Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA

December 12, 2024 Add Comment

 


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akitoa vyeti kwa Wahitimu Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.



Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza  Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.


Matukio Mbalimbali Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.

Na Mwandishi Wetu,Pwani

KATIKA kuimarisha huduma za afya serikali inaendelea na juhudi za ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu na huduma za afya katika hospitali zote kuanzia ngazi za chini hadi hospitali za rufaa.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024. Amesema kuwa serikali imejipanga vyema ili kuhakiisha kwamba inakuwa na vifaa bora na vya kisasa kwaajili ya kujifunzia na kutoa huduma za afya katika ngazi zote nchini.

"Maono ya Rais Dkt. Samia hayawezi kuwa na tija kama kutakosekana wataalamu wa kufanya kazi ndio maana nawapongeza kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita kwa kuzalisha wataalamu wasaidizi katika fani Utabibu, Uuguzi, Ukunga, Famasia na wataalamu wa Maabara.

"Juhudi zenu tunazijua na tunazitambua ndugu zanguni endeleeni kuzingatia ubora maana wahitimu hawa si kwamba wanakwenda kuokoa maisha ya watu wetu bali hata sisi hapa ni wateja wao tunaomba muwapokee mtakapokuwa huko makazini"

Akijibu risala ya Mkuu wa Chuo hicho, Kipanga amesema kuwa atawasiliana na TAMISEMI pamoja na TARURA ya Mkoa wa Pwani ili kuona namna bora ya kuboresha miundombinu ya barabara ya kufika hapa chuoni na katika kampasi nyingine kama zilivyoandikwa kwenye risala.

Pia ametoa wito wa wahitimu hao kuonesha weledi katika kazi kwasababu kusoma ni jambo jingine na kufanya kazi ni jambo jingine, unaweza ukasoma lakini usielimike.

"Wito wangu kwenu ni kahakikisha yale ambayo mmeyapata mnakwenda kuyatumia pale mnapoenda kufanya kazi kwa weledi." Amesema Kipanga

Pia amewaasa kuepuka masuala ya rushwa ufisadi na kujikinga na magonjwa mbambali kwani taifa linawahitaji sana.

Aidha amesema ni muhimu mkafahamu kwamba elimu haina mwisho kimsingi wanavyosheherekea mahafali wajuae kwamba wamefungua njia ya kuendeleza taaluma waliyopata hadi wawe wataalamu bobezi katika fani zao.

Kwa Upande wa Mkuu wa Chuo, Kelvin Kenan ameiomba serikali kuwasaidia kutengeneza miundombinu ya barabara itakayofika chuoni hapo ili kuchochea maendeleo zaidi katika chuo hicho.

Kwa upande wa Wahitimu wa Chuo hicho wamewashukuru wakufunzi wao lakini pia wameomba kuwepo na bajeti za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ili kuweza kupata elimu bora.

Pia wameiomba serikali kuwapatia mikopo wanafunzi wa vyuo vya kati kwani changamoto kubwa ni kutokuwa na fedha za kujikimu kimaisha wawapo chuoni.

Licha ya hayo wameomba kuwe na fursa ya wahitumu wa chuo hicho kwenda kusoma nje ya nchi kama ilivyo vyuo vikuu vingine.

MWANAFUNZI LIGHTNESS AOMBA SAPOTI YA RAIS SAMIA, FLAVIANA MATATA AWE MWANAMITINDO WA KIMATAIFA

December 01, 2024 Add Comment

 

Mwanafunzi Lightness Enock Ngwangwalu mwenye umri wa miaka 16 aliyemaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mbabala, Dodoma amesema ndoto yake ni kuwa mwanamitindo wa Kimataifa hivyo anaomba msaada kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata ili aendelezwe hadi kufikia ndoto yake hiyo.

Alifikia kuomba msaada huo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii baada ya kuongoza vyema shoo ya wanafunzi wenzie waliovalia mitindo mbalimbali ya mavazi wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo.



Lightness akieleza jinsi alivyofanikisha shoo hiyo ya mitindo ya mavazi.


Lightness Enock Ngwangwalu.




 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MSIMAMIZI MKUU KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203 Mwanafunzi Lightness Enock Ngwangwalu mwenye umri wa miaka 16 aliyemaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mbabala, Dodoma amesema ndoto yake ni kuwa mwanamitindo wa Kimataifa hivyo anaomba msaada kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata ili aendelezwe hadi kufikia ndoto yake hiyo. Alifikia kuomba msaada huo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii baada ya kuongoza vyema shoo ya wanafunzi wenzie waliovalia mitindo mbalimbali ya mavazi wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo. Lightness akieleza jinsi alivyofanikisha shoo hiyo ya mitindo ya mavazi. Baadhi ya wanafunzi walioshiriki shoo hiyo ya mitindo ya mavazi. Lightness Enock Ngwangwalu.

ENOCK KOOLA ACHANGIA MILIONI 6.5 AGAPE LUTHERAN SEMINARY

November 25, 2024 Add Comment



Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro 

Mdau wa maendeleo ya jamii na Wananchi kwa ujumla Bwana  *Enock Koola* ambaye ni MCHUMI kitaaluma , amechangia sh 6,500 000 ( milioni sita na laki tano ) kwa ajili ya ujenzi wa  jengo jipya ya ghorofa tatu ambalo linatarajiwa kuwa na Maktaba  ya kisasa  chumba Cha computer na ukumbi wa Mithiian 

Enock Koola  alitoa mchango huo kwenye hafla  ya mahafali ya 28 ya kidato cha 4 yaliyofanyika shuleni hapo Agape seminary iliyopo kata ya Mamba wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo ndugu Enock Koola alikuwa mgeni rasmi .
 
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bwana Koola  alisema fedha hizo zimetolewa na yeye pamoja na familia yake kwa lengo la kusaidia ujenzi wa maktaba hiyo, ambayo itawawezesha wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa weledi na kufikia malengo yao katika masomo. “Huu ni mchango wetu kwa wanafunzi wa Agape Seminary ili waweze kupata mazingira bora ya kujifunza. Niwaombe wazazi na walezi ambao watoto wao wanasoma hapa, wawe mfano kwa kuchangia maendeleo ya shule hii, hasa katika ujenzi wa maktaba hii,” alisema Bwana Koola .


Aidha, alizungumzia umuhimu wa kushiriki katika maendeleo ya elimu na kuwa sehemu ya mabadiliko chanya. “Elimu ni nguzo muhimu katika jamii na ndiyo ufunguo wa maisha. Nawaomba wazazi muwe sehemu ya mabadiliko, ili watoto wetu wapate elimu bora,” aliongeza.

 Koola pia alipongeza juhudi za uongozi wa Shule ya Agape Seminary, akimshukuru Mkuu wa Shule na Viongozi wa dini   wa Kanisa la Kiutheri ( KKKT)   Dayosisi ya kaskazini  kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea katika shule hiyo ikiwa ni pamoja na huduma za Afya 
. Alisema kuwa shule hiyo inatoa mchango mkubwa kwa jamii kwa kuandaa vijana wenye elimu bora, na kwa kutoa  ajira kwa walimu 32 na watumishi wengine 21 wa shule hiyo .


 Koola alimalizia kwa kutoa ahadi kwa wanafunzi wa shule hiyo, akisema: “Nikiwa kama mdau wa maendeleo, mimi naahidi  zawadi kwa wanafunzi wote watakaofaulu kwa division 1, ili kuwapongeza kwa juhudi zao.”

Katika hotuba yake, Koola  alitoa miongozo muhimu kwa wahitimu wa shule hiyo;
Alisisitiza umuhimu wa kumcha Mungu, kuwa na umakini katika masomo, na kuepuka mienendo mibaya  kama vile ulevi na uasherati. 

. “Safari yenu imeanza rasmi, na ni muhimu kuongeza juhudi katika elimu yenu. Kuwa na hofu ya Mungu, jitunze kiroho na kimwili, na ujipe nafasi ya kufanikiwa,” alisema.

Aliongeza: “Kwa wanafunzi wa leo, ambaye atapata nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha sita, ni muhimu kuwa na malengo na juhudi za kufikia ndoto zako. Kumbukeni kwamba elimu ni ufunguo wa mafanikio ya baadaye.”


Aidha Koola  pia aliwashukuru wazazi, walezi na wachungaji walioshiriki katika mahafali hayo, na kuwataka washiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na kijamii. Aliwahimiza kushiriki kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakafanyika  tarehe 27 November mwaka huu  na kuwachagua  viongozi wenye maadili mema, utashi na uwezo wa  kuchochea maendeleo katika taifa letu.


Kwa upande mwingine, Mkuu wa Shule ya Agape  Lutheran Seminary , Goodluck  Lyimo  alisisitiza umuhimu wa nidhamu kwa wanafunzi, akiwataka kuwa mfano mzuri katika jamii, hasa wanapokuwa nyumbani au wanapohitimu. “Nidhamu ni msingi wa mafanikio, na nashukuru kwa malezi bora mliyopata hapa shule,” alisisitiza

WADAU WA MADINI WAPEWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA KEMIKALI

November 09, 2024 Add Comment


Na Okello Thomas

Wadau wanaojishughulisha na matumizi ya kemikali Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wamehimizwa kuzingatia Sheria na Kanuni za matumizi ya kemikali ili kuondokana na athari ambazo hujitokeza endapo kemikali hazitotumika kwa kuzingatia usalama.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga alitoa wito huo wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi salama wa Kemikali kwa wadau wanaojihusisha na shughuli za kemikali katika mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika leo katika Hoteli ya Omary City iliyopo wilayani Chunya.

“Kemikali hutumika katika uchimbaji na uchakataji wa madini, hivyo kemikali hizi zinahitaji uangalifu katika kutumia, kutunza ili kuepuka kusababisha madhara mbalimbali kwa watumiaji, wauzaji, wanyama na mazingira,” alisema Mhe. Batenga.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ya usimamizi salama wa kemikali kwani uchimbaji wa madini huchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo Mamlaka iendelee kutoa elimu ya kemikali kwani wadau wapo wengi.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima amewataka wadau walioshiriki mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kuwa mabalozi kwa jamii lakini pia ametoa wito kwa wadau ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo, kuwa mafunzo hayo ni endelevu hivyo wawe tayari kushiriki wakati Mamlaka itakapotangaza tena.

“Hii elimu tutaendelea kutoa mara kwa mara kwa wadau na kuhakikisha kwamba kemikali zinatumika vizuri na hazileti madhara kwa watumiaji wenyewe, lakini pia na jamii inayowazunguka, alisema Mulima.

Naye Omary Hamisi kutoka kampuni ya Small Scale Miners - Chunya, ameishukuru Mamlaka kwa kuwafikia na kuwapa elimu ya matumizi salama ya kemikali kwa sababu wamekutana na mambo mengi ya kigeni kwenye masuala ya matumizi ya kemikali ikiwemo kuzifahamu sheria, alama za kemikali, utunzaji na namna ya utumiaji wa kemikali hatarishi.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga, (aliyesimama) akiongea wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau mbalimbali wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya, katika Hotel ya Omary City Chunya, Novemba 07, 2024
Meneja, Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima, akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, kufungua mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya, yaliyofanyika katika Hotel ya Omary City Chunya, Novemba 07, 2024.

Meneja Mulima amesema kuwa mafunzo hayo siku mbili kuanzia Novemba 07-08, 2024 katika Mkoa wa Kimadini Chunya, yamelenga kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau mbalimbali wanaoshughulika na matumizi ya kemikali kuhusu matumizi yaliyo salama ya kemikali kwa afya zao na Mazingira kwa ujumla.



Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Chunya, Eng. Laurent Mayale , akiongea kuwasalimu washiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya.

Mwenyekiti wa Wachimbaji madini Mkoa wa Mbeya, Saddam Kyando akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya



Washiriki wa mafunzo kutoka Mkoa wa Kimadini Chunya, wakimsikiliza Mgeni rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya.


Watumishi wa Mamlaka kutoka Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Georgina Kilindo, (picha ya juu) na Jansen Bilaro, (picha ya chini) wakiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya.


Munisi Jonas kutoka kampuni ya Anglo De Beer (pcha ya juu, aliyesimama) na Paschal Kalonga kutoka Kampilipili Gold Family (picha ya chini, aliyesimama) wakitoa maoni yao kwenye mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali kwa wadau wanaojishughulisha na kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya.


Washiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa Kemikali, Michael Makosa (picha ya juu aliyesimama) na Bahati Muhanga (picha ya chini aliyeshika kipaza sauti) wakiuliza maswali mbalimbali baada ya mawasilisho ya mada.


Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga, (katikakati waliokaa) akiwa na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na masuala ya kemikali katika Mkoa wa Kimadini Chunya baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya Umsamizi wa kemikali Omary City Hotel Chunya, Novemba 07,2024