tangu mwaka jana (2024) baada ya kushinda zabuni kutoka COSTECH.

"Tulishirikiana na COSTECH kuhakikisha jengo hili linakidhi mahitaji yao yote. Pia tuna uhakika kwamba mkandarasi tuliyempata ana uwezo wa kutekeleza mradi huu kwa ubora unaotakiwa," alisema Martin.


Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa TIL Construction Limited, Ding Fubing, ameahidi kwamba kazi itafanyika kwa ufanisi na kumalizika kwa wakati.

"Tunaanza rasmi kesho kwa kulisafisha eneo lote, na baada ya wiki mbili hadi tatu, tutaingia kwenye ujenzi wenyewe. Tunaahidi kufanya kazi nzuri na kukamilisha mradi kwa muda uliopangwa au hata kabla," alisema Fubing.


Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa COSTECH, Imanuel Mgonja, amesema taasisi hiyo ina imani na mshauri elekezi pamoja na mkandarasi, akiwashukuru kwa kujitolea kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ubora unaohitajika..

WANANCHI WA CHAMWINO DODOMA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MIJI 28

March 25, 2025 Add Comment

 Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

 

Mafundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India wakiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akifanya vipimo wakati ujenzi wa kituo cha kusukumia maji kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akisuka nondo wakati wa ujenzi wa tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Fundi kutoka  Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akisuka nondo wakati wa ujenzi wa tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.



Ujenzi wa Mradi wa Miji 28 Chamwino, Mkoa wa Dodoma unaendelea ambapo visima 8 vitakavyopeleka maji kwenye tanki la kuvunia maji vimekamilika.

Kazi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi wa matanki mawili ya lita laki mbili (200,000) eneo la Msanga, tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) katika eneo la Chamwino na ujenzi wa kituo cha kusukumia maji eneo la Chamwino.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi MEGHA Engineering &Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

Mradi huu unatekelezwa chini ya Wizara ya Maji ambapo Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ni miongoni mwa wanufaika katika kanda yake ya Chamwino.

Akizungumza leo Jumatatu, Machi 24, 2025 Kaimu Meneja wa Chamwino, Gray Mbalikila amesema Mji wa Chamwino unakua kwakasi, hivyo kupitia mradi huu hali ya maji itaimarika zaidi na kuweza kusogeza huduma maeneo ya pembezoni ambayo yanakua kwa kasi zaidi kwasababu uzalishaji wa  maji utaongezeka na miundombinu ya mabomba itaboreshwa zaidi.



“Mradi huu unahusisha kazi ya uchimbaji na uendelezaji wa visima virefu ambavyo vinapatikana katika eneo la bonde la maji la Chamwino, ujenzi wa tanki la kuvunia maji katika eneo la Chamwino lenye ujazo wa lita lakitano. Tanki hili litakusanya maji kutoka kwenye visima virefu 8," amesema Mbalikila



Pia ujenzi wa kituo kikuu cha kusukumia maji kwenda katika tanki la Buigiri lenye ujazo wa lita milioni mbili na laki tano (2,500,000) na tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga.

Kazi nyingine ni usambazaji wa maji kwenda katika eneo la huduma ya kitokea kwenye tanki la Buigiri kwa bomba kubwa kwenda katika maeneo ya Buigiri, Chinangali II, Mwegamile na Chamwino na usambazaji wa maji kutoka kwenye tanki la Msanga kwenda katika maeneo ya Msanga

Halima Kambi
Ass. Communication OfficerDodoma Urban Water Supply and Sanitation Authority (DUWASA)P.O. BOX 431 Dodoma
Mobile; 0655 729791/ 0785 303969
DODOMA

WASIRA: VIONGOZI WA VIJIJI,VITONGOJI MSIWARUHUSU WAGENI KUPORA ARDHI

March 25, 2025 Add Comment

 

                                                      Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Karagwe

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amewataka viongozi wa vijiji na vitongoji kutowaruhu wageni kutoka nchi jirani kuingia nchini na kuweka makazi ya kudumu kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwa siku za baadaye.


Aidha, Wasira ameahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa alitafute ufumbuzi wa haraka kuhakikisha wageni wote wanazingatia na kufuata utaratibu sahihi wa kuingia na kuishi nchini.

Wasira ameyaleza hayo leo Machi 23, 2025 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera ambao walimweleza kuwa kuna wageni kutoka nchi jirani wanapora ardhi ya Watanzania katika baadhi ya maeneo ya wilaya hizo.

“Nataka kuwaambia viongozi wetu wa vijiji na vitongoji msiwakaribishe, hatuwazuii kuja kwetu lakini waje kwa kufuata utaratibu. Mkiwaruhusu wakaingia wakajenga nyumba tena za kudumu siku ya kuwatoa itakuwa vita na watasema kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, kumbe kuna vita ya wageni na Watanzania walionyang’anywa ardhi,” ameema.

Amesisitiza kuwa kama kuna jambo gumu duniani ni ardhi, hivyo wananchi wa mipakani wakiruhusu ikaangiliwa itakuja kuleta shida hapo baadaye kwa kuwa ardhi haiongezeki, lakini watu wanaongezeka.

“Kama kuna jambo gumu duniani ni ardhi, mkiruhusu ardhi yenu ikaingiliwa, mnasema kubwa, huku mnazaa namna hii, watu wanaongezeka kwa asilimia tatu kwa mwaka. Wakati nchi inapata uhuru tulikuwa milioni nane lakini leo tuko watu milioni 63, hawa ni watu wengi wanaongezeka.

“Ardhi inabaki ile ile, kwa hiyo msisherehekee jambo hili, sisi tuliwapeni viongozi wa vijiji na vitongoji mamlaka ya kusimamia hakikisheni hawa wageni hawapewi ardhi na hawaingii bila utaratibu.

“Tunawaambia kabisa na hatuna ugomvi kule wanakotoka sisi ni rafiki zetu, lakini na sisi tukitoka hapa Karagwe tukahamia kule watatufukuza tena watatufukuza haraka maana wako wengi na ardhi yao ni ndogo, nchi yao ina watu milioni 12 lakini ukubwa wake ni unazidiwa na Mkoa wa Kagera,” amesema.