Na WMA – Dar es Salaam
16 Agosti 2026
Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo (WMA) wameshiriki katika CRDB Bank Marathon 2026, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo watumishi kutoka Makao Makuu Dodoma na WMA Mkoa wa Dar es Salaam waliungana na washiriki wengine katika mbio hizo.
Mbio hizo zilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na zililenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kuzingatia afya.
Ushiriki wa WMA katika mbio hizo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi ni msingi muhimu wa afya bora, huimarisha mwili na akili, husaidia kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuchangia kuongeza nguvu, uchangamfu na ufanisi katika shughuli za kila siku.
Watumishi walioshiriki katika mbio hizo wametoa shukrani za dhati kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, kwa kuwawezesha kushiriki katika CRDB Bank Marathon 2026, wakieleza kuwa fursa hiyo imewapa hamasa zaidi ya kuendelea kufanya mazoezi na kuzingatia afya zao.
WMA — Vipimo Sahihi, Afya Bora





EmoticonEmoticon