Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

VITUO VYA AFYA VITANO VIPYA VYAJENGWA WILAYA YA HAI

October 04, 2024 Add Comment

             


                  

Na WAF – Kilimanjaro

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwa kujenga vituo vya Afya Vitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 4, 2024 akiwa katika ziara ya siku Sita Mkoani Kilimanjaro ambao ameanza kwa kukagua na kuzindua miradi ya Sekta mbalimbali iliyotolewa fedha na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo Sekta ya Afya.

“Mkoa huu wa Kilimanjaro umepokea zaidi ya Bilioni 10 ili kutekeleza miradi ya Afya vilevile Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza milioni 150 kwa ajiri ya vifaa tiba vitakavyotumika katika kituo cha Afya Masama Kati.” Amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa kukamilisha ununuzi wa vifaa tiba ili Zahanati ya Kimashuku ianze kufanya kazi ifikapo Oktoba 30 mwaka huu.

“Kwa kuwa Mhe. Rais Samia ameleta Milioni 100 ya umaliziaji wa Zahanati hii na Milioni 50 ya ununuzi wa vifaa tiba, jambo la kwanza naomba fedha ya vifaa ipelekwe Bohari ya Dawa haraka sana, nimachotaka kuona Zahanati hii upatikanaji wa dawa usiwe wa mashaka.” Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama ameukata uongozi huo kuhakikisha huduma za uzazi wa dharula kwa kina mama zinapatikana ikiwemo vitanda maalum vya kujifungulia ili wakina mama wapate eneo salama na zuri la kujifungua na kuwapunguzia adha wananchi ya kufuata huduma hizo mbali.

“Tunatamani Zahanati hii iwe mkombozi kwa akina mama, wazee, vijana na watoto wetu, nitoe wito kwa Halmashauri yetu kuhakikisha Zahanati yetu inasimamiwa vizuri na tunaamini Zahanati hii itaenda kutoa huduma zinzotakiwa.” Amesisitiza Waziri Mhagama

Mwisho, Waziri Mhagama amewataka wananchi wote wa Hai kwenda kujiandikisha kuboresha taariza kwenye tume ya uchaguzi ili kupata fursa ya kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa ambao wanaleta maendelea katika maeneo yao.     

SERIKALI, SEKTA BINAFSI KUENDELEA KUSHIRIKIANA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KISASA KUTOA HUDUMA BORA

October 04, 2024 Add Comment



Na WAF, DAR ES SALAAM

Serikali kupitia Wizara ya Afya imezitaka Hospitali zote nchini ikiwemo za Sekta binafsi kuwekeza kwenye matumzi ya teknolojia na miundombinu za kisasa katika kutoa huduma za Afya ili kuendana na mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Dkt. John Jingu leo October 4,2024 alipotembelea Hospitali Binafsi ya Kairuki iyopo jijini Dar es Salaam na kujionea hatua mbalimbali za maendeleo ya utoaji wa huduma bora za afya katika Hospitali hiyo.

“Ajenda yetu Kubwa kwa sasa ni ubora wa huduma unaoendana na mazingira ya sasa hivi na mazingira ya dunia ya sasa ni ya kiteknolojia, tumetoka kuwapongeza wenzetu wa Hospitali ya Kairuki kwa uwekezaji mkubwa walioufanya, Lakini pia mnafahamu Serikali imewekeza kwenye Hospitali za umma na kununua vifaa vya teknolojia mbalimbali za kisasa ambazo zinatuwezesha kuto huduma bora.” Amesema Dkt. Jingu

Adha Dkt. Jingu ameipongeza Hospitali ya Kairuki na nyinginezo za sekta binafsi kwa namna zinavyojipambanua katika kutoa huduma bora za Afya na kuwa wadau wakubwa wa serikali kwa kusaidia utoaji huduma kwa wananchi.

“Kiufupi huduma zinatolewa vizuri, sekta binafsi ni mdau Mkubwa sana katika maendeleo lakini katika eneo hili ni mdau muhimu sana kwenye utoaji wa huduma za Afya. Ukija hapa utaungana na mimi katika hili na kuona sekta binafsi inahakikisha watanzania wanakuwa na afya njema.” Amesema Dkt. Jingu

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amezitaka Hospitali na watoa huduma za Afya ikiwemo sekta binafsi kuzingatia miongozo ya Afya katika kutoa huduma pamoja na huduma za upandikizaji mimba ambazo zimeanza kutolewa hapa nchini na kutaka huduma hizo kusambazwa vijijini.

“Wizara ya Afya inatengeneza miongozo na sera lakini pia inalea Hospitali na Vituo binafsi vya kutolea huduma ili tushirikiane kwa pamoja kutoa huduma kwa wananchi. Tumeanzisha pia huduma ya upandikizaji mimba watu wanahitaji huduma hii hivyo kuwa na huduma hizi nyingi zaidi ni wajibu wetu na tutaendelea kuhamasishana ili huduma hizi zifike mbali.” Amesema Prof. Nagu

Dkt. Asser Mchomvu ni Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya kairuki amesema hospitali itaendelea kuwekeza katika utoaji wa huduma bora ikiwemo huduma ya sasa ya uondoaji uvimbe bila kupasua ambayo hadi sasa imeshafanyika kwa wananchi zaidi ya mia moja.

“Zamani upasuaji ulikuwa unafanyika kwa kukata,ambapo kwanza unabaki na kidonda kisha kovu, lakini sasa hivi teknolojia imeongezeka unaweza kuondoa uvimbe bila kupasua na mtambo huo tunao hapa haukuachi na kidonda wala kovu.” Amesema Dkt. Mchomvu      

WAZIRI WA AFYA AANZA ZIARA MKOANI KILIMANJARO

WAZIRI WA AFYA AANZA ZIARA MKOANI KILIMANJARO

October 04, 2024 Add Comment

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameanza ziara yake ya siku Sita leo Oktoba 4, 2024 katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya Sekta ya Afya iliyotolewa fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika ziara yake Waziri Mhagama amekagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika kituo cha Afya Masama Kati na kuweka jiwe la msingi, ametembelea na kukagua jengo la kuhifadhia maiti pamoja na kuweka jiwe ka msingi katika kituo cha Afya Longoi, ametembelea na kukagua jengo la Zahanati ya Kimashuku na kuizindua.









WADAU WA AFYA NCHINI WAJADILI UMUHIMU WA KUWEKEZA KATIKA KINGA YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NA YANAYOAMBUKIZA

October 04, 2024 Add Comment

 


Mkurugenzi wa Mtendaji wa THPS Dkt.Redempta Mbatia akiwasilisha mada katika Jukwaa la Afya kwenye mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).
Mkurugenzi wa Mtendaji wa THPS Dkt.Redempta Mbatia akiwa katika Mduara 'Panel' wakati wa uwasilshaji wa mada katika Jukwaa la Afya kwenye mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).
Daktari Bingwa wa Hospitali ya Kibong’oto, Profesa Stella Mpagama akitoa mada kuhusu ujumuishaji wa matokeo ya utafiti wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kwa vitendo katika mifumo ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania wakati wa uwasilshaji katika Jukwaa la Afya kwenye mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya matibabu kupitia ima Tanzania Dkt. Ismail Gatalya, akiwasilisha mada kuhusu rasilimali fedha za afya kwa utaratibu wa bima unaozingatia magonjwa yasiyoambukiza katika Jukwaa la Afya kwenye mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).
Meneja Programu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) wa Wizara ya Afya Dkt.Prosper Faustine aliwasilisha mada kuhusu mafanikio na changamoto wanazopitia wapokea huduma za tiba na matunzo ya VVU wenye umri mkubwa katika Jukwaa la Afya kwenye mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).
Mkurugenzi Mtendaji na daktari mshauri katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Kisukari Prof. Kaushik Ramaiya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza na kupendekeza uundaji wa muundo jumuishi wa huduma za matunzo ya magonjwa sugu kwenye Jukwaa la Afya katika mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).

Picha ya pamoja ya wadau wa afya mara baada ya kuhitimisha mduara wa utoaji mada kwenye Jukwaa la Afya katika mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Zanzibar

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Redempta Mbatia amesema Tanzania inakabiliwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza, huku kukiwa na ongezeko la magonjwa ya kuambukiza, ikiwa ni pamoja na VVU, Kifua Kikuu na magonjwa mengine ya mlipuko.

Dkt.Mbatia aliyasema hayo katika Jukwaa la Afya katika mkutano wa 11 wadau wa Afya Tanzania (THS) lililondaliwa na THPS kwa kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC) lilofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar (ZITF).

Alisema jukwaa hilo lililenga kujadili namna nzuri ya kushughurikia magonjwa hayo katika kipindi ambacho bajeti ya afya nchini bado ni ndogo na pia katika miaka ya hivi karibuni hata ufadhili wa afua za afya umekuwa ukipungua kwa kiasi kikubwa.

Kwahiyo ni muhimu kwa sekta ya umma, kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali na sekta binafsi ili kuwekeza katika kinja na utoaji wa huduma za afya jumuishi.

Dkt. Mbatia alizumumzia uzoefu wa Shirika ya THPS katika kutoa huduma jumuishi za magonjwa yasiyoambukiza katika kliniki za tiba na matunzo za VVU nchini kwa kipindi cha Machi 2023 hadi Agosti 2024.

Aliongeza kuwa THPS inalenga katika kushughulikia changamoto mbalimbali za afya ya umma, ikiwa ni pamoja na VVU na UKIMWI, kifua kikuu, ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, huduma za afya ya uzazi, uzazi, watoto wachanga, watoto na vijana, maabara na mifumo ya taarifa za usimamizi wa afya, UVIKO- 19, na tathmini za afya ya umma.

Amesema mradi wa CDC/PEPFAR Afya Hatua (Oktoba, 2021- Septemba, 2026)

Kupitia mradi wa CDC/PEPFAR Afya Hatua ambao unatekelezwa katika mikoa minne ya Tanzania: Kigoma, Pwani, Shinyanga na Tanga, THPS imekuwa ikitoa huduma za kinga, matunzo, na matibabu ya VVU, ikijumuisha Tohara Kinga kwa wanaume (VMMC) katika mikoa ya Kigoma na Shinyanga, na Mpango wa DREAMS mkoani Shinyanga.


Mpango wa DREAMS ni mpango wa ambao unalenga wasichana rika balehe na wamama wadogo kwa ajili ya kuwapatiz huduma mbalimbali za VVU.

Jukwaa hilo lilijikita kwenye mada "Ushirikiano wa Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi katika huduma endelevu za kinga na matunzo katika kushughulikia magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza."

“Athari zinazohusiana na magonjwa yasiyoambukiza zinaongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha na gharama kubwa za huduma ya afya kwa magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na upungufu wa rasilimali ndani ya bajeti ya sekta ya afya na kupungua kwa ufadhili inabidi mtazamo wetu ujikite zaidi katika kuzuia magonjwa na kuunganisha huduma zenye gharama nafuu "amesema Dkt.Mbatia

Aidha Jukwaa hilo lililenga kuwaleta pamoja wataalam ili kujadili mikakati endelevu ya kushughulikia magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya kuambukiza nchini Tanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo.

"Ujumuishaji wa huduma bora wa huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu ndani ya huduma za VVU utaimarisha afya za wapokea huduma za tiba na matunzo, ubora na huduma zinazomlenga mtu binafsi na kupelekea kupata huduma za afya zilizo endelevu na thabiti." Alisema Dkt. George S. Mgomella Mkurugenzi wa Miradi CDC Tanzania.

Nae Mkurugenzi Mtendaji na daktari mshauri katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Kisukari Prof. Kaushik Ramaiya alitoa wasilisho kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kupendekeza uundaji wa muundo jumuishi wa huduma za matunzo ya magonjwa sugu.

Amesema wagonjwa wakipata huduma jumuishi kutapunguza vifo vya wenye ukimwi kutokana kudhibiti mapema kwa magonjwa yasioambukiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ndogo ya matibabu kupitia ima Tanzania Dkt. Ismail Gatalya, ambaye aliwasilisha mada kuhusu rasilimali fedha za afya kwa utaratibu wa bima unaozingatia magonjwa yasiyoambukiza.

Meneja Programu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) Dkt.Prosper Faustine aliwasilisha mada kuhusu mafanikio na changamoto wanazopitia wapokea huduma za tiba na matunzo ya VVU wenye umri mkubwa,

Daktari Bingwa wa Hospitali ya Kibong’oto, Prof. Stella Mpagama akijadili kuhusu ujumuishaji wa matokeo ya utafiti wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kwa vitendo katika mifumo ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania.

WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA MUHIMBILI UPANGA NA MLOGANZILA, ASEMA SERIKALI KUENDELEA KUENDELEA KUBORESHA UBORA WA HUDUMA NCHINI

September 10, 2024 Add Comment


WAZIRI wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma bora za afya popote alipo na kwa wakati.

Mhe. Mhagama ametoa kauli hiyo mapema leo, alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa lengo la kujionea namna hospitali hiyo inavyotoa huduma, ambapo ameupongeza uongozi na watumishi wa Muhimbili kwa namna wanavyotoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wananchi kwa kuzingatia weledi ubora unaotakiwa.

Mhe. Mhagama amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miundombinu, vifaa tiba vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu na kusomesha wataalam imewezesha wataalam hao hususani wa Muhimbili (Upanga &Mloganzila) kutoa huduma za ubingwa bobezi na kupunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

“Sekta ya afya hapa Tanzania ndani ya miaka hii mitatu imekuwa kuliko kipindi chochote kwani katika hospitali zetu za Taifa na kipekee Muhimbili tunazo zaidi ya aina 35 za matibabu ya ubingwa bobezi ikiwemo upandikizaji wa uloto, upandikizaji wa figo, matibabu ya magonjwa ya moyo n.k, uwekezaji ambao unaacha deni kwetu la kutoa huduma bora kwa Watanzania wenzetu ili waweze kufurahia matunda ya uwekezaji huo” amebainisha Mhe. Mhagama

Aidha, Mhe. Mhagama ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha na kuwajengea uwezo wataalam ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea duniani kwa lengo la kuendelea kuimarisha utoaji wa matibabu hapa nchini kadiri mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanavyojitokeza duniani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MNH Dkt. Ellen Senkoro amemuhakikishia Mhe. Waziri kuwa bodi itashirikiana na menejimenti kuhakikisha kuwa wanatafsiri kwa vitendo maono ya Mhe. Rais na maelekezo ya wizara hatimaye watu wote wanaotibiwa Muhimbili wapate huduma bora na zenye kukidhi matarajio yao.

Mhe. Waziri katika ziara yake ameambatana na viongozi mbalimbali wa Wiraza ya Afya akiwemo Naibu Katibu Mkuu Bw. Ismail Rumatila pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa wizara hiyo.