TUME YA MADINI YASISITIZA ELIMU YA LOCAL CONTENT NA UTEKELEZAJI WA CSR

November 21, 2025

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, ametoa wito kwa Waratibu wa Local Content na CSR nchini kuimarisha elimu na usimamizi wa kanuni hizo katika ngazi zote za mikoa ili kuhakikisha Watanzania wananufaika kikamilifu na rasilimali za madini.


Mhandisi Lwamo amesema kuwa elimu ndiyo nguzo muhimu inayowasaidia wananchi kuchangamkia fursa za ajira, biashara na huduma ndani ya sekta ya madini, hasa katika kipindi hiki ambacho kampuni zinazomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100 zinatakiwa kutoa bidhaa na huduma mbalimbali kulingana na orodha iliyowekwa.


Ameongeza kuwa Waratibu wa Local Content na CSR wanapaswa kuwa viungo imara kati ya Makao Makuu ya Tume na Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa ili kuhakikisha utekelezaji wa kanuni unafanyika kwa uwazi, umakini na ufanisi.


Sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na mchango wake kufikia asilimia 10 ya Pato la Taifa, hivyo ni wajibu wa wadau wote kuhakikisha ukuaji huo unaleta manufaa makubwa kwa Watanzania.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »