Na Augusta Njoji, Handeni TC
Makundi mbalimbali ya wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Handeni yameeleza namna yalivyojipanga kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, wakisisitiza umuhimu wa kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara, wajasiriamali, na wananchi wamesema wamejipanga mapema kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura asubuhi ili kuepuka msongamano na kuhakikisha sauti zao zinasikika kupitia sanduku la kura.
Mmoja wa wajasiriamali katika Soko la Kidereko, Hadija Saidi amesema anahamasisha wenzake kupigakura mapema kwa amani na kuendelea na shughuli zao.
Kwa upande wake, Charles Mkomwa, Mfanyabiashara kata ya Kidereko, amesema uchaguzi ni fursa muhimu kwa watanzania kuchagua viongozi watakaosikiliza sauti zao.
Naye, Mwenyekiti wa Kikundi Kinamoto cha utengenezaji samani, Maulid Gumbo, amesema ana kila sababu za kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili kuchagua viongozi watakaoendelea kuchochea maendeleo ya wananchi.



EmoticonEmoticon