Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA NCHINI TANZANIA-WAZIRI MHAGAMA

December 02, 2024 Add Comment

 

Leo ni tarehe 1 Desemba 2024, ambapo dunia inaadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani. Kitaifa, maadhimisho haya yamefanyika Mkoani Ruvuma yakiongozwa na mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Philip Mpango.

Akitoa taarifa yake, Waziri wa Afya nchini, Mheshimiwa Jenista Mhagama, ameeleza juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. 

Amesema, Serikali imeendelea kugharamia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs), hatua inayosaidia wananchi wanaoishi na maambukizi ya virusi hivyo kuendelea na maisha ya kawaida.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, wananchi takriban milioni 1.7 wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini. 

Serikali imetumia shilingi bilioni 750 kununua dawa za ARVs, ambapo gharama ya matibabu kwa kila mgonjwa mmoja ni takriban shilingi 400,000 kwa mwaka.

"Maadhimisho haya ni fursa muhimu ya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na kupunguza unyanyapaa" amesema Mhe. Jenista

Pamoja na hayo  amehimiza jamii kuchukua hatua za kinga na matibabu kwa ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali. 

Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuimarisha mshikamano wa kidunia katika kukomesha maambukizi mapya na kuboresha huduma kwa walioathirika.

MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA NCHINI TANZANIA-WAZIRI MHAGAMA

December 01, 2024 Add Comment




Leo ni tarehe 1 Desemba 2024, ambapo dunia inaadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani. Kitaifa, maadhimisho haya yamefanyika Mkoani Ruvuma yakiongozwa na mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Philip Mpango.


Akitoa taarifa yake, Waziri wa Afya nchini, Mheshimiwa Jenista Mhagama, ameeleza juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. 


Amesema, Serikali imeendelea kugharamia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs), hatua inayosaidia wananchi wanaoishi na maambukizi ya virusi hivyo kuendelea na maisha ya kawaida.


Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, wananchi takriban milioni 1.7 wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini. 


Serikali imetumia shilingi bilioni 750 kununua dawa za ARVs, ambapo gharama ya matibabu kwa kila mgonjwa mmoja ni takriban shilingi 400,000 kwa mwaka.


"Maadhimisho haya ni fursa muhimu ya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na kupunguza unyanyapaa" amesema Mhe. Jenister


Pamoja na hayo  amehimiza jamii kuchukua hatua za kinga na matibabu kwa ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali. 


Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuimarisha mshikamano wa kidunia katika kukomesha maambukizi mapya na kuboresha huduma kwa walioathirika.

SERIKALI YADHAMIRIA KUMALIZA TATIZO LA UKIMWI NCHINI

December 01, 2024 Add Comment


Siku ya Ukimwi Duniani, Imeadhimishwa Kitaifa leo tarehe 01/12/2024, maadhimisho yamefanyika katika Uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. 

Hafla hii imeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ambaye amesisitiza azma ya serikali kuhakikisha inatokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) nchini

Katika hotuba yake, Mhe. Dkt. Mpango, ameonesha dhamira ya dhati ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupambana na maambukizi mapya ya VVU.

Takwimu zinaonesha kwamba vijana, hasa wa kike, wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, serikali imeweka mkazo mkubwa katika kutoa elimu kwa vijana ili kuwasaidia kujitambua, kuchukua hatua za kujikinga, na kwa wale wanaoishi na VVU, kuhakikisha wanafuata taratibu kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs).

Aidha, Mhe. Dkt. Mpango ametoa wito kwa jamii nzima kushirikiana, kuhakikisha kwamba maambukizi mapya yanapungua, kwa kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi, matumizi sahihi ya kinga, na upimaji wa afya mara kwa mara


WAZIRI MHAGAMA AZINDUA USAMBAZAJI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI 2022-2023

November 29, 2024 Add Comment




Na.Mwandishi Wetu -Ruvuma

Waziri Afya Mheshimiwa Jenista Mhagama amezindua Usambazaji wa Ripoti ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI 2022-2023 Mkoani Ruvuma.


 Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma tarehe 29 Novemba, 2024 Waziri Mhagama alieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya UKIMWI nchini Tanzania ambapo imeelezwa kuwa kiwango cha Maambukizi Mapya kimepungua huku akipongeza juhudu zinazofanywa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Nchini 

"Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kiwango cha maambukizi ya UKIMWI nchini kimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 7 mwaka 2022 hadi asilimia 4.4 mwaka 2023. Aidha, juhudi za kupunguza maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto zimezaa matunda, ambapo kiwango cha maambukizi kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 8.1 mwaka 2023," alisema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama alieleza kuwa mafanikio haya yametokana na juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, sekta binafsi, na jamii katika kuimarisha programu za utoaji elimu, upimaji wa hiari, na matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs).


Alisisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi hizi ili kufikia malengo ya kumaliza maambukizi mapya ya UKIMWI, hasa kwa watoto, ifikapo mwaka 2030. Vilevile, aliwahimiza wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi na kufuata ushauri wa kitaalamu.

Aidha alitoa wito kwa jamii kuunga mkono mikakati ya kitaifa ya kupambana na UKIMWI ili kuhakikisha maendeleo ya afya ya jamii na uchumi wa taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga, amesema Watanzania wamepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU)ambapo asilimia 98 ya Watanzania wanaohitaji dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo (ARVs) sasa wanatumia dawa hizo, hatua ambayo imevuka malengo yaliyowekwa kitaifa na kimataifa.

Mhe. Ummy alibainisha kuwa mafanikio haya ni matokeo ya jitihada za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu ya afya, upimaji wa hiari, na utoaji wa dawa kwa urahisi katika vituo vya afya.

Pia ametumia nafasi hiyo kuhimiza wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuendelea kutumia dawa kwa walioambukizwa ili kuboresha maisha yao na kupunguza maambukizi mapya.


Serikali inaendelea kuweka mikakati imara kuhakikisha kila Mtanzania anayehitaji huduma za matibabu anazipata kwa wakati.
Maadhimisho ya Wiki ya UKIMWI Duniani yanaadhimishwa Kitaifa mkoani Ruvuma yenye kauli Mbiu isemayo "Chagua Njia Sahihi, Tokomeza UKIMWI"

=MWISHO=

WAZAZI WENYE WATOTO WANAOISHI NA KIFAFA WALILIA TOTO AFYA CARD

November 26, 2024 Add Comment


Na Arodia PETER 


WAZAZI wenye watoto wanaougua ugonjwa wa kifafa wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kurudishia utaratibu wa Bima ya afya kwa watoto (Toto Afya Card) ili waweze kupata matibabu ya uhakika.


Walisema baada ya Serikali kusitisha utaratibu wa "Toto Afya Card" watoto wao wameacha kutumia dawa kutokana na gharama kubwa, hivyo kutishia uhai wao wa kuishi. 


Ombi hilo kwa serikali lilitolewa na baadhi ya wazazi wenye watoto wanaishi na hali ya kifafa waliohudhuria kongamano lililiandaliwa Chama cha Wazazi Wenye watoto wenye kifafa Tanzania (UWAKITA) kwa kushirikiana na Idara ya Afya ya Akili Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Jumamosi Novemba 23 mwaka huu. 



Mmoja wa wazazi hao, Glory Elihuruma Mrema mkazi wa Dar es Salaam alisema mtoto wake ameacha kwenda hospitali kuhudhuria kliniki na kupata dawa zaidi ya miezi 9 sasa kutokana na yeye kushindwa kumudu gharama hizo tangu bima ya watoto ilipositishwa na serikali. 


Alisema gharama za matibabu kwa watoto wenye ukifafa zina gharama kubwa kwa mtu ambaye hana kipato cha kutosha, jambo ambalo linatishia uhai wa watoto hao pamoja na kuwasababishia wazazi msongo wa mawazo.


"Kwa mfano kidonge kimoja cha mil gram 500 kinauzwa shilingi 1500 kwa bei ya rejareja. Na kwa mujibu wa watabibu wetu, mtoto mmoja anapaswa kumeza vidonge vinne kila siku, yaani viwili asubuhi na viwili jioni, hapo bado dawa ya usingizi ambayo kidonge kimoja kinauzwa shilingi 500. Hivyo kwa siku moja mgonjwa wa kifafa anatumia Shilingi 6500.



"Kilio changu kwa Rais wetu, Samia Suluhu Hassan atuangalie kwa jicho la pekee, watoto wanaoishi na kifafa usalama wao ni dawa na chakula. Kama mtoto mwenye hali hiyo hajanywa dawa, ndani hapakaliki, wazazi tumebaki majumbani  tunashindwa kufanya shughuli za kujitafutia kipato kwa sababu huwezi kumwacha huyu mtoto peke yake ndani." alisema Glory. 


Mzazi mwingine, Avelia Said ambaye mtoto wake anaishi na kifafa kwa miaka 17 sasa, anasema kilio chake kwa serikali ni kupata matibabu ya uhakika kwa mtoto wake.


Alisema gharama za dawa kwa siku ni zaidi ya Shilingi 6000, na yeye hana kipato baada ya mumewe kufariki mwezi Agosti mwaka huu. 


Anasema kwa sasa mtoto wake anaishi kwa kutegemea misaada ambapo mtu akimwonea huruma anamnunulia dawa za ziku tano au nusu mwezi, na zinapokwisha hali ya mtoto inazidi kuwa mbaya. 


"Ombi langu kuu sisi wenye watoto wanaotegemea kuishi kwa dawa, serikali ituangalie kwa jicho la kipekee tupate hiyo bima ya watoto ili watibiwe kwa uhakika"alisisitiza Avelia.


Naye daktari bingwa wa magonjwa Afya ya akili wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt Kuganda Said alisema inahitajika elimu sahihi kwa jamii kuhusu ugonjwa wa kifafa kwamba dawa na wataalam wapo na unatibika.


Dkt.Kuganda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa watoto wenye kifafa Tanzania  (UWAKITA), alisema chama hicho kinasisitiza elimu juu ya ugonjwa huo na jamii ielewe kwamba wataalam wa wapo, vifaa vya uchunguzi vipo na ugonjwa wa kifafa unatibika, hivyo watu waache unyanyapaa kwani ni kikwazo kwenye tiba ya ugonjwa huo.


Kwa upande wake,  Dkt. Nuruel Kitomary ambaye pia ni bingwa Afya na magonjwa ya akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili -Upanga Dar es Salaam, alisema zaidi ya watu milioni 50 duniani wanaishi na hali ya ukifafa; ambapo asilimia 80 wanatoka nchi zenye hali duni barani Afrika na Tanzania ikiwemo.


"Kati ya hao, watu milioni 10 wanaishi Afrika, na Tanzania  inakadiriwa kuwa na watu 450, 000 mpaka 500,000 wanaoishi na hali ya ukifafa ambapo ni asilimia 3.7 tu ndiyo wapo  kwenye matibabu.


"Hata hivyo hawa ni wale wenye usajili rasmi hospitalini, lakini kuna kundi kubwa nje ya hao ambao wamefichwa majumbani au wapo kwa waganga wa kienyeji, makanisani nakadhalika." alisema Dkt Kitomary.


Naye Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasiyoambukiza na afya ya akili kutoka Wizara ya Afya, Omary Ubuguyu alisema mkakati wa Serikali ni kuhakikisha vipimo na dawa ya msingi iitwayo phinobabitol inapatikana katika hospitali na vituo vya afya nchi nzima.


"Ingawa kuna dawa nyingine zaidi ya hiyo, lakini angalau hiyo ya msingi ambayo inasaidia kwa asilimia 70 wagonjwa wa kifafa inawasaidia.


Kuhusu bima ya afya, Dkt Ubuguyu alisema serikali ipo mbioni kukamilisha mpango wa afya kwa wote ambapo kila mtanzania atanufaika na huduma hiyo.