ORYX GAS ZANZIBAR YANOGESHA TAMASHA LA KIZIMKAZI,YAKABIDHI MITUNGI YA GESI 200

August 14, 2026
Na Mwandishi Wetu ,Zanzibar

ORYX Gas Zanzibar imeeleza hatua mbalimbali inazochukua kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na katika Tamasha la Kizimkazi kampuni hiyo imetoa mitungi ya gesi 200 huku mkakati kwasasa ni kutoa majenerata yanatotumia gesi ya LPG katika hoteli na viwanda visiwani Zanzibar.

Imesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika matumizi ya LPG na kwamba katika kipindi cha miaka sita matumizi ya nishati safi ilikuwa asilimia sita mwaka 2020 lakini mwaka 2025 ni zaidi ya asilimia 30 ya watumiaji wa nishati safi ya kupikia ya gesi na muamko huo umechangiwa na sekta binafsi,Serikali na wadau wengine.

Akizungumza katika kongamano la nishati safi lililofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi Zanzibar lililoanza Agosti 12 na kuhitimiswa leo Agosti 14,2026, Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Shuwekha Khamis amesema kampuni hiyo Oryx wanamchango mkubwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Hii kazi tumeianza muda mrefu na tumekuwa tukizisaidia taasisi katika mabadiliko na hapa Zanzibar oryx tumeshapiga hatua kuzibadilisha baadhi ya taasisi zikiwemo shule shule 25,Jeshi la Kujenga Uchumi, JKU kuna kambi sita Unguja na Pemba

“Pia kwa kushirikiana na Mwanamke Initiative Foundation tumebadilisha gereza la Kiinua Mguu , vituo vya polisi viwili, vituo vya afya 12 pamoja na baadhi ya ofisi za Serikali na ofisi nyingine.Kwahiyo tunaona kuna hatua kubwa ambayo tumeifanya katika kuzibadilisha taasisi.”

Awali katika tamasha hilo la Kizimkazi Oryx Gas imetoa mitungi ya gesi ya kupikia 250 bure kwa wananchi lengo likiwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hasa kwa kutambua mkakati wa Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »