MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Selebosi amechukizwa na kitendo cha mabasi makubwa kuendelea kuzagaa katikati ya mji huku kituo rasmi cha mabasi cha Kange kikishindwa kufanya kazi ipasavyo licha ya Serikali kuwekeza mabilioni ya fedha.
Akizungumza kwenye kikao katika kikao cha Baraza la Madiwani ambapo alisema kuwa tayari walitoa maelekezo mabasi yote makubwa yaanze kutumia kituo hicho rasmi ili kupunguza msongamano wa magari mjini, lakini bado utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.
Meya huyo aliwataka LATRA na TARURA kushirikiana badala ya kuoneshana tofauti katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa sheria.

“Sote tunajenga nyumba moja. Isiwe kama kuna wivu wa ukusanyaji wa mapato,” alisema Selebosi.
Katika kauli yake iliyobeba hisia kali, Selebosi alikosoa kitendo cha mabasi kupakia abiria katika vituo vya mafuta badala ya kutumia stendi rasmi, akisema hali hiyo ni uvunjifu wa sheria unaofanyika waziwazi huku mamlaka zikiwa kimya.
“Leo kuna watu wana vituo vya mafuta lakini wanapakilia mabasi hapo hapo. Sheria inasemaje kuhusu hilo?” alihoji.
Aidha, Meya huyo alisema hatakuwa tayari kufumbia macho changamoto zinazolinyima Jiji mapato, akisisitiza kuwa nafasi yake amepewa na wananchi na si mtu binafsi.
“Nimepata udiwani na umeya kwa kura za wananchi. Nitabaki na msimamo wangu,” alisema.

Selebosi pia aliibua hoja ya hasara kubwa iliyopatikana katika kituo kikuu cha mabasi cha Tanga ambacho kilijengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 3 tangu mwaka 2008/2009, huku baadaye Serikali ikiendelea kuwekeza zaidi ya bilioni 8 katika maboresho ya mradi huo.
Kwa mujibu wa Meya huyo, kituo hicho kilikuwa mfano wa kuigwa nchini ambapo halmashauri mbalimbali zilifika kujifunza mfumo wa uwekezaji wake, lakini hadi sasa hakitumiki kikamilifu kutokana na uzembe wa utekelezaji.

“Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 8 lakini kituo hakifanyi kazi kama ilivyokusudiwa. Hii ni hasara kubwa kwa halmashauri na Serikali,” alisisitiza.

Mwisho, Selebosi aliwataka watendaji wa mamlaka mbalimbali kusimamia sheria bila kumuogopa mtu yeyote na kuhakikisha mabasi yote yanaelekezwa katika kituo rasmi ili kuongeza mapato ya halmashauri na kuondoa msongamano mjini.
Mwisho.
EmoticonEmoticon