RC MTANDA AKABIDHI PIKIPIKI 18 KWA VIKUNDI 2 VYA VIJANA BUCHOSA

June 23, 2026



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 23 Juni, 2026 amekabidhi pikipiki 18 zenye thamani ya Tshs. Milioni 54.9 vya vikundi viwili vya vijana vya Bodaboda Lugasa na Waungwana Group Mbugani.


Akiongea kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mhe. Mtanda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye eneo la matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa maendeleo ya wananchi.

Halmashauri ya Buchosa inafanya vizuri sana , kwanza kwenye kukusanya mapato na pili kwenye kutumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kutumia mapato yao kununua vyombo kama pikipiki na kukopesha kwa vijana. Amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, ametoa wito kwa halmashauri hiyo kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo ili itumike kununua zingine na kuwezesha makundi mengine yaweze kukopeshwa.

Aidha, amewataka vijana walionufailka na mkopo huo kuheshimu sheria za usalama barabarani kwa kuendesha kwa staha kwa usalama wao na wa watumia barabara wengine aidha kuzitumia pia kwa malengo mahsusi na sio kuzizidishia matumizi.

"Hii siyo sadaka huu ni mkopo na dawa ya deni ni kulipa, wasiolrejsha mkopo wakamatwe wapelekwe polisi hadi walipe ili ikawasaidie wengine kuweza kukopeshwa" Ameongeza Mkuu wa Mkoa.





 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »