KIZIMKAZI 2026: WIZARA YA NISHATI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

August 13, 2026


Wataalam wa Wizara ya Nishati wanaendelea kutoa elimu na ufafanuzi kwa wananchi wanaotembelea Banda la Wizara na taasisi zake katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, yanayofanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Wananchi wanapata fursa ya kufahamu shughuli, miradi na huduma mbalimbali zinazotekelezwa katika sekta ya nishati, ikiwemo masuala ya umeme, mafuta, gesi asilia na nishati safi ya kupikia.


Karibu tukuhudumie.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »