WAKILI JUDITH KAPINGA AENDELEA KUOMBA KURA ZA CCM

October 22, 2025

 🗓️ *22.10.2025* 



📡 *Mbinga-Ruvuma* 


📌 *Ndugu.David Kihenzile ashiriki Jimbo la Mbinga Vijijini kumuombea Kura, Dkt.Samia,Dkt.Emmanuel Nchimbi,Ndugu.Judith Kapinga na Ndugu.Maurus Nchimbi*


📌 *Ndugu.Kapinga aendelea kuahidi Maendeleo*


📌 *CCM yaendelea kunadi Sera*


🔰Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia tiketi ya CCM *Wakili.Ndugu.Judith Kapinga* leo tarehe *22 Oktoba,2025* ameendelea kuomba Kura za CCM Katika Vijiji vya Ugano,Kitesa na Matekela-Kata ya Kambarage.*Ndugu.Kapinga* amezungumza na Wananchi na kupokea Changamoto mbalimbali za Maendeleo ameahidi kuzishughulikia na kusimamia Changamoto hizo iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge.



🔰Katika hatua nyingine,Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kusini, *Ndugu.David Kihenzile* ameshiriki Kampeni za Mbinga Vijijini na kumuombea Kura, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* , *Ndugu.Balozi.Dkt.Emmanuel Nchimbi,* *Ndugu.Judith Kapinga* na *Ndugu.Maurus Nchimbi* -Mgombea Udiwani Kata ya Kambarage.*Ndugu.Kihenzile* amewaomba Wananchi wa Kata ya Kambarage waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kuchagua Viongozi wanaotokana na CCM ifikapo Oktoba 29.




🔰Kwa Upande wa CCM,kupitia Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbinga, *Ndugu.Johnbosco Mkandawile* ameendelea kunadi Sera za Maendeleo za CCM na kusisitiza Wananchi waichague CCM.


         *Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la  Mbinga Vijijini,Leo tarehe 22.10.2025*

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »