WANABUKOMBE SITAWAANGUSHA,NINA DENI KUBWA KWENU-DKT.BITEKO

October 27, 2025


Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko amewashukuru wana Bukombe kwa heshima waliyompa kipindi chote Cha kampeni Katika wilaya ya Bukombe.

Dkt. Biteko ametoa shukurani hizo Oktoba 27, 2025 wakati wa kuhitimisha  kampeni Katika Uwanja wa Igulwa, Wilayani Bukombe, Mkoani Geita.


"Nataka niwaambie wana Bukombe huwa mnanipa deni kubwa sana moyoni mwangu hamjui tu, huwa hamjui huwa najiona mmenipa stahili nisiyostahili kwa sababu kama binadamu nina mapungufu yangu mengi lakini mnanipa heshima"- amesema Biteko.

Dkt. Biteko amewashukuru pia vijana wa hamasa na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali.


"Nitafanya kila linalowezekana vijana wa hamasa wasiishie Kwenye kampeni ni vijana wetu lazima tuwakomboe. Nataka niwaambie kila wakati tukiwaita mnakuja mnanipa deni na heshima kubwa sana"



Aidha Dkt. Biteko amewakumbusha wana Bukombe Kuwa leo ilikuwa siku ya kuhitimisha kampeni katika jimbo la Bukombe na tarehe 29 wajiyokeze kwa wingi vituoni kupiga kura kwa wagombea wote wa CCM Ili Chama hicho kiendelee Kuwa madarakani.


Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »