Na Mwandishi Wetu, Handeni TC
MRADI wa Shule Bora upo hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa darasa jipya katika Shule ya Msingi Birikani, Halmashauri ya Mji Handeni, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elieskia Mmbuji, ametoa taarifa hiyo kwa Timu ya Usimamizi ya Halmashauri iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Maryam Ukwaju, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo.
Mmbuji amesema kuwa hadi sasa jumla ya Sh.11,774,310 zimetumika katika hatua mbalimbali za ujenzi, kati ya Sh. milioni 15 zilizopokelewa kutoka Mradi ya Shule Bora mnamo Mei 27, 2025.
Ameeleza kuwa ujenzi huo umeanzishwa kwa lengo la kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi na kuimarisha mazingira ya kujifunzia, jambo litakalosaidia walimu kutoa elimu bora zaidi.
“Ukamilishaji wa darasa hili utapunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya kujifunza, hivyo kuongeza ubora wa elimu katika shule yetu,” amesema Mmbuji.
EmoticonEmoticon