
Na, Mwandishi wetu – Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amekutana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, katika ziara maalum ya kutembelea, kukagua na kutoa elimu katika Kituo cha Maarifa cha Mdaula kilichopo Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 18 Mei, 2026 ambapo Dkt. Yonazi alipata fursa ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Pwani, hususan katika utekelezaji wa Afua za masuala ya UKIMWI hasa huduma na mipango inayohusu WAVIU (Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI).
Taarifa hiyo ilieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii kwa wananchi wa mkoa huo.
Aidha kwa upande wake amesema Serikali kwa sasa imeongeza bajeti katika hutuma za VVU na UKIMWI ii kungeza ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi.
Zahanati ya Mdaula ilianza kutoa huduma za afya mwezi Oktoba mwaka 2022, ikiwa ni pamoja na huduma za wagonjwa wa nje, huduma za mama na mtoto, uzazi pamoja na huduma za chanjo kupitia kliniki tembezi. Kwa sasa, zahanati hiyo ina tawi dogo lililopo kandokando ya barabara ambalo linatoa huduma za maarifa ya jamii kwa wananchi na wasafiri wanaopita katika eneo hilo.
Tawi hilo lilifanyiwa maboresho na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kupitia Mradi wa SATTF uliokuwa unasimamiwa na TANROADS wakati wa utekelezaji wa ujenzi wake. Maboresho hayo yamelenga kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu na huduma zinazohusiana na mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na huduma nyingine za afya ya jamii. 
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon