Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

KAMATI YA BUNGE UJENZI WA BARABARA YA TANGA-PANGANI BAGAMOYO UENDELEE KUPITIA ENEO LA HIFADHI YA TAIFA YA SAADANI

March 14, 2025 Add Comment


Na Oscar Assenga, PANGANI

KAMATI ya Kudumu ya Bunge Miundombinu imeshauri Serikali ujenzi wa barabara ya kutoka Tanga-Pangani –Bagamoyo upitie katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani ili kufungua mkoa huo kiuchumi na kuongeza idadi kubwa ya watalii.

Ushauri huo wa Kamati ulitolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Moshi Kakoso mara baada ya kamati hiyo kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani pamoja na kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Pangani

Alisema kwa sababu Serikali haijengi barabara kuwafurahisha wananchi bali kuufungua uchumi wa nchi sasa kama wanapeleka barabara na kuichepusha kwenye eneo ambalo lingekuwa na tija zaidi wanaomba hilo walifanyie upembuzi yakinifu huko serikali na wapate majibu ya msingi yenye ufanisi kwenye miradi ambayo ni ya kimkakati.

“Kujenga barabara hiyo wangeiacha na Serikali iliamua kujenga barabara upande wa ufukweni pembezoni mwa bahari ili ilete maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo sasa hawakatai kile kipande ambacho kimepita huko hivyo nendeni mkakae kile kipande ambacho kitakuwa kimebaki cha kukatisha pale nendeni mkakae mkiingize kwenye mfumo ambao mtaujua nyie”Alisema

Mwenyekiti hiyo alisema kwamba wakakae Wizara na Ofisi ya Makamu ya Rais ili kuangalia uwezekano wa barabara hiyo iweze kuifungua iende eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadan na kuweza kuufungua ushoroba wa utalii pamoja na kuifungua kiuchumi mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

“Mhe Naibu Waziri tunawapongeza kwa ujenzi unaoendelea wa daraja ni mzuri na maendeleo ya mradi wa daraja bunge limeridhishwa na litakapokamilika litaleta sura nzuri kwenye maeneo ya wilaya ya Pangani na mkoa na litakuwa kivutio na daraja pekee ambalo litakuwa juu sana na wanaona serikali uwekezaji wake utakuwa na tija zaidi”Alisema Mwenyekiti huyo wa kamati.

Hata hivyo akizungumza wakati akihitimisha ziara ya kamati hiyo aliishauri Serikali kuhakikisha inakamilisha haraka barabara ya Tanga-Pangani ili kuepusha serikali kutokuingia gharama nyengine za kulipa fidia.

Alisema kwamba uwekezaji unaowekezwa katika Daraja la Mto Pangani hautakuwa na maana iwapo barabara unganishi haitakuwepo huku akitaka lifanyiwe kazi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ili uende sambamba na daraja.

Hata hivyo aliiomba Serikali iwasimamie wakandarasi waweze kukamilisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa mkataba ambao mlishakubaliana nao wabunge wamehoji kuna wasiwasi kwamba ile miezi minne kwamba wanaweza kukamilisha kipande cha barabara na wasipowasimamia wataongeza muda mwengine wa ziada.

“Simamieni kile kipande kikamilike kije kuunga kwenye eneo la Barabara narudi kusema Bunge lingependa barabara ya Kutoka Tanga ingeenda kupitia eneo la Hifadhi ya Saadani wangekuwa wameufungua mkoa kiuchumi na kuongeza idadi ya watalii”Alisema

Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi Msonde wataendelea kufuatilia kuona wapi inakwama na nni kifanyike

Msimamizi wa Barabara ya Tanga-Pangani kutoka Wakala wa Barabarani nchini (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Godson Yohana alisema daraja la Mto Pangani lina urefu wa mita 525 ambapo kwa miradi ya madaraja nchini hilo ni daraja la pili kwa ukubwa na la kwanza ni Kigongo Busisi Mwanza.

Alisema ujenzi wa mradi huo ulianza Desemba 7 mwaka 2022 na gharama za mradi Bilioni 82.2 na unatekelezwa na Kampuni ya Shandon Likway Group ya kutokea nchini china na ujenzi huo umefikia asilimia 55 na unahusisha barabara na ujenzi wa daraja.

Mhandisi huyo alisema kwamba nguzo zote za kushika daraja zimekwisha kamilika na wanaendelea na ujenzi na mkandarasi yupo eneo la mradi huku akieleza ujenzi wa barabara loti ya kwanza umefikia asilimia 75 na mkandarasi mpaka sasa amekamiisha kipande cha kiliomita 15.8.

Alisema changaoto kubwa iliyowachelewesha kwenye mradi huo ni upatikanaji wa jiwe lenye sifa ya kutumika kwa lami ambayo wanaiweka hapo kutokana na uwepo wa teknolojia mpya kwamba mawe yanayotumika kusagia kokoto yanatakiwa kuwa na nguvu na viwango vya juu.

“Jiwe hilo tumelipata Muheza kilimota 60 kutoka eneo la mradi na walikuwa na leseni za watu wanaoyamiliki ilikuwa na changamoto kidogo lakini yamekamilila mradi huo unatarajiwa kukamilika 16June 2025”Alisema

Hata hivyo alisema kilomita zilizobaki ni 34 ambapo wanaishukuru Serikali tayari imemlipa mkandarasi huyo tokea Desemba mwaka jana kiasi cha Bilioni 4.7 na mwezi wa pili mwaka huu walilipaswa Bilioni 10.8.

Alisema mwanzoni walikuwa na changamoto mbalimbali kusimama kwa mradi na wamempa wiki mbili arudi kazi na kwa sasa wanaendele kuweka vifaa ili kuendelea na ujenzi huo

Mwisho.

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA SERIKALI KWA MABORESHO MAKUBWA YA MIUNDOMBINU BANDARI YA TANGA

March 13, 2025 Add Comment


Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Serikali kwa maboresho makubwa ya miundombinu katika Bandari ya Tanga ambayo yamekuwa chachu ya kuongeza ufanisi katika utendaji wake.

Kauli ya Kamati hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Moshi Kakoso baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maboresho na miundombinu ya sekta ya Uchukuzi katika Mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba kamati hiyo imeridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo hasa baada ya maboresho ya miundombinu iliyofanywa na Serikali na hivyo kuiongezea ufanisi wa kazi pamoja na ukusanyaji wa mapato.

“Kwa kweli sisi kama Kamati tumeridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka ya Bandari na nieleze kwamba tutaendelea kuisadia TPA kutimiza maono ya Rais na kufikia malengo yao na Serikali kwa ujumla”Alisema

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile aliishukuru kamati kwa ziara yao iliyowawezesha kujionea kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika katika kuboresha sekta hiyo.

“Niwahakikishie kamati kwamba maoni, ushauri na maelekezo mliyoyatoa yatafanyiwa kazi kuhakikisha mkoa wa Tanga unafunguka kiuchumi kutokana na maboresho yanayoendelea kufanywa na Wizara ya Uchukuzi”Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Plasduce Mbosa alisema kukamilika awamu ya mbili za maboresho ya maboresho ya Bandari ya Tanga kwa gharama ya shilingi Bilioni 429.1 kumekuwa chachu ya maendeleo na kufungua ushoroba wa kanda ya kaskazini.

“Niishukuru kamati ya kudumu ya Bunge Miundombinu kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa TPA ili mamlaka hiyo iweze kutekeleza mipango yake ya maboresho ya Bandari na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa Taifa “Alisema

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE ZIARANI JAPAN AKUTANA NA VIONGOZI, KUSUKUMA AJENDA YA ELIMU

March 13, 2025 Add Comment
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bw. Yohei Sasakawa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nippon jijini Tokyo. Bw. Sasakawa, mwenye umri wa miaka 86, ni mtu mashuhuri wa kusaidia miradi ya kijamii duniani. Katika mazungumzo yao, waligusia nafasi ya sekta binafsi katika kusaidia elimu, hasa kupitia taasisi zisizo za kiserikali. Vilevile, Bw. Sasakawa alishangaza dunia baada ya kufanikisha kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 12 Februari 2024, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 85 ya kuzaliwa kwake – hatua inayothibitisha kuwa umri si kikwazo kwa ndoto kubwa.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Waziri wa Fedha wa Japan Mhe. Atsushi Mimura jijini Tokyo














 Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), yupo Tokyo nchini Japan kwa ziara maalum yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya GPE na serikali ya Japan katika kutatua changamoto za elimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.

 

Katika siku yake ya kwanza Tokyo, Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama, pamoja na Naibu wake, Mhe. Atsushi Mimura. Mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kifedha ili kusaidia miradi ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa nchi zinazoendelea.

 

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Mstaafu Kikwete alikutana na Bw. Akihiko Tanaka, Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA). Shirika hili limekuwa na mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika, na mazungumzo yalihusu namna JICA inaweza kusaidia jitihada za GPE katika kukuza elimu bora.

 

Dkt. Kikwete pia alikutana na Bw. Yohei Sasakawa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nippon. Bw. Sasakawa, mwenye umri wa miaka 86, ni mtu mashuhuri wa kusaidia miradi ya kijamii duniani. Katika mazungumzo yao, waligusia nafasi ya sekta binafsi katika kusaidia elimu, hasa kupitia taasisi zisizo za kiserikali. Vilevile, Bw. Sasakawa alishangaza dunia baada ya kufanikisha kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 12 Februari 2024, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 85 ya kuzaliwa kwake – hatua inayothibitisha kuwa umri si kikwazo kwa ndoto kubwa.

 

Katika siku zinazofuata, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. T. Miyaji, pamoja na wabunge wa Bunge la Japan, ambapo ajenda kuu itakuwa nafasi ya elimu na teknolojia katika maendeleo ya jamii. Pia, atashiriki mijadala maalum kuhusu elimu na teknolojia, kufanya mahojiano na vyombo vya habari, pamoja na kukutana na Mhe. Tetsuro Yano, Rais wa Taasisi ya AFRECO, ambayo inahusika na kukuza ushirikiano kati ya Japan na Afrika.

 

Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Dkt. Kikwete katika kuboresha mifumo ya elimu duniani, hasa katika nchi zinazoendelea. Japan ni mshirika muhimu wa maendeleo ya elimu barani Afrika, na ushirikiano huu unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata fursa ya elimu bora.

 

ENDS

RC TANGA ALIPONGEZA SHIRIKA LA TASAC KWA UTOAJI WA ELIMU JUU YA MADHARA YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA YA BAHARI

March 12, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga,TANGA


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepongeza kutokana na juhudi zake kubwa za kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wadau mbalimbali juu ya madhara yatokanayo na uchafuzi wa mazingira ya bahari ambayo yanaweza kuelekea athari za kiuchumi kwa mtu moja moja na Taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt.Batilda Buriani wakati akifungua warsha ya mpango wa Taifa wa kujiandaa na mapambano ya umwagikaji wa mafuta katika bahati na mafuta.

Ambapo alisema licha ya sekta ya uchumi kuathirika kuna uwezekano mkubwa wa kupotea kwa viumbe vya bahari endapo juhudi mbalimbali hazitafanyika.

Aidha alisema kwamba jamii inapaswa kutambua umwagikaji wa mafuta katika bahari na maziwa unaweza ukaathiri vyanzo vya mapato ya wananchi wakiwemo wavuvi na hivy kuathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini Taifa kwa ujumla

"Niseme tu kwamba Semina hii ina umuhimu mkubwa kwani mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo na kivifaa.



“Kwa kweli tunalipongeza shirika la TASAC kwa juhudi mbalimbali inazozifanya ikiwemo kutoa elimu jumuishi pamoja na ugawaji wa vifaa vinavyoweza kutumika wakati wa dharuraniwatake kuendelea kuongeza elimu hiyo kwa wadau wakiwemo wananchi sambamaba na kuwa na vifaa vya kutosha”Alisema



Hata hivyo alitumia wasaa huo kusifu juhudi za shirika hili la kutoa vifaa vya kukabiliana na changamoto hizo huku akitaka lazima wawe na utaribu mzuri wa kuvitumia ili kuweza kufikiwa kwa urahisi ili oparesheni ikitokea iwe rahisi kuvipata.


Alisema mkoa umejipanga kutoa elimu kwa wadau wote wa bahari pamoja na wananchi jinsi ya kutumia vifaa vitakavyotumika wakati wa kupambana na dharura ya umwagikaji wa mafuta hii ikilenga kuongeza zaidi ushirikiano katika kupambana na majanga pale yatakapotokea.


"Bandari ya Tanga hususani eneo la Chongoleani linatarajiwa kuwa lango kuu la kupokea na kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Chongoleani , ujenzi wa bomba hilo upo katika hatua za mwisho wenzetu tayari wameshaweka matank ya kuhifadhia mafuta, Mkoa una mashamba ya mafuta umeyatenga tumeshatenga vitalu ambapo wenzetu wa makampuni makubwa wana maeneo yao"

"Umuhimu wa hii semini ni mkubwa sana mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo, kivifaa.



Awali akizungumza Mkurugenzi wa Idara ya Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira kutoka TASAC Leticia Mutaki alisema kuwa katika kuendelea kudhibiti na kupambana na athari za kimazingira katika bahari shirika hilo linaendelea kutekeleza mpango wa kitaifa wa umwagikaji wa mafuta.



Ambapo alisema mpango huo unahusisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika ngazi za wilaya hii ikiwa na lengo la kuongeza uelewa na itayati wa kupambana na majanga yanapotokea.



Aidha Mutaki alisema kuwa TASAC inaendelea kusiamamia usalama wa vyombo vyote vinavyofanya safari katika bahati kuhakikisha vinakuwa na ubora wakati wote hii ikiwa na lengo la kupambana na athari za kimazingira ambazo zinaweza kujitokeza na kuelekea athari kwa viumbe na rasilimali nyingine zinazopatikana baharini.


"Pia tunashughulika na usalama wa vyombo vinavyopita kwenye maji tunaviangalia ili visichafue mazingira yetu sasa hivi tuna suala la uchumi wa buluu ambao sasa hivi Duniani imeelekeza kwamba Kuna maliasili nyingi kwenye maji lazima tuvune kwa namna ambayo itaweza kuwa endelevu TASAC tunawajibu wa kuhakikisha kwamba maliasili zote zilizopo kwenye maji zinabaki salama"



Alisema wamekuja mkoani hapa kujenga timu ili kunatokea bahati mbaya ya umwagikaji wa mafuta ili wawe na watu ambao wanaweza kufanya nao kazi katika kudhibiti athari zianazoweza kujitokeza kutokana na mafuta mabayo yanavuja.



“Tunao mradi wa EACOP ambao unaosafirisha mafuta kutoka kule Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania kama itatokea dharira yeyote ya umwagikaji wa mafuta ili kuweza kupunguza athari za kimazingira" Alisema.



Hata hivyo Mwakilishi kutoka shirika la bandari Zanzibar Abubakar Ally amelipongeze shirika la uwakala wa Meli Tanzania 'TASAC' kutokana na mafunzo hayo ambayo wameendelea kuyatoa kwa wadau wa usafirishaji wa majini pamoja na wananchi ambapo matokeo yake yameonekana na kufanikiwa kwa asilimia kubwa.

Mwisho.
Tanzania na Russia Zaongeza Ushirikiano wa Kisayansi katika Uhifadhi wa Misitu

Tanzania na Russia Zaongeza Ushirikiano wa Kisayansi katika Uhifadhi wa Misitu

March 12, 2025 Add Comment




PHOTO-2025-03-11-17-46-17.jpg
Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu
PHOTO-2025-03-11-17-44-24.jpg
Prof Silayo na Wageni toka Russia

PHOTO-2025-03-11-17-42-38.jpg
Wataalamu Kutoka Russia wakifuatilia wasilisho

PHOTO-2025-03-11-17-37-27.jpg
Tunafuatilia
PHOTO-2025-03-11-17-35-33.jpg
tunafuatilia
PHOTO-2025-03-11-17-29-11.jpg
Picha ya pamoja

PHOTO-2025-03-11-17-16-45.jpg

Morogoro – Tanzania imepiga hatua muhimu katika sekta ya misitu baada ya wataalamu wa misitu kutoka Russia kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kwa lengo la kujadili na kuimarisha utafiti wa kisayansi katika uhifadhi wa misitu.

Ziara hiyo iliyofanyika Machi 11,2025, iliyojumuisha maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi, Profesa Dos Santos Silayo, ililenga kuboresha ushirikiano wa kisayansi, kielimu na kiteknolojia kati ya Tanzania na Russia katika sekta ya misitu na uhifadhi wa mazingira.

Wataalamu hao wa misitu, wakiongozwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ufundi wa Misitu cha Jimbo la Saint Petersburg, Chuo Kikuu cha Petrozavodsk na Chuo Kikuu cha Misitu na Teknolojia cha Jimbo la Voronezh, walijadili maeneo mbalimbali ya utafiti wa pamoja. TAFORI iliwasilisha tafiti muhimu zilizoainisha fursa za kushirikiana katika nyanja za ikolojia, usimamizi wa misitu na teknolojia za kisasa za uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho, Profesa Silayo alieleza kuwa ushirikiano huu unalenga kutatua changamoto zinazokabili sekta ya misitu, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, magonjwa ya mimea na matumizi ya teknolojia bunifu kama setilaiti na ndege zisizo na rubani (drones) katika usimamizi wa misitu.

“Ushirikiano huu unaleta pamoja wataalamu wa Tanzania na Russia, na tunatarajia kunufaika kupitia kubadilishana maarifa na uzoefu wa kisayansi,” alisema Profesa Silayo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI, Dk Revocatus Mushumbusi, alisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika utafiti wa misitu, hususan katika kukabiliana na moto wa misitu na kuendeleza mbinu za kisasa za utafiti.

“Ushirikiano huu utatufundisha mbinu mpya na teknolojia zinazotumika Russia, ambazo zinaweza kusaidia kuboresha uhifadhi wetu wa misitu,” alisema Dk Mushumbusi.

Watafiti kutoka Russia walielezea mafanikio yao katika matumizi ya teknolojia za kisasa kama setilaiti na drones ili kutathmini hali ya misitu kwa ufanisi mkubwa. Aidha, waligusia umuhimu wa utafiti wa pamoja katika maeneo ya uzalishaji wa miti bora, entomolojia na matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI) katika usimamizi wa misitu.

Mtafiti Mkuu wa TAFORI, Dk Chelestino Peter Balama, alibainisha kuwa taasisi hiyo imepiga hatua katika uhifadhi wa mazingira na kulinda mimea iliyo hatarini kutoweka, akisisitiza kuwa ushirikiano huu utaongeza ufanisi katika juhudi hizo.

Ziara hii inatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo zaidi katika sekta ya misitu kwa kubadilishana ujuzi, utafiti na teknolojia kati ya Tanzania na Russia, ikiwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha uhifadhi endelevu wa misitu nchini.

Tulizo Henry Kilaga I A Brand Communication Strategist,

Located: Dodoma I Dar es Salaam - Tanzania. 

Call/WhatsApp: +255 765 888887

www.thestrategist.co.tz