Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, akizungumza wakati akiwasilisha kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA)
....
Tanzania imepiga hatua muhimu katika kulinda mali ya kiakili na kudhibiti bidhaa bandia, baada ya Tume ya Ushindani (FCC) kutangaza mpango mpya wa kurekodi za Alama za Biashara (Trademark Recordation) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwaka huu.
Mpango huo, ambao ni sehemu ya maboresho ya mfumo wa kisheria unaohusu alama za biashara, ulitangazwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, wakati wa uwasilishaji kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Bi. Ngasongwa amesema kuwa mpango huo una umuhimu mkubwa katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kujenga mazingira salama ya biashara.
“Mpango huu umebeba uzito mkubwa katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kujijengea hadhi ya kuwa taifa lenye mazingira salama ya biashara kwa kulinda wamiliki wa Alama za Biashara,Kwa niaba ya Tume ya Ushindani, kikao hiki ni fursa muhimu ya kujadili mfumo mpya unaolenga kuimarisha ulinzi na utekelezaji wa haki za alama za biashara nchini,” amesema Bi. Ngasongwa
Akitolea ufafanuzi juu ya muktadha wa mpango huo, Bi Ngasongwa amesema kuwa biashara ya bidhaa bandia ni haramu na inaendelea kuwa changamoto kubwa duniani, jambo linalodhoofisha usalama wa watumiaji na kuathiri ushindani wa haki.
Amesema Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi na kitovu cha biashara Afrika Mashariki—inatambua wajibu wake wa kukabiliana na changamoto hizo ili kulinda ustawi wa biashara halali.
“Serikali imekuwa ikiboresha mfumo wa kisheria ili kuendana na mahitaji ya sasa, ikiwemo marekebisho ya Sheria ya Alama za Biashara Sura ya 85 (R.E. 2023) pamoja na uandaaji wa Kanuni za Alama za Biashara za mwaka 2025, ambazo ndizo msingi wa mpango huu,” ameeleza
Kupitia mfumo huo mpya, wamiliki wa alama za Bidhaa au wawakilishi wao watatakiwa kurekodi alama zao kabla ya kuingiza bidhaa nchini, hatua itakayowezesha FCC na mamlaka za forodha kufanya ukaguzi madhubuti na kuzuia bidhaa bandia kuingia sokoni.
Bi. Ngasongwa amesema kuwa utekelezaji wa mpango huo utasaidia kuimarisha ulinzi kwa watumiaji, kukuza ushindani wa haki, kuongeza mapato na kuongeza uwezo wa FCC katika kutekeleza majukumu yake.
Katika kuzungumzia ushirikiano wa kimataifa, Bi. Ngasongwa amesema Tanzania inakusudia kufanya kazi kwa karibu na wanachama wa INTA pamoja na taasisi nyingine duniani ili kubadilishana uzoefu na kuimarisha mikakati ya kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka.
“Ushirikiano huu ni muhimu kuhakikisha bidhaa bandia hazipati nafasi katika masoko ya kikanda na kimataifa,” amesema
Hata hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa alama za biashara kushiriki kikamilifu katika mpango huo mpya:
“Ushiriki wenu utakuwa chachu ya kuhakikisha soko la Tanzania linaendelea kutambulika kwa uadilifu, ukweli na ushindani wa haki.”
Mpango huo utaanza kutekelezwa rasmi Desemba 1, 2025, baada ya kukamilika kwa taratibu za mwisho za utengenezaji wa mfumo husika huku FCC ikiahidi kuendelea kutoa elimu kwa wadau ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Hyatt Hoteli tarehe 19 Novemba, 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, akizungumza wakati akiwasilisha kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, akizungumza wakati akiwasilisha kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA)

Washiriki wa kikao wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA)

Washiriki wa kikao wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha kwa chama cha mawakili cha International Trademark Association (INTA).
EmoticonEmoticon